WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Kenya imesema kauli iliyotolewa na Mbunge wa jimbo la Starehe nchini humo, Charles Njagua Kanyi maarufu Jaguar si kauli ya Serikali, hivyo amewataka Watanzania wawe watulivu.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Juni 25, 2019) wakati akitoa kauli ya Serikali kuhusu kauli iliyotolewa na mbunge huyo ya kuwataka wafanyabiashara kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania waondoke nchini Kenya ndani ya saa 24.
Amesema
baada ya mbunge huyo kutoa kauli hiyo, Serikali ilianza kulifanyiakazi
jambo hilo ambapo ilimuita Balozi wa Kenya nchini Tanzania ili kujua
kama huo ni msimamo wa Serikali yao ama la, ambapo balozi huyo alimesema
ile si kauli ya Serikali ya Kenya wala wananchi.
Hata
hivyo, Waziri Mkuu amesema mbali na kuwasiliana na Balozi huyo, pia
Serikali imewasiliana na Balozi wa Tanzania nchini Kenya ili afuatilie
kuhusu kauli ya Mbunge huyo, hivyo amewataka Watanzania waendelee
kushirikiana na Wakenya.
“Si
kauli nzuri na kauli hii iliyotolewa na mtu mmoja linajenga chuki baina
ya mtu na mtu, nchi na nchi na tayari Serikali ya Kenya inalifanyia
kazi suala hili na imetuomba Watanzania tuendelee kuwa wavumilivu.”
Waziri
Mkuu amesema tamko lile linaweza kuibua chuki na vurugu miongoni mwa
nchi mbalimbali zikiwemo za Afrika Mashariki na tayari Wabunge wa Bunge
Afrika Mashariki wanaoendelea na kikao cha Bunge hilo jijini Arusha
wamepinga na kulaani kauli hiyo.
Wamesema hawatoa nafasi kwa mtu yeyote kuvuruga nchi hizo.
Hivyo,
Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwasihi Watanzania popote walipo
waendelee kuishi vizuri na Wakenya kwa kuwa wao hawana chuki na
Watanzania bali ni mtu binafsi. Pia amewatahadharisha wananchi wa Afrika
Mashariki wawe makini na kauli zao ili kuepusha vurugu.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.