Monday, July 13, 2020

WAZEE NACHINGWEA WAMCHANGIA RAIS DKT. MAGUFULI, WAZIRI MKUU AWASHUKURU AAHIDI KUFIKISHA SALAM

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akimsikiliza Mzee Hamis Kambona (wapili kutoka kushoto) wakati akipokea  mchango wa Shilingi laki moja kutoka kwa wazee wa wilaya na Nachingwea kwa ajili ya kumchangia, Rais Dkt.  John Magufuli katika kampeni za uchaguzi wa  mwaka huu, kwa kutambua mchango mkubwa katika kuiletea Tanzania maendeleo. Tukio hilo lilifanyika kwenye uwanja wa Ndege wa Nachingwea wakati Waziri Mkuu alipowasili akiwa jiani kwenda Ruangwa, Julai 13, 2020.

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akipokea risiti ya malipo ya shilingi Laki moja kutoka kwa Mzee Abdalah Saidi Kaliondima, kwa ajili ya kumchangia, Rais Dkt. John Magufuli katika kampeni za uchaguzi wa mwaka huu, kwa kutambua mchango mkubwa katika kuiletea Tanzania maendeleo, Tukio hilo lilifanyika kwenye uwanja wa Ndege wa Nachingwea wakati Waziri Mkuu alipowasili akiwa jiani kwenda Ruangwa, Julai 13, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akipokea risiti ya malipo ya shilingi Laki moja kutoka kwa Mzee Abdalah Saidi Kaliondima, kwa ajili ya kumchangia, Rais Dkt. John Magufuli katika kampeni za uchaguzi wa mwaka huu, kwa kutambua mchango mkubwa katika kuiletea Tanzania maendeleo, Tukio hilo lilifanyika kwenye uwanja wa Ndege wa Nachingwea wakati Waziri Mkuu alipowasili akiwa jiani kwenda Ruangwa, Julai 13, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiwashukuru wazee wa wilaya na Nachingwea baada ya kupokea risiti ya malipo ya shilingi Laki moja walizozitoa kwa ajili ya kumchangia, Rais Dkt.  John Magufuli katika kampeni za uchaguzi wa  mwaka huu, kwa kutambua mchango mkubwa katika kuiletea Tanzania maendeleo. Tukio hilo lilifanyika kwenye uwanja wa Ndege wa Nachingwea wakati Waziri Mkuu alipowasili akiwa jiani kwenda Ruangwa, Julai 13, 2020.

Wednesday, July 8, 2020

MAJALIWA ATEMBELEA TAASISI YA UTAFITI WA KILIMO NALIENDELE

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama maziwa yanayotokana na korosho wakati alipotembelea  Taasisi ya Utafiti wa Kilimo, Naliendele, Mtwara, Julai 7, 2020. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa. 

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Taasisi  ya Utafiti wa Kilimo Naliendele, Dr. Fortunus Kapinga (kushoto) kuhusu utafiti wa mbegu bora za mhogo unaofanyika katika Taasisi hiyo, Julai 7, 2020. Wa pili kushoto ni Mtafiti Mkuu katikaTaasisi hiyo, Bernadetha Kimata. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Berbadetha Kimata ambaye ni  Mtafiti Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo, Naliendele ya Mtwara  kuhusu utafiti wa mbegu za mhogo wakati alipoitembelea, Julai 7, 2020. Katikati ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais  Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni Mstaafu, George Mkuchika. 


Tuesday, July 7, 2020

TUTAFUFUA VYUO NA VITUO VYA UTAFITI WA KILIMO-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli itahakikisha kwamba vyuo na vituo vyote vya utafiti wa kilimo nchini vinafufuliwa, hivyo Wizara ya Kilimo inatakiwa kutenga fedha za kutosha katika bajeti yake kila mwaka. 

“Nataka niwahakikishie Serikali yenu imedhamiria kuimarisha kilimo pamoja na utafiti wake. Mwezi mmoja uliopita nilikuwa Mlingano mkoani Tanga kuona shughuli za utafiti wa zao la mkonge lakini miezi miwili iliyopita nilikuwa kwenye chuo kipya tulichokianzisha kule Kigoma cha utafiti cha Kihinga na nimeona kazi yake na tutapata mafanikio makubwa.”

Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo jana (Jumanne, Julai 07, 2020) alipotembelea Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Naliendele iliyoko mkoani Mtwara kwa lengo la kujionea shughuli za utafiti wa mazao mbalimbali ya kilimo zinazoendelea kituoni hapo. 

