Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri
Mkuu Bi:Dorothy Mwaluko awakumbusha
watumishi wa Ofisi yake wajibu wa majukumu yao wawapo kazini na kuwataka
kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa kila moja kwenye eneo lake.
Katibu Mkuu amesema
hayo kwenye mkutano na watumishi wa Ofisi
yake katika kukamilisha wiki ya Utumishi wa uuma kwa mwaka 2020, iliyobeba
kauli mbiu isemayo “jukumu la mtumishi wa umma
katika kujenga na kudumisha amani iliyopo miongoni mwa jamii”
Katika kikao hicho
aliwakumbusha kuwa na nidhamu ya kutosha katika uwajibikaji wa kazi na kila
mtumishi kuzingatia sheria na taratibu za kazi awapo kazini.
Aidha aliwakumbusha pia
watumishi kukamilisha ujazaji fomu za upimaji utendaji kazi yani (OPRAS)
ambacho ndicho kipimo sahihi cha uwajibikaji wa mtumishi wa umma.
Naye Mkurugenzi wa Utawala
na Rasilimali watu Bw:Greyson Mwaigombe
alimshukuru Katibu Mkuu kwa niaba ya
watumishi wote na kuahidi kutekeleza yale yote aliyo elekeza.
Mkutano huo ulifanyika
katika ukumbi wa hazina jijini Dodoma uli hudhuriwa na watumishi wote wa Ofisi
ya Waziri Mkuu na mada mbalimbali zilitolewa za kuwakumbusha watumishi wajibu wao
na kuzingatia maadili ya kazi na Usalama mahala pakazi.
Watumishi wa Ofisi ya
Waziri Mkuu wakimsikiliza Katibu Mkuu Bi Dorothy Mwaluko katika Mkutano wa Maadhimisho
ya Wiki ya Utumishi wa Umma.
|
Watumishi wa Ofisi ya
Waziri Mkuu wakimsikiliza Katibu Mkuu Bi Dorothy Mwaluko katika Mkutano wa Maadhimisho
ya Wiki ya Utumishi wa Umma.
|
Watumishi wa Ofisi ya
Waziri Mkuu wakimsikiliza Katibu Mkuu Bi Dorothy Mwaluko katika Mkutano wa Maadhimisho
ya Wiki ya Utumishi wa Umma.
|
MWISHO
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.