WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa ameshiriki katika mazishi ya mwanasiasa mkongwe na
Mwenyekiti wa zamani wa CCM wa wilaya ya Ruangwa, Bw. Kaspar Selemani
Mmuya yaliyofanyika kwenye Kitongoji cha Mtakuja, kijiji cha Nangumbu
wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.
Akizungumza
katika mazishi hayo, Waziri Mkuu amesema marehemu Bw. Mmuya enzi za
uhai wake alitoa ushirikiano mzuri kwa viongozi na wananchi wa Ruangwa
kwa ujumla na wakati wote alikuwa tayari kutoa ushauri katika masuala
ya siasa na uongozi.
Waziri
Mkuu ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Ruangwa mkoani Lindi, ameshiriki
katika mazishi ya mwanasiasa huyo mkongwe yaliyofanyika leo (Jumanne,
Novemba 5, 2019). Amesema marehemu alikuwa kiongozi makini na mwenye
kupenda ushirikiano.
“Marehemu
alikuwa kiongiozi wangu na mshauri wa masuala ya siasa na kijamii
wakati wote nilipomuomba au yeye mwenyewe alipoona iko haja ya kufanya
hivyo. Wakati wote wa uhai wake alikuwa tayari kusikiliza na kushauri, “
alisisitiza Waziri Mkuu .
Mazishi hayo pia yamehudhuriwa na Naibu Waziri wa Nchi OWM - Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana, Anthony
Mavunde, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi, Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa
wa Lindi, Fadhili Juma, Viongozi wa chama cha Walimu Tanzania wa Mkoa
wa Lindi na Wilaya ya Ruangwa pamoja na viongozi wa Serikali na vyama
vya Siasa.
Mapema leo asubuhi Mheshimiwa Majaliwa alishiriki katika kikao cha Bunge kwenye ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.