Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Menejimenti ya Maafa, imezishauri Kamati za Usimamizi wa Maafa katika mikoa 8 na vijiji 184 vinavyopatikana katika wilaya 24 zilizopo katika mikoa ya Kagera, Geita,
Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Manyara na Tanga, ambapo Mradi wa Bomba la Mafuta utatekelezwa kuuweka Mradi huo katika Mipango yao ya kujiandaa na kukabiliana na Maafa ili kuhakikisha mradi huo hauthiriwi na majanga yanayoweza kutokea.
Kwa mujibu wa sheria ya Usimamizi wa maafa Na. 7 ya mwaka 2015,
inaainisha majukumu ya kamati za usimamizi wa Maafa kuanzia ngazi ya
Kijiji hadi mkoa, ambapo kwa mujibu wa sheria hiyo, jukumu la msingi ni kutoa
taarifa za tahadhari ndani ya eneo husika, Kuratibu na kusimamia shughuli za
usimamizi wa maafa na operesheni za dharura ndani ya Kijiji wilaya au
mkoa, pamoja na kutafuta rasilimali kwa ajili ya usimamizi wa maafa katika
ngazi husika.
Akiongea mara baada ya kutembelea eneo la kwenye peninsula ya
Chongoleani karibu na bandari ya Tanga ambapo utekelezaji wa Mradi huo utatekelezwa,
Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy
Matamwe amefafanua kuwa Kamati za maafa zinalo jukumu la kuchukua tahadhari ya
namna ya kuhakikisha majanga yanayoweza kuuathiri mradi huo yanakuwa katika
mipango yao ya menejimenti ya maafa ili faida zitakazotokana na utelelezaji wa
mradi huo zinakuwa endelevu.
Kwa upande wake, Kaimu
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Noel Kazimoto ameeleza kuwa utekelezaji wa
mradi huo utafungua fursa za kiuchumi kwa watanzania hivyo ni dhahiri kuwa eneo
la Chongoleani litakuwa na mwingiliano mkubwa wa watu na shughuli nyingi za
kiuchumi na kijamii zitakuwa zikiendeshwa, kwa kuwa wananchi ni wadau wa
menejimeti ya maafa kupitia kamati za menejimenti za maafa kuanzia ngazi ya vijiji, wataendelea
kuelimishwa juu ya majanga yanayoweza kuuathiri
mradi huo ili waweze kuhakikisha mradi unakuwa endelevu.
Kwa mujibu wa Tovuti rasmi ya Kampuni
inayojenga mradi huo, East African Crude Oil Pipeline www.eacop.com. Kampuni hiyo inabainisha kuwa wanao
mpango unaohakikisha utelezaji wa mradi huo unazingatia majanga na maafa wakati
wa kupanga, kujenga na kuendesha Bomba, ambapo Mpango huo
unahakikisha kwamba, katika tukio la dharura linaloweza kutokea, hatua za
haraka, zinachukuliwa.
Mradi
wa Bomba la Mafuta Ghafi unatekelezwa kwa ubia
wa ujenzi na uendeshaji kwa kushirikisha kampuni za Total ya Ufaransa, CNOOC ya
China, Tullow ya Uingereza na Serikali za Tanzania na Uganda. Mafuta
ghafi yatasafirshwa kutoka Kabaale katika Wilaya ya Hoima nchini Uganda hadi
bandari ya Tanga nchini Tanzania. Mradi wa Bomba hilo una umbali wa
kilometa 1,445 ambapo kilometa 298 zitakuwa nchini Uganda, na kilometa 1,147
zitakuwa nchini Tanzania.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.