|
Daktari katika mpaka wa Tanzania na Kenya kwenye eneo la Namanga, Anna
Anthony, akiwapima wasafiri wanaopita katika mpaka huo, wakati
wa zoezi la
Kupima Utayari wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Kukabiliana na
magonjwa ya mlipuko mipakani, leo tarehe 13 Juni, 2019. |
Na. OWM, NAMANGA.
Kufuatia zoezi
linaloendelea mpakani mwa Tanzania na Kenya kwenye eneo la Namanga, ambalo linajikita
katika Kupima Utayari wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
Kukabiliana na magonjwa ya mlipuko mipakani, leo tarehe 13 Juni, 2019, Wataalamu
wa sekta za Afya wa Tanzania na Kenya, katika makundi tofauti wameweza
kutekeleza kwa vitendo kwa kutumia Dhana ya Afya moja katika Kupima kwa vitendo
hatua za kujiandaa na kukabili Ugonjwa wa Homa ya Bonde la Ufa.
Wataalam hao
wameweza kutathmini uwezo wa uchunguzi na usimamizi wa wagonjwa wa Homa ya
Bonde la Ufa mpakani, pamoja na kufanyia majaribio ya utekelezaji wa Mipango ya
Dharura ya Taifa na Kanda, Miongozo ya Utendaji katika kukabili na kupunguza
madhara ya ugonjwa wa Homa ya Bonde la Ufa kwa Wanyama na Binadamu.
Zoezi hilo,
linazingatia Dhana ya Afya moja ambayo hujumuisha sekta ya afya ya
binadamu, wanyamapori, mifugo na mazingira katika kujiandaa, kufuatilia na
kukabili magonjwa yanayoathiri binadamu.
MWISHO.
|
Askari Mpakani mwa
Tanzania na Kenya kwenye eneo la Namanga akimwekea kwenye mikono Dawa ya
kusafishia mikono msafiri aliyekuwa akipita katika mpaka huo wakati wa zoezi la
Kupima Utayari wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Kukabiliana na
magonjwa ya mlipuko mipakani, leo tarehe 13, Juni 2019.
|
|
Mtaalamu wa Afya
akimhudumia mmoja wa wasafiri waliokuwa
wakipita katika mpaka wa Tanzania na Kenya, kwenye eneo la Namanga aliyeigiza
kuugua, wakati
wa zoezi la
Kupima Utayari wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Kukabiliana na
magonjwa ya mlipuko mipakani, leo tarehe 13 Juni, 2019.
|
|
Baadhi ya Wataalamu
wa Afya wakimhudumia mmoja wa wasafiri waliokuwa wakipita katika
mpaka wa Tanzania na Kenya, kwenye eneo la Namanga aliyeigiza kuugua, wakati wa zoezi la Kupima Utayari wa
nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Kukabiliana na magonjwa ya
mlipuko mipakani, leo tarehe 13 Juni, 2019.
|
|
Mtaalamu wa Afya akipata maelezo kutoka kwa ndugu wa mmoja wa wasafiri waliokuwa wakipita katika
mpaka wa Tanzania na Kenya, kwenye eneo la Namanga aliyeigiza kuugua, wakati wa zoezi la
Kupima Utayari wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Kukabiliana na
magonjwa ya mlipuko mipakani, leo tarehe 13 Juni, 2019 |
|
Mtaalamu wa Afya
akinyunyizia dawa gari ambalo lilikuwa limewabeba abiria walioigiza kuumwa wakati wakitaka kupita katika mpaka wa
Tanzania na Kenya, kwenye eneo la Namanga, wakati wa zoezi la Kupima Utayari wa
nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Kukabiliana na magonjwa ya
mlipuko mipakani, leo tarehe 13 Juni, 2019.
|
|
Baadhi ya Wataalamu wa Afya
katika mpaka wa Tanzania na Kenya,
kwenye eneo la Namanga wakivua nguo za kinga mara baada ya kuwahudumia wasafiri
walioigiza kuumwa wakati wakipita kwenye
mpaka huo, wakati
wa zoezi la
Kupima Utayari wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Kukabiliana na
magonjwa ya mlipuko mipakani, leo tarehe 13 Juni, 2019.
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.