Sunday, September 22, 2019

MAJALIWA AWEKA JIWE LA MSINGI LA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA GEITA NA KUFUNGUA NYUMBA ZA WATUMISHI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mkoa wa Geita baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita Septemba 22, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na viongozi wa Mkoa wa Geita wakifurahia baada ya Waziri Mkuu kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita na kukagua ujenzi wa Hospitali hiyo, Septemba 22, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa   akifungua  Nyumba za Makazi za Wakuu wa Idara na Vitengo wa Secretarieti ya Mkoa wa Geita, Septemba 22, 2019. Wengine pichani kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu, Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Geita, Alhaj Said Kalidushi, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri na kulia ni Mbunge wa Viti Maalum, Vicky Kamata.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa   akikata utepe wakati alipofungua Nyumba za Makazi za Wakuu wa Idara na Vitengo wa Secretarieti ya Mkoa wa Geita, Septemba 22, 2019. Wengine pichani kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu, Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Geita, Alhaj Said Kalidushi, Mkuu wa mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel, Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani,Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri, Mbunge wa Viti Maalum, Vicky Kamata na dulia ni Waziri wa Madini, Doto Biteko.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye pia ni Mjumbe wa kamati Kuu  ya CCM, akizungumza baada ya kukagua ujenzi wa Ofisi ya CCM ya Mkoa wa Geita, Septemba  22, 2019.  Wa tatu kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Geita, Alhaj Said Kalidushi, kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel na wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.