*Ni vya shule ya sekondari na zahanati ya Nandangala
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea msaada wa vifaa mbalimbali kutoka benki ya NMB vyenye thamani ya sh. milioni 25.
Vifaa
hivyo ni fremu 46 za madirisha ya alminium na vioo vyake, milango 18,
mabati 56, misumari na mbao, kompyuta 10, madaftari 4,050 vyote vikiwa
na thamani ya sh. milioni 25/-.
Akipokea
msaada huo leo mchana (Jumapili, Julai 28, 2019) kwenye zahanati ya
Nandagala, wilayani Ruangwa mkoani Lindi, Waziri Mkuu amewashukuru
viongozi wa benki hiyo kwa kuamua kuchangia vifaa hivyo.
Akizungumza
na wakazi wa kijiji cha Nandagala, Waziri Mkuu ambaye ni mbunge wa
jimbo la Ruangwa, amesema mchango uliotolewa unamaanisha kazi ya
kukamilisha jengo la wodi ya wagonjwa na vyumba vya madaktari ni lazima
ifanyike haraka.
“Tunamshukuru
Mkurugenzi Mkuu wa NMB kwa msaada huu mkubwa. Hii maana yake ni kwamba
ni lazima tuharakishe kukamilisha jengohili ili tuanze kutoa huduma kwa
wananchi wa Nandagala na wa vijiji vya jirani,” alisema.
“Tulianza
na ujenzi wa zahanati kisha tukajenga jengo la upasuaji lenye wodi
mbili. Moja ya wanaume na nyingine ya wanawake ambazo kila moja ina
uwezo wa kulaza wagonjwa 20 kwa wakati mmoja.”
Jengo
hili jipya ambalo tumelianza ujenzi wake, likikamilika litakuwa na
uwezo wa kulaza wagonjwa 60. Pia kuna jengo lenye vyumba vya madaktari,
vyumba vya upasuaji na vyumba vya kujifungulia.
Waziri
Mkuu aliwataka wakazi hao wafikirie uwezekano wa kujenga wodi nyingine
na pamoja na jiko ili wagonjwa watakaokuwa wanalazwa hapo, wapate mahali
pa kupikiwa chakula.
Mapema, akitoa
taarifa ya msaada huo, Mkuu wa Idara ya Huduma za Serikali katika benki
ya NMB, Bi. Vicky Bishubo alisema kipaumbele cha benki hiyo kila mara
ni kutatua changamoto za afya na elimu kwani sekta hizo ni nguzo kuu ya
maendeleo kwa Taifa lolote.
“Vitu
hivi (mabati, madirisha ya aluminium, kompyuta na madaftari)
tunavyokabidhi leo ni moja ya ushiriki wetu katika maendeleo ya jamii na
sisi kama benki inayoongoza Tanzania tunahakikisha jamii inayotuzunguka
inafaidika kutokana na faida tunayoipata,” alisema.
Alisema
kwa mwaka huu, NMB imetenga zaidi ya shilingi bilioni moja kwa ajili ya
kuchangia maendeleo ya jamii ikiwemo kusaidia sekta ya afya na elimu.
“Mpaka ninavyoongea leo, tayari tumetoa misaada yenye thamani ya zaidi
ya millioni 600 kwa mwaka huu wa 2019 tu,” alisema.
Akielezea
kuhusu programu ya WAJIBU, Bi. Bishubo alisema hadi sasa wameshawafikia
vijana wasiopungua 42,000 katika shule za msingi na sekondari kwa
kuwapa elimu ya fedha na kujifunza kuweka akiba katika umri mdogo
kupitia programu yake ya ‘Jifunze, Jipange na Wajibika’ (WAJIBU).
“NMB
imekuwa ikiwawezesha vijana kupata elimu ya fedha katika shule za
msingi na sekondari Tanzania. Elimu hii ya fedha kwa vijana hutolewa na
wafanyakazi wetu wa benki kwenye shule zilizopo karibu na benki ikilenga
kuwafundisha vijana umuhimu wa kuweka akiba na mipango kwa ajili ya
maendeleo yao na kukidhi mahitaji ya muhimu,” alisema.
Kwa upande wake, Diwani
wa Kata ya Nandagala, Bw. Andrew Chikongwe aliishukuru benki hiyo kwa
kuwasaidia vifaa hivyo ambavyo alisema vimefika kwa wakati muafaka.
“Majengo yalikwishakamilika, yakabakia madirisha na milango, pamoja na
vifaatiba, kwa hiyo sasa hivi tunaweza kuendelea na ujenzi,” alisema.
(mwisho)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.