Alisema Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefurahishwa na kazi nzuri za utafiti wa mazao mbalimbali zinazofanywa na vituo vya utafiti na matokeo mazuri ya utafiti huo kwa wakulima wa Watanzania.

Waziri Mkuu alisema “Azma ya kusimamia na kuona vyuo vya utafiti vinafanya kazi yake vizuri ni pamoja na maboresho haya kwanza wizara husika lazima itambue  kuwa vyuo vya utafiti vinamchango mkubwa, wizara kwenye bajeti zake ipeleke fedha nyingi kwenye utafiti na tuone utafiti unagundua mambo na yale yanayogunduliwa yaende yakafanyiwe kazi.”

Vilevile, Waziri Mkuu alisema idadi ya udahili wa wanafunzi katika vyuo vya kilimo itaongezwa ili wapatikane wataalamu na watafiti wengi ambao wanahitajika sana katika kufanikisha mapinduzi ya kilimo nchini.

Tasisi ya hiyo ya Kilimo ya Naliendele ni miongoni mwa vituo vya utafiti wa kilimo nchini ambavyo vimewawezesha wakulima wengi kujiongezea tija na kujikwamua kiuchumi baada ya kutumia mbegu bora zinazozalishwa kituoni hapo kama za korosho, ufuta na muhogo.
  
(mwisho)

Friday, July 3, 2020

WAZIRI MKUU AFUNGUA MAONESHO YA 44 YA BIASHARA

*Asema Serikali itaendelea kuviwezesha viwanda vidogo, vya kati
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kuweka mazingira rafiki na wezeshi ili kuviwezesha viwanda vidogo sana, vidogo na vya kati kukua na kufanya kazi kwa tija zaidi.

Ametoa kauli hiyo leo jioni (Ijumaa, Julai 3, 2020) wakati akifungua rasmi Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (44TH DITF) yaliyoanza Julai mosi, 2020 kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu ambaye amefungua maonesho hayo kwa niaba ya Rais, Dkt. John Pombe Magufuli amesema ili nchi iweze kuwa na mafanikio makubwa, taasisi za kifedha hazina budi kuweka mikakati ya kutoa huduma ya mikopo rafiki ili kuwezesha ukuaji wa viwanda kwa kuzingatia viwanda vidogo na vya kati ikiwemo vinavyoratibiwa na SIDO katika kila mkoa.

“Taswira hii ya maendeleo ya sekta ya viwanda inafanana na taswira ya maendeleo ya viwanda katika nchi karibu zote duniani. Kwa mfano, Japan, viwanda vidogo sana, vidogo na vya kati vinachukua takribani asilimia 99 ya sekta ya viwanda; Kenya asilimia 98; Malaysia asilimia 97.3; Indonesia asilimia 99.9; Canada asilimia 98 na Ujerumani asilimia 99.”

Amesema Serikali inaendelea kuimarisha sekta ya biashara na viwanda nchini ili kuchochea maendeleo ya nchi kwa ujumla. Akielezea mafanikio ya Serikali katika kipindi cha miaka mitano, Waziri Mkuu amesema: “Jumla ya viwanda vipya 8,477 vimejengwa na kuchangia kuzalisha ajira mpya 482,601… mchango wa sekta ya viwanda katika Pato la Taifa kwa mwaka 2019 ulikua kwa asilimia 8.5 ikilinganishwa na asilimia 8.05 mwaka 2018, sawa na ongezeko la asilimia 0.45.”

Amesema mchango huo, ni matokeo ya kuongezeka kwa shughuli za uzalishaji wa bidhaa viwandani nchini ambao unaendelea kuimarika na kukua vizuri. Akitoa mfano, Waziri Mkuu amesema mwaka 2019, bidhaa za viwanda zilikuwa na thamani ya sh. trilioni 10.2 ikilinganishwa na sh. trilioni 9.6 mwaka 2018 ambao ukuaji wake ni sawa na asilimia 5.8.

Kuhusu viwanda vidogo na biashara ndogo, Waziri Mkuu amesema sekta hiyo inaendelea kutoa mchango mkubwa katika pato la taifa wa wastani wa asilimia 35 kwa mwaka. “Kwa mwaka 2019/2020, jumla ya miradi 304 inayohusiana na ujenzi wa viwanda imesajiliwa ambayo inatarajiwa kuongeza jumla ya ajira 11,793.”

