Tathmini
ya Uharibifu na Mahitaji Baada ya Maafa, ni mfumo wa kimataifa uliokubaliwa
kuainisha madhara, hasara za kiuchumi, na gharama
za mahitaji ya kurejesha hali baada ya maafa kutokea.
Mfumo huo hutumiwa na mataifa mengi duniani katika kuainisha athari hizo kwa kuzingatia aina ya maafa wanayoyapata, ambapo serikali
hutambua ni kwa kiwango gani maafa yamekuwa yakiathiri maendeleo ya kijamii na
kiuchumi pamoja na pato la taifa na hivyo kuweka mikakati thabiti ya kuzuia na
kupunguza madhara.
Ofisi
ya Waziri Mkuu, Idara ya menejimenti ya maafa imeratibu zoezi la kufanya
tathmini kwa kutumia mfumo huo kwa mara ya kwanza hapa nchini mkoani Tanga kwa
kuwa mkoa huo ni miongoni mwa mikoa iliyopata maafa ya mafuriko na kupata
madhara makubwa katika sekta za Kilimo, Afya, Elimu, Mazingira na Miundombinu
kufuatia athari ya mvua za vuli za mwezi Oktoba hadi
Desemba, mwaka jana (2019).
Akiongea wakati
wa kufuatilia uratibu wa tathmini hiyo jijini Tanga, Mkurugenzi Idara ya
Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe, amefafanua kuwa Serikali kwa kushirkiana na benki ya dunia mwaka jana walitoa
mafunzo kwa watalaam wa sekta mbalimbali kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa
kitaalamu wa kufanya tathmini hiyo na
kwa sasa wanafanya tathmini kwa vitendo mkoami humo, lengo ni kuwa na wataalamu wenye uwezo huo kuanzia
ngazi za msingi za menejimenti ya maafa.
“Mfumo huu utatusaidia kupata taarifa ya kina ya madhara, matokeo na rasilimali
zinazohitajika katika kurejesha hali kwa
kila sekta iliyoathiriwa, pia taarifa zake zinasaidia kuandaa mkakati wa kitaifa
na wa kimkoa wa kurejesha hali na hatimaye Kuweka mfumo wa Kitaifa na kimkoa
wa kurejesha hali kwa kipindi cha sasa
na baadaye.”Amesisitiza Kanali, Matamwe.
Kanali Matamwe, amefafanua
kuwa Tathmini hiyo ni shirikikshi kwa maana ya sekta ya umma na sekta binafsi
ambapo wadau wa masuala ya maafa hushirikishwa yakiwemo mashirika ya umoja wa
mataifa, Benki ya dunia na Mashirika
yasiyo ya kiserikali.
Aidha, ameeleza kuwa zoezi hilo linalenga kujenga uwezo kwa vitendo kwa
wataalamu kutoka katika ngazi ya wizara, mkoa na wilaya katika kufanya tathmini
ya uharibifu na mahitaji kutokana na maafa kwa kila sekta.
Naye mwenyekiti wa Kamati ya
Usimamizi wa Maafa, kwa mujibu wa sheria ya Maafa Na.7 ya mwaka 2015, ambaye
ni Katibu Tawala wa mkoa, akiwakilishwa na
Kaimu Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga, Noel Kazimoto amefafanua kuwa mkoa huo
mvua za msimu uliopita wa vuli wa mwaka jana, mkoa huo ulipata athari
zinazojumuisha vifo, uharibifu wa miundombinu ya barabara, maji, na miundombinu
ya kutolea huduma za elimu na afya, pia
kubomoka kwa makazi na kuharibika kwa mfumo wa maisha ya kijamii ya kila
siku.
Aidha,
ameongeza kuwa, Tathmini hiyo itaujengea
uwezo mkoa huo kuandaa mipango na mikakti ya muda mfupi, muda wa kati na muda
mrefu katika kurejesha hali katika ubora zaidi, kwa kuwa imejikita katika kuangalia madhara
yaliyojitokeza katika sekta ya elimu, afya, kilimo, makazi, miundombinu pamoja
na huduma za maji na usafi. Vilevile tathmini hiyo imeangalia masuala mtambuka,
kama vile mazingira, masuala ya upunguzaji wa athari za maafa na usawa wa
kijinsia.
Tathmini
hiyo iliyofadhiliwa na Benki ya Dunia, kwa kuratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu,
Idara ya Menejimenti ya Maafa chini ya Uongozi wa mtaalam mshauri kutoka nchini
Ghana Seth Vordzorgbe, imewahusisha wataalamu
kutoka katika ngazi ya wizara, mkoa na wilaya pamoja na wadau wa sekta binafsi
na mashirika yasiyo ya kiserikali.
MWISHO
Mtaalamu
Mshauri kutoka nchi Ghana, Seth Vordzorgbe, akisisitiza umuhimu wa Tathmini ya Uharibifu na Mahitaji Baada ya
Maafa kutokea, Jijini Tanga, wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalam
wanaohusika na Tathmini kabla ya kufanya tathmini hiyo ambayo huainisha madhara, hasara za kiuchumi, na gharama za mahitaji ya
kurejesha hali baada ya maafa kutokea.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.