Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi,
Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama, ametoa maagizo sita
kwa waratibu na wadau wa Programu ya mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa
kutumia teknolojia ya Kitalu Nyumba “Greenhouse”na kuwataka kutekeleza, kwa
wakati na ufanisi maagizo yake yanayojikita katika kuimarisha
usimamizi na uendeshaji wa mafunzo hayo ili yawe na ubora zaidi na tija kwa
vijana.
Waziri
Mhagama ameagiza
kufanyika maamuzi ya haraka yatakayowezesha vijana katika halmashauri ambazo
bado mradi huo haujafika wanafikiwa. Aidha, Fedha zote zilizokusanywa na vijana
katika awamu ya kwanza ya mafunzo hayo zikaguliwe na vijana washirikishwe ili
waweze kutoa taarifa ya idadi ya mazao waliyozalisha na kiwango walichoweza
kuuza.
Akitoa
magizo hayo leo, Machi 11 2020 kwa kikao
kilichowakutanisha vijana, Wadau,Waratibu ambao ni Ofisi ya
Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ofisi ya Rais TAMISEMI,
Wizara ya Viwanda na Biashara, Wizara ya Kilimo, Tume ya Taifa ya Umwagiliaji
na wakandarasi ambao walijenga vitalu nyumba, amewagiza kuanzishwa
mfumo wa ufuatiliaji ambao utakuwa na taarifa ya utekelezaji wa majukumu.
"Kuanzia
sasa ni lazima mikopo kwa vijana ipatikane kwa wakati, nataka
upatikanaji wa mikopo ambayo itawasaidia vijana hao kuanzisha vitalu nyumba
vyao, pia tengenezeni mfumo wa ukusanyaji mapato na matumizi. Wakandarasi
waliojenga vitalu nyumba katika halmashauri 84 awamu ya kwanza fanyeni
marekebisho kwenye vitalu nyumba ambavyo vimekuwa na matatizo.
Nataka usimamizi na uendeshaji wa programu ya mafunzo ya kilimo cha kisasa
kwa kutumia teknolojia ya Kitalu Nyumba “Greenhouse” uwe chachu ya
kuongeza ajira kwa vijana katika sekta ya kilimo" amesisitiza Mhagama.
Waziri
Mhagama amefafanu akuwa, Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ina nia ya dhati
ya kuwawezesha vijana kupitia programu mbalimbali inazoazisha kwa lengo la
kuwasaidia vijana kuondokana na changamoto ya ajira.
“Serikali ina lengo
la kufikisha ujuzi huo wa kilimo cha kisasa katika halmashauri zote za Tanzania
bara kwa kuwa asilimia 63 ya fursa za ajira zinapatikana kwenye kilimo na tena
maeneo ya vijijini,” alisema Mhagama
Waziri
Mhagama, amebainisha kuwa, Ofisi ya Waziri Mkuu ambayo ndio yenye dhamana
na masuala ya vijana iliamua kupitia ilani ya uchaguzi ibara ya 6 kifungu (a)
inayosema kuhamasisha kilimo kupitia kauli mbiu ya Kilimo Kwanza kwa
kuwawezesha wakulima kupata mafunzo ya kilimo cha kisasa, pembejeo, zana za
kisasa na wataalamu wa ugani pamoja na mbinu za kuyafikia masoko ya uhakika ya
mazao yao, ambao ulipelekea kutambua umuhimu wa mchango wa vijana hasa waliopo
vijijini ndipo mradi huu wa Kilimo cha kisasa kwa kutumia teknolojia ya Kitalu
Nyumba ulianzishwa kwa lengo la kuwezesha vijana,” amesema Mhagama.
“Mataifa
makubwa mengi yaliyoendelea wamekuwa wakitumia kilimo cha aina hiyo kwa lengo
la kulima kisasa, kuongeza thamani ya mazao, kupata masoko endelevu na la
uhakika na kulima kwa tija, hivyo tukiwawezesha vijana wetu watanufaika na
kilimo hicho na sekta hiyo italeta tija katika kukuza uchumi wa nchi,” alieleza
Mhagama.
Waziri
Mhagama amewataka vijana kutumia ujuzi waliopata katika mafunzo hayo ili waweze
kusimamia mradi huo vizuri na wajenge moyo wa kuthubutu katika kuwasaidia
vijana wenzao kupata ujuzi wa mafunzo hayo ya kilimo cha kisasa.
Wakati
huo huo, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu) Bw. Andrew Massawe amesema kuwa ameyakupokea maagizo hayo na kuahidi
kuyafanyia kazi ili programu hiyo ya mafunzo ya kilimo cha kisasa iweze kuwa
endelevu.
“Ofisi ya
Waziri Mkuu iliona umuhimu wa kushirikiana na , Ofisi ya Rais TAMISEMI, Wizara
ya Viwanda na Biashara, Wizara ya Kilimo, Tume ya Taifa ya Umwagiliaji,
wakandarasi pamoja na Vijana ili kutathmini utekelezaji wa mradi huo na kuona
namna ya kukabili changamoto ambazo zilijitokeza, mafanikio yaliyopatikana ili
kuona namna bora ya kuimarisha mafunzo hayo,” amesema Massawe.
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa Ajira na Ukuzaji Ujuzi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Ally Msaki
ameelezea maazimio waliyofikia pamoja na wadau katika kuimaarisha usimamizi na
uendeshaji wa mafunzo hayo
"Pamoja na
kuangalia namna bora ya kuendesha mafunzo haya, tumemua kuwa tutasimamia
uwepo wa utaratibu maalum wa makusanyo, utunzaji na matumizi ya fedha,
kuwezesha vijana kuwa na ujuzi wa kuongeza thamani ya mazao, kuelezea wananchi
mafanikio yaliyopatikana kupitia mradi huo wa kilimo cha Kitalu nyumba,kuwezesha
vijana kufanya kilimo biashara na uwepo wa muendelezo wa kutoa mafunzo na
kuongeza vitalu nyumba katika kila halmashauri" amesitiza Msaki.
Naye
Mmoja wa wanufaika wa Programu hiyo Bw. Festo Masiba ameishukuru Ofisi ya
Waziri Mkuu kwa kuwapatia mafunzo hayo ambayo yamewajengea ujuzi mkubwa wa
kuweza kulima kwa tija.
“Tunaishukuru
Serikali kwa kutuamini sisi vijana na kutuwezesha kupata mafunzo ya Kilimo bora
kwa kutumia eneo dogo na upatikanaji wa mazao ni mwingi, tumeweza kukua
kiuchumi na tunaujuzi wa kuwajengea wadau wengine vitalu nyumba,” alisema Masiba .
MWISHO
Baadhi ya Wakuu wa Idara kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu wakifuatilia mijadala wakati wa mkutano huo. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.