Na. OWM, DAR ES SALAAM
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe.
Jenista Mhagama leo tarehe 26 Novemba,
2019 anatarajia kutangaza utaratibu mpya wa kununua Nyumba za gharama nafuu 480 za Mradi wa Buyuni
zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya Ilala, Chanika -Buyuni, Jijijni Dar es Salaam.
Akiongea mara baada ya kumaliza kukagua mradi huo wa nyumba zinazomilikiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa
Umma (PSSSF), tarehe 25 Novemba 2019, Mhe. Mhagama amebainisha kuwa atatoa utaratibu
huo mpya wa namna ya kununua nyumba hizo zilizo wazi ili wananchi waweze
kunufaika kwa kupata makazi bora na salama.
Mfuko
wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), unaratibiwa na Ofisi ya
Waziri Mkuu, na umeanzishwa na Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ya mwaka
2018, Jukumu kuu la mfuko huo ni kukusanya michango na kulipa mafao ya kustaafu
kwa watumishi wa umma.
|
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu,
Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akiongozana na
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi , Vijana ,Ajira na Watu wenye Ulemavu)
Andrew Massawe (Kulia) na kushoto kwake Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Hosea Kashimba,
kukagua Nyumba za gharama nafuu 480 za Mradi wa Buyuni
zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya Ilala, Chanika -Buyuni, Jijijni Dar es Salaam |
|
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista
Mhagama akiteta jambo na Katibu Mkuu
Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi , Vijana ,Ajira na Watu wenye Ulemavu) Andrew
Massawe wakati alipokagua Nyumba
za gharama nafuu 480 za Mradi wa Buyuni zilizopo katika Halmashauri ya
Wilaya Ilala, Chanika -Buyuni, Jijijni
Dar es Salaam.
|
|
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista
Mhagama akisalimiana na mkazi wa Buyuni, Benjamini Mvungi wakati
alipokagua Nyumba za gharama
nafuu 480 za Mradi wa Buyuni zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya Ilala,
Chanika -Buyuni, Jijijni Dar es Salaam.
|
|
Muonekanao wa mojawapo ya nyumba Nyumba za gharama nafuu 480 za Mradi wa Buyuni zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya Ilala, Chanika -Buyuni, Jijijni Dar es Salaam zinazonilikiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF). |
|
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na mmoja wa wananchi waliofanikiwa kununua Nyumba za gharama nafuu za Mradi wa Buyuni zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya Ilala, Chanika -Buyuni, Jijijni Dar es Salaam |
|
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista
Mhagama akisalimiana na mmoja wa wananchi waliofanikiwa kununua Nyumba za gharama nafuu za Mradi wa Buyuni zilizopo
katika Halmashauri ya Wilaya Ilala, Chanika -Buyuni, Jijijni Dar es Salaam wengine ni Katibu Mkuu
Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana ,Ajira na Watu wenye Ulemavu) Andrew
Massawe na Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Hosea Kashimba.
|
|
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na mmoja wa wananchi waliofanikiwa kununua Nyumba za gharama nafuu za Mradi wa Buyuni zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya Ilala, Chanika -Buyuni, Jijijni Dar es Salaam.
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.