WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa ameongoza wakazi wa jiji la Dar es Salaam na
maeneo mengine kwenye mazishi ya Mfanyabiashara na Mwanazuoni Maarufu wa
dini ya Kiislam, Alhaj Aziz Massanga (Zingizi), yaliyofanyika katika
makaburi ya Msasani.
Alhaj
Zingizi amefariki dunia Jumatano, Novemba 27 jijini Johanesburg nchini
Afrika Kusini alikikwenda kwa ajili ya kupatiwa matibabu. Marehemu
Alhaj Zingizi alikuwa akisumbuliza na ugonjwa wa saratani ya kibofu.
Akizungumza
baada ya mazishi hayo yaliyofanyika jana jioni (Ijumaa, Desemba 29,
2019), Waziri Mkuu aliwaasa wananchi kumuenzi marehemu Alhaj Zingizi kwa
kufanya mambo mema kama alivyokuwa akiyafanya enzi za uhai wake.
“Marehemu Zingizi alikua ni mtu mwenye kusaidia jamii kwa hali na mali.”
“Marehemu
ametenda mengi mema katika msikiti wake na jamii iliyomzunguka.
Alisaidia wenye mahitaji, hivyo na sisi hatuna njia nyingine ya kumuenzi
marehemu bali ni kutenda mema kwa jamii hususani kwa kuwajali watu
wenye shida ili wale waliokua wananufaika wasione pengo kubwa. ”
Waziri
Mkuu alisema kuwa Serikali ipo pamoja na viongozi wote wa dini na wala
wasisite kuijulisha pale wanapopatwa na jambo lolote ipo tayari
kushirikiana nao kwa namna moja au nyengine.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.