Amesema SIDO imeratibu na kuhudumia viwanda vidogo vipya 1,400 vinavyotoa ajira 4,200. “Sekta hii muhimu imeajiri Watanzania zaidi ya milioni tisa ikiwa ni ya pili kwa sekta za kiuchumi katika kutoa ajira baada ya sekta ya kilimo,” ameongeza. 

Amesema maendeleo ya uwekezaji katika sekta ya viwanda nchini yameongeza uzalishaji wa bidhaa mbalimbali ikiwemo bidhaa za chuma, saruji, vigae, nguo na mavazi, ngozi na bidhaa za ngozi, kusindika nyama, chakula, mbogamboga na matunda, maziwa, mafuta ya kula, sukari, vifungashio, mbolea, dawa za binadamu, sabuni na sigara pamoja na ubanguaji wa korosho.  

Kwa upande wa biashara, Waziri Mkuu amesema utekelezaji wa Blueprint for Regulatory Reform to Improve Business Environment umewezesha maboresho ya tozo 173 ambapo kati ya tozo hizo, tozo 163 zimefutwa na tozo kero 10 zimepunguzwa viwango.

“Kati ya tozo zilizofutwa, 114 ni za sekta ya kilimo na mifugo, tano ni za Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), 44 za Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mamlaka za Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), utalii, maji, uvuvi na iliyokuwa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA).”

Amesema tozo zilizopunguzwa za GCLA, zimewezesha kuhamisha jukumu la usimamizi wa masuala ya chakula kutoka iliyokuwa TFDA kwenda TBS ili kuondoa muingiliano wa majukumu. “Maboresho hayo yamesaidia kuondoa urasimu na kupunguza gharama za kufanya biashara,” amesisitiza.

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na washiriki wa maonesho hayo, Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa alisema kati ya mwaka 2015 na 2019, viwanda 8,477 vilianzishwa katika maeneo mbalimbali nchini ambapo kati ya hivyo, viwanda 201 ni vikubwa, 460 ni vya kati, 3,406 ni vidogo na 4,410 ni vidogo sana.

“Uwepo wa viwanda vyetu vya ndani, ulitusaidia hata wakati wa janga la corona tuliweza kutengeneza barakoa, mavazi ya watoa huduma, vitakasa mikono na bidhaa nyingine nyingi.”

Akisisitiza matumizi ya bidhaa zinazozalishwa nchini, Waziri Bashungwa amesema: “Hakuna soko endelevu na lenye uhakika kama soko la ndani. Kwa hiyo, wazalishaji wa ndani wazalishe bidhaa zenye ubora, na Watanzania wapende kununua bidhaa za ndani. Kwa njia hiyo, tutaimarisha soko la ndani na kulinda viwanda vyetu,” alisisitiza.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TanTrade, Dkt. Ngw’anza Kamata alisema kutokana na changamoto ya COVID 19, mwaka huu idadi ya washiriki imepungua kiasi. “Washiriki wa ndani wamepungua kutoka 3,250 hadi 2,837 wakati wa washiriki wa nje nao wamepungua kutoka 520 hadi 43,” alisema.  

(mwisho)

MAJALIWA AFUNGUA MAONYESHO YA BIASHARA YA KIMATAIFA YA DAR ES SALAAM

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipunga baada ya kukata utepe wakati alipofungua  Maonyesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya  Dar es salaam , Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam, Julai 3, 2020. Wengine pichani kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda, Mhandisi Stella Manyanya, Waziri wa Biashara na Viwanda, Innocent Bashungwa,Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro na kulia ni Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mashine ya kuranda na kuweka urembo kwenye mbao wakati alipotembelea banda la Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogovidogo (SIDO) kabla ya kufungua Maonyesho  ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya  Dar es salaam , Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam, Julai 3, 2020. Kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa na wa tatu kulia ni Kaimu Mkurugenzi  wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogovidogo (SIDO), Shoma Kibende.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kufungua Maonyesho  ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Nnee ya Dar es salaam, Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam, Julai 3, 2020.Wengine pichani kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda, Mhandisi Stella Manyanay, Waziri wa Biashara na Viwanda, Innocent BashungwaNaibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro na kuliani Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Maonyesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya  Dar es salaam , Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam, Julai 3, 2020.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Maonyesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya  Dar es salaam , Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam, Julai 3, 2020.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Maonyesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya  Dar es salaam , Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam, Julai 3, 2020.