Baadhi ya waandishi wa Habari wakifuatilia Mkutano wa Waandishi wa Habari na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Mohamed Aboud Mohamed (hayupo pichani) wakati wa akifafanua kuhusu Mkutano wa kwanza wa Kamati ya Mawaziri wenye dhamana ya masuala ya Menejimenti ya Maafa kwa Nchi Wanachama Jumuiya ya MaendeIeo Kusini mwa Afrika, tarehe 16 Februari 2020, Ukumbi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) Mnazi mmoja. |
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Ndugu
Wananchi,
Kama
tunavyoelewa kuwa kufuatia Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Maendeleo
Kusini mwa Afrika (SADC), uliofanyika mwezi Agosti 2019 ambapo, Mhe. Dkt. John Joseph Pombe Magufuli, Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipokea rasmi uenyekiti wa jumuiya hiyo, hali
hiyo imepelekea mkutano mbalimbali ya
Kisekta kufanyika hapa Tanzania.
Ndugu
Wananchi,
Mkutano huu unafanyika kutokana na umuhimu mkubwa wa
Mawaziri wa nchi wanachama wa SADC wanaohusika na masuala ya maafa kukutana
kwa lengo la kujadili na kuweka mikakati ya pamoja ya namna bora ya kukabiliana
na matukio ya maafa yanayoukabili ukanda
huu yakiwemo vimbunga, mafuriko, ukame, na hata ajali za baharini ambayo
yamekuwa yakisababisha athari kubwa kwa maisha ya watu na mali.
Sote ni mashuhuda athari za Kimbunga Idai na Keneth
vilivyotokea katika nchi za Madagascar, Malawi, Msumbiji na Zimbabwe
vilipelekea vifo vya maelefu ya watu na wengine kutoonekana kabisa na
kupelekea mahitaji ya kiasi cha dola
bilioni 10 za Kimarekani kwa ajili ya kurejesha hali.
Ndugu Wananchi,
Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania itakuwa mwenyeji wa Mkutano wa Kwanza wa Kamati ya
Mawaziri wanaohusika na Menejimenti ya Maafa kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya
Maendeleo Kusini mwa Afrika utakaofanyika katika hoteli ya Madinat Al Bahri
Mbweni, tarehe 18 – 21 Februari, 2020, hapa Zanzibar. ambapo Kaulimbiu ya Mkutano
huu: “Ushiriki wa Kisekta kwenye Kupunguza madhara ya maafa ni njia bora ya kujenga
uhimili katika ukanda wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa
Afrika” (SADC)
Ndugu
Wananchi,
Mkutano
huu unakuja kipindi ambacho nchi nyingi wanachama katika ukanda huu zimekuwa
zikiathiriwa na majanga ya asili mara kwa mara na kusababisha madhara makubwa. Hali
iliyoonesha wazi umuhimu wa mashirikiano ya kikanda katika kukabiliana na
maafa ili kupunguza athari za maafa,
kukuza uwezo wa kujiandaa na kukabiliana
kwani mara nyingi athari zinazotokana na majanga ya kimaumbile yakiwemo ukame,
mafuriko, maradhi ya mlipuko na mengineyo, hupelekea vifo kuharibu miundombinu
muhimu ikiwemo barabara na hudumaza msingi za jamii kama vile afya na elimu na
kupelekea gharama kubwa katika kurejesha
hali baada ya maafa kutokea.
Ndugu
Wananchi,
Katika
hatua ya kujenga mataifa yenye uhimili katika kukabiliana na maafa, SADC
imefanikiwa katika kuimarisha mifumo ya tahadhari za mapema inayoendana na
majanga ya Hali ya hewa, kuandaa vikao vya mwaka kwa nchi wananchama kwa ajili
ya kujikinga, kujiandaa na kukabiliana na maafa pamoja na kuandaa mipango ya dharura na kutoa mafunzo
ya utafutaji na uokozi kwa majanga ya baharini kwa nchi wananchama.
Ndugu Wananchi,
SADC
imetekeleza program ya ufanyaji wa tathmini na uchambuzi wa usalama wa chakula kwa
nchi wananchama 14 zilizoathiriwa na majanga yanayoendana na hali ya hewa
yakiwemo ukame, imeandaa mpango na mkakati wa pamoja kwa ajili ya kujikinga na
kukabili maafa. Mikakati yote hiyo ni kwa ajili ya kupunguza athari za maafa
katika kanda hii. Mnamo mwaka 2017-2018 takribani watu wapatao milioni 7
waliathiriwa na maafa idadi ambayo ni ndogo ikilinganishwa na watu milioni 17 walioathirika
katika miaka ya 2015-2016.
Kwa
upande wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imekamilisha kuandaa nyaraka zote
muhimu katika masuala ya kukabiliana na maafa ikiwemo sheria ya Usimamizi wa
Maafa ya Kitaifa Na. 7 ya 2015, Sheria ya
Kukabiliana na Maafa Zanzibar No. 1 ya mwaka 2015, Sera za Kukabiliana na
Maafa, Mipango ya Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa na Mkakati wa Mawasiliano
Wakati wa Maafa na rasimu ya Mkakati wa Kukabiliana na Maafa pamoja kuanzisha
vituo vya mawasiliano na operesheni za dharura na vituo vya uokozi hasa kwa
majanga ya baharini.
Mkutano huu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa
Afrika unalenga katika kushajihisha juhudi zilizopo katika kukabiliana na maafa
kwa kuziwezesha nchi wanachama kuandaa mikakati ya uhimili kutokana na athari
za maafa, kuandaa mkakati wa kujiandaa na kukabiliana na maafa. Aidha, mikakati
hii itaisaidia sana juhudi za ukanda huu katika kupunguza athari za maafa na
kuimarisha uwezo wa nchi husika katika kukabiliana na maafa pamoja na kurejesha
hali baada ya maafa kutokea.
Ndugu Wananchi,
Nachukua
fursa hii kuwakaribisha waandishi wa habari na wananchi kwa ujumla kufuatilia
juu ya Mkutano huu ambao utakuwa ni fursa tosha ya kutangaza utalii wetu na
kukuza uchumi wan chi pamoja na kupunguza athari za maafa.
Ahsanteni
kwa kunisikiliza.
Mhe. Mohamed Aboud Mohamed
Mhe. Mohamed Aboud Mohamed
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa wa Pili wa Rais Zanzibar
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.