Ofisi
ya Waziri Mkuu imefanya mafunzo ya kujenga uwezo wa kutekeleza majukumu
waliyokasimiwa kwa maafisa 36 kutoka idara na vitengo vya ofisi hiyo. Mafunzo hayo
ya wiki moja yamefanyika kuanzia tarehe 24 hadi 28 Agosti 2020, Jijini Dodoma,
ambapo Wakala wa Serikali ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) waliendesha mafunzo
hayo kwa ufadhili wa Shirika la Chakula Duniani.
Lengo
la mafunzo hayo lilikuwa ni kujenga uwezo kwa maafisa wake katika maeneo ya Uchambuzi
wa Sera, Ufuatiliaji na Tathmini ya Sera na Uandishi wa taarifa. Mafunzo hayo pia
yamewezesha maafisa hao kuongeza umahiri wa utekelezaji majukumu waliyokasimiwa
kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ya mwaka 1977, Ibara 52, ambapo jukumu la msingi la Ofisi hiyo ni
kuratibu na kusimamia shughuli za Serikali katika sekta zote na Bungeni pamoja
na majukumu mengine yaliyoainishwa kwenye Tangazo la Serikali Na. 144 Aprili
2016, lililofanyiwa mabadiliko tarehe 7 Oktoba 2017.
Akiongea wakati akifunga rasmi mafunzo hayo, leo tarehe 28
Agosti jijini Dodoma, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia elimu,
Gerald Mweli hakusita kueleza furaha yake juu ya utaratibu wa Ofisi ya
Waziri Mkuu kuendesha mafunzo kwa watumishi yanayolenga kujenga uwezo wa kutekeleza
majukumu waliyokasimiwa.
“Nimevutiwa sana na mbinu zilizotumika katika ufundishaji wa
mafunzo haya. Nimeambiwa katika kuhakikisha mnapata mbinu na umahiri kwenye Tathmini
na Ufuatiliaji wa Sera, mmepitia Mpango Jumuishi wa Kitaifa wa masuala ya Lishe.
Naelewa Ofisi ya Waziri Mkuu ndiyo mratibu wa mpango huu na sisi TAMISEMI
tunatekeleza. Nakusudia na mimi Kufanya mafunzo kama haya kwa watumishi wa
wizara yangu” amesisitiza Mweli.
Kwa
upande wake, Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji), Dorothy Mwaluko
amelishukuru Shirika la Chakula Duniani
kwa ufadhili wa mafunzo hayo, ambapo matokeo ya mafunzo hayo ni Ofisi hiyo kuwa na mfumo bora wa uratibu wa
shughuli za serikali kutokana na mamlaka
iliyonayo kikatiba ya kuratibu shughuli zote za Serikali pamoja na masuala
mtambuka ikiwemo masuala ya lishe.
“Mafunzo
haya yatakuwa ni mwendelezo kwa maafisa
wote na menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, lengo ni kuongeza umahiri kwa uchambuzi
bora wa sera, ufuatiliaji na tathmini ya sera pamoja na kuwa na mfumo bora wa mawasiliano ya utekelezaji wa
majukumu kwa idara zote ndani ya Ofisi, pia na mfumo bora wa uratibu wa
shughuli za serikali” amesisitiza Mwaluko.
Awali
akiongea kabla ya kufungwa kwa mafunzo hayo, Kaimu mkurugenzi mkuu wa Wakala ya Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLA),
Dickson Mwanyika amefafanua kuwa mafunzo hayo yaliyoendeshwa kwa utaratibu wa
mijadala washiriki walipata fursa ya kufahamu mbinu za kimkakati za
uchambuzi wa Sera na kanuni za uratibu wa Sera, njia za kufanya ufutiliaji na
tathmini, vigezo vya kuzingatia katika kufanya tathmini na ufuatiliaji pamoja
na namna ya kuandika taarifa na muundo
wa taarifa.
Wakiongea
kwa nyakati tofauti kwenye mafunzo hayo, baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo, Frank
Mwega na Elilanga Kaaya wamebainisha
kuwa mafunzo hayo yamekuwa msaada mkubwa kwa washiriki katika kuwajengea uwezo.
Aidha, wameshauri uendelevu wa mafunzo ya namna hiyo yenye kuwajengea uwezo
watumishi kwenye maeneo ya utendaji.
