NA. MWANDISHI WETU
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi Mhe. William Lukuvi ametoa wito kwa wakuu wa mikoa kuhakikisha
wanawalinda wamiliki wa ardhi ambao wapo kisheria.
Waziri Lukuvi alitoa agizo hilo jana
Desemba 05, 2019 wakati wa mkutano wa mashauriano kati ya Serikali, wafanyabiashara
na wawekezaji uliofanyika mjini Kibaha na kuongozwa na Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Mhe. Angellah Kairuki.
wawekezaji na wafanyabiashara
walipata nafasi kufikisha malalamiko yao ambayo ni kikwazo katika shughuli zao.
Waziri Lukuvi alibainisha kuwa
Mkoa wa Pwani unaongoza kwa uvamizi ambapo Wilaya ya Bagamoyo inatajwa kuwa
kinara.
Lukuvi alisema, wakuu hao wa mikoa wana
askari wanaweza kuwaondoa waliojimilikisha ardhi kinyume cha sheria.
“Tumieni mabaraza ya ardhi yaliyoundwa
kisheria kuondoa wavamizi kwenye maeneo ambayo yanamilikiwa kisheria"
alisema.
Naye Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet
Hasunga aliwahimiza wawekezaji kuwekeza kwenye kilimo cha alizeti na michikichi
kwa ajili ya mafuta ya kupikia.
Waziri Hasunga alisema, kuna uhitaji
wa mafuta ya kula tani 650 ambazo kiasi cha shilingi billion 675 zimekuwa
zikitumika kuagiza mafuta kutoka nje ya nchi.
Alisema, upande wa mafuta wawekezaji
ni wachache, hivyo wakipatikana wawekezaji wengi wataokoa fedha ambazo zinaenda
nje ya nchi zibaki hapa nchini.
Aidha kuhusiana na mikopo kwa
wakulima alisema, kwa anayetaka kulima awasiliane na mfuko wa pembejeo pamoja
na benki ya kilimo kupata taratibu.
Akihitimisha mkutano huo Waziri
Kairuki amewahahakikishia kuwa majibu yote ambayo hayajapatikana papo hapo
wizara inaandaa bango kitita ambalo malalamiko na changamoto zote zitajumuishwa
na kupelekwa ngazi zote akiwemo Mhe. Rais na Waziri Mkuu.
Amewapongeza wawekezaji wazao ambao
wameweza kusajili miradi zaidi ya 70 kwa mwaka huu pekee huku akizitaka taasisi
za kibenki kuondoa urasimu katika kutoa mikopo kwa wawekezaji wazawa badala
yake waweke mazingira rafiki.
Mkutano
huo wa mashauriano wa siku moja ulihudhuriwa na mawaziri watatu pamoja na
manaibu Mawaziri tisa, Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Angellah Kairuki, Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi
, Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga, Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, Naibu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mussa Sima, Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii,Constantine Kanyasu ,Naibu Waziri wa Mambo wa Ndani ya Nchi,Hamad
Masauni, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, Naibu Waziri wa
Nishati, Subira Mgalu, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, Naibu
Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Antony Mavunde (Kazi, Vijana na Ajira), Naibu Waziri Ofisi ya
Rais Tamisemi, Josephat Kandege.
Pia ulihudhuriwa na Taasisi wezeshi,
mwenyekiti wa wafanyabiashara Mkoa wa Pwani, mwenyekiti wa wafanyabiashara
ndogondogo machinga, wawekezaji pamoja na viongozi wengine kutoka Halmashauri
na Mkoa.
=MWISHO=
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.