Friday, October 11, 2019

OFISI YA WAZIRI MKUU YAINGIA MAKUBALIANO YA AWALI NA MFUKO WA KIMATAIFA WA MAENDELEO YA KILIMO –IFAD

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko akimkabidhi Mkurugenzi wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo, IFAD kwa nchi za Tanzania na Rwanda Bw. Francesco Rispoli nakala ya mkataba wa Makubaliano ya Awali ya Programu ya Kuendeleza Sekta ya Uvuvi na Uzalishaji wa Mbegu Bora za Mazao ya Kilimo mara baada ya zoezi la  uwekaji saini mkataba huo, Mikataba hiyo imesainiwa Oktoba 11, 2019 katika Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma.
Baadhi ya washiriki wa kikao cha zoezi la uwekaji wa saini kati ya Serikali na IFAD kuhusu Mkataba wa Makubaliano ya Awali ya Programu ya Kuendeleza Sekta ya Uvuvi na Uzalishaji wa Mbegu Bora za Mazao ya Kilimo wakifuatilia maelekezo ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi Dorothy Mwaluko (hayupo pichani) wakati wa kikao hicho.
Naibu Katibu Mkuu Kilimo Profesa Siza Tumbo akimsikiliza Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Sera na Shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Paul Sangawe (mwenye suti ya kaki) wakati wa zoezi la Uwekaji saini Mkataba wa Makubaliano ya Awali ya Programu ya Kuendeleza Sekta ya Uvuvi na Uzalishaji wa Mbegu Bora za Mazao ya Kilimo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko pamoja na Katibu Mkuu Uvuvi Dkt. Rashid Tamatama wakipitia Mkataba wa Makubaliano ya Awali ya Programu ya Kuendeleza Sekta ya Uvuvi na Uzalishaji wa Mbegu Bora za Mazao ya Kilimo kabla ya zoezi la utiaji saini wa mkataba huo kati ya Serikali na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo Oktoba 11, 2019.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko akizungumza wakati wa kikao cha uwekaji saini wa Makubaliano ya Awali ya Programu ya Kuendeleza Sekta ya Uvuvi na Uzalishaji wa Mbegu Bora za Mazao ya Kilimo.Mikataba hiyo imesainiwa Oktoba 11, 2019 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko pamoja na Mkurugenzi wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo, IFAD kwa nchi za Tanzania na Rwanda Bw. Francesco Rispoli wakiweka saini ya mkataba wa Makubaliano ya Awali ya Programu ya Kuendeleza Sekta ya Uvuvi na Uzalishaji wa Mbegu Bora za Mazao ya Kilimo.Mikataba hiyo imesainiwa Oktoba 11, 2019 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko akimkabidhi Mkurugenzi wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo, IFAD kwa nchi za Tanzania na Rwanda Bw. Francesco Rispoli nakala ya mkataba wa Makubaliano ya Awali ya Programu ya Kuendeleza Sekta ya Uvuvi na Uzalishaji wa Mbegu Bora za Mazao ya Kilimo mara baada ya zoezi la  uwekaji saini mkataba huo, Mikataba hiyo imesainiwa Oktoba 11, 2019 katika Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko akimkabidhi nakala ya Mkataba wa Makubaliano ya Awali ya Programu ya Kuendeleza Sekta ya Uvuvi na Uzalishaji wa Mbegu Bora za Mazao ya Kilimo Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Sera na Shughuli za Serikali wa Ofisi hiyo Bw. Paul Sangawe mara baada ya zoezi la utiaji saini mikataba hiyo.
Baadhi ya washiriki wa kikao cha zoezi la uwekaji wa saini Mkataba wa Makubaliano ya Awali ya Programu ya Kuendeleza Sekta ya Uvuvi na Uzalishaji wa Mbegu Bora za Mazao ya Kilimo wakifuatilia maelekezo ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi Dorothy Mwaluko (hayupo pichani) wakati wa kikao hicho.



No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.