MWISHO.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji), Dorothy
Mwaluko akisisitiza kuwa Ofisi hiyo itaendelea kutoa mafunzo ya kujenga uwezo
kwa maafisa wa ofisi hiyo, lengo ikiwa ni kutekeleza majukumu waliyokasimiwa
kwa ufanisi na weledi. Mafunzo hayo ya siku tano, yameendeshwa na Wakala ya
Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLA) na kufungwa leo jijini Dodoma tarehe 28
Agosti, 2020.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji), Dorothy
Mwaluko, akimshukuru Afisa Lishe kutoka Shirika la Chakula Duniani, Neema
Shosho, kwa ufadhali wa mafunzo ya kujenga uwezo kwa maafisa wa ofisi hiyo,
lengo ikiwa ni kutekeleza majukumu waliyokasimiwa. Mafunzo hayo ya siku tano, yameendeshwa
na Wakala ya Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLA) na kufungwa leo jijini Dodoma tarehe
28 Agosti, 2020.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi
ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia elimu, Gerald Mweli akisisitiza umuhimu wa ubora wa
Uratibu wa shughuli za serikali wakati akifunga rasmi mafunzo ya kujenga uwezo kwa
maafisa wa ofisi hiyo leo jijini Dodoma tarehe 28 Agosti 2020, kushoto kwake ni Katibu Mkuu Ofisi ya
Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji), Dorothy Mwaluko na kulia ni Kaimu mkurugenzi mkuu wa Wakala ya Mafunzo kwa njia ya mtandao
(TaGLA) Dickson Mwanyika,
Baadhi Maafisa wa Ofisi ya
Waziri Mkuu wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu
Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia
elimu, Gerald Mweli wakati akifunga rasmi mafunzo ya kujenga uwezo kwa
maafisa wa ofisi hiyo leo jijini Dodoma tarehe 28 Agosti 2020, Mafunzo hayo ya siku tano, yameratibiwa
na Ofisi ya Waziri Mkuu na kuendeshwa na Wakala ya Mafunzo kwa njia ya mtandao
(TaGLA).
Mchumi Mwandamizi Ofisi ya Waziri Mkuu. Frank Mwenga, akieleza umuhimu wa
mafunzo ya kujenga uwezo kwa maafisa wa
ofisi hiyo wakati wa kufunga mafunzo hayo leo jijini Dodoma tarehe 28 Agosti 2020, Mafunzo hayo ya siku tano, yameratibiwa
na Ofisi ya Waziri Mkuu na kuendeshwa na Wakala ya Mafunzo kwa njia ya mtandao
(TaGLA).
Mchumi Ofisi ya Waziri Mkuu. Elilanga Kaaya, akieleza umuhimu wa mafunzo ya kujenga uwezo kwa maafisa wa ofisi
hiyo wakati wa kufunga mafunzo hayo leo jijini
Dodoma tarehe 28 Agosti 2020, Mafunzo
hayo ya siku tano, yameratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu na kuendeshwa na Wakala
ya Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLA).
Naibu Katibu Mkuu Ofisi
ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia elimu Gerald
Mweli, akimkabidhi cheti Afisa Habari Mwandamizi Ofisi ya
Waziri Mkuu Isabela Katondo, baada ya
kuhitimu mafunzo ya Uchambuzi wa Takwimu, Ufuatiliaji na Tathmini ya Sera na Uandishi wa Taarifa, leo
jijini Dodoma tarehe 28 Agosti 2020, Mafunzo
hayo ya siku tano, yameratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu na kuendeshwa na Wakala
ya Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLA).
Naibu Katibu Mkuu Ofisi
ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia elimu Gerald
Mweli, akimkabidhi cheti Afisa Utumishi Ofisi ya Waziri Mkuu
Herman Chando, baada ya kuhitimu mafunzo ya Uchambuzi wa Takwimu,
Ufuatiliaji na Tathmini ya Sera na
Uandishi wa Taarifa, leo jijini Dodoma tarehe 28 Agosti 2020, Mafunzo hayo ya siku tano, yameratibiwa
na Ofisi ya Waziri Mkuu na kuendeshwa na Wakala ya Mafunzo kwa njia ya mtandao
(TaGLA).
Washiriki wa mafunzo ya Uchambuzi wa Takwimu, Ufuatiliaji na Tathmini ya Sera na Uandishi wa Taarifa
wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu Ofisi
ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia elimu, Gerald Mweli (mwenye tai), kulia kwake ni Katibu Mkuu Ofisi ya
Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji), Dorothy Mwaluko, leo jijini Dodoma tarehe 28 Agosti 2020, Mafunzo hayo ya siku tano, yameratibiwa
na Ofisi ya Waziri Mkuu na kuendeshwa na Wakala ya Mafunzo kwa njia ya mtandao
(TaGLA).
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.