· Ujumbe wa Tanzania
ukiongozwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu umeshiriki katika mkutano wa
Dunia wa wadau wa lishe duniani uliofanyika tarehe 4- 7 Novemba, 2019 jijini
Kathmandu, Nepal. Ujumbe huo ulijumuisha wataalam kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi
ya Rais TAMISEMI, Taasisi ya Chakula na Lishe, Wabunge, Wawakilishi wa wadau wa
maendeleo,Mashirika Yasiyo ya Kiserikalina Sekta binafsi. Mhe. Rais Mstaafu wa Awamu
ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
alishiriki pia katika mkutano huo na kutoa mada kuhusu hali ya utekelezaji wa
Masuala ya Lishe nchini na mafanikio yaliyopatikanakuanzia kipindi alipokuwa madarakani.
·
Mkutano huo ulifunguliwa na Makamu wa Waziri
Mkuu wa nchi hiyo Dkt. Ishwor Pokharel kwa niaba ya Mhe. Waziri Mkuu wa Nepal
Khagda Prasad Oli. Washiriki wapatao 1,200 kutoka nchi mbalimbali waliweza
kushiriki katika mkutano huo.
·
Lengo la kushiriki Mkutano
huo ni kubadilishana uzoefu na kujadiliana masuala mbalimbali yanayohusu lishe
duniani ikiwa ni pamoja na changamoto zinazokabili ulimwengu katika kupambana
na lishe ili kuimarisha juhudi hizo na kuhakikisha kuwa utapiamlo unatokemezwa
duniani ifikapo mwaka 2030.
·
Katika mkutano huo uliojumuisha warsha 25
pamoja na mambo mengine ya kuimarisha juhudi za utekelezaji wa hatua za
kumaliza tatizo la lishe duniani, kuwa na mifumo bora ya uzalishaji wa chakula,
mbinu za kukabiliana na Utapiamlo wa Uzito uliokithiri,Upatikanaji na matumizi
ya takwimu,utekelezaji wa pamoja wamikakati ya kumaliza changamoto ya lishe,
uimarishaji wa juhudi katika kanda za ushirikiano na misaada ya kiufundi katika
kuimarisha juhudi za kupambana na utapiamlo.
Ushiriki wa Tanzania katika mkutano huo
umekuwa na manufaa ikiwa ni pamoja na
o
Kuimarisha ushirikiano na nchi wanachama.
Aidha, Tanzania imekubaliana na nchi za Peru na Zambia kubadilishana uzoefu
katika mbinu za kupambamba na utapiamlo ili kuongeza kasi ya utekelezaji wa
Mikakati Jumuishi wa Lishe wa Taifa,
o
Kujenga uelewa wa wadau wa Lishe kuhusu
mbinu za kupambana na utapiamlo ambapo Waheshimwa Wabunge watasaidia kuimarisha
juhudi za kujenga uelewa kwa jamii juu ya umuhimu wa kupambana na changamoto
hiyo,
o
Vile vile, ujumbe wa Tanzania ulikutana na Bi.
Gerda Verburg (Mratibu wa Msukumo wa Masuala ya Lishe Duniani (SUN Movement
Coordinator) na Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa) ambae ameahidi
kusaidia Tanzania katika maandalizi ya Mkakati Jumuishi wa Lishe wa Taifa 2021
– 2026 ambao unatazamiwa kuanza kuandaliwa kuanzia mwaka 2020.
· Katika mkutano huo nchi wanachama
zimekubaliana kuainisha hatua zitakazochukuliwa kuimarisha juhudi za utekelezaji
wa Mikakati ya Kupambana na Utapiamloikiwa ni pamoja na kutenga fedha. Hatua
hizo zitakuwa ni sehemu ya maazimio katika Mkutano wa Nutrition For Growth
utakaofanyika mwaka 2020 nchini Japan.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.