Saturday, January 9, 2021

SERIKALI KUTUMIA MBINU YA MAKAMBI KWA WANAFUNZI WASICHANA KUWAWEZESHA KUFIKIA MALENGO

Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania imepanga kutumia Mbinu ya kuwaweka kwenye Kambi wanafunzi wasichana balehe wanaotoka kwenye kaya masikini,  kwa kuwapa Mafunzo ya namna ya Kujikinga na VVU na UKIMWI, Stadi za Maisha na Mafunzo ya masomo ya Sayansi na Hisabati, ili waweze kufanya vizuri kwenye masomo, kujitambua, kujiamini na kuweza kutimiza malengo yao.

Kwa mara ya Kwanza Ofisi ya Waziri Mkuu, kupitia Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania imeratibu kambi ya majaribio ya siku tano, kuanzia tarehe 4-8 Januari, 2021, Jijini Dodoma, kwa  wanafunzi wasichana 105 wa shule 18 kutoka kaya masikini zilizo chini ya mpango wa TASAF za Halmashauri ya wilaya ya Bahi, jijini Dodoma.

Akiongea wakati wa kufunga kambi hiyo Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Bi. Dorothy Mwaluko amebainisha kuwa kufanikiwa kwa majaribio ya kambi hiyo kutawezesha serikali kupitia ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania, kuendesha kambi za namna hiyo kwenye Halmashauri nyingine hapa nchini ili kuweza kuwasaidia wanafunzi wasichana balehe wanaotoka kaya masikini kuweza kutimiza malengo yao.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda, amefafanua kuwa wilaya hiyo wamepanga kuwa na utaratibu wa kuwa na kambi za wanafunzi wasichana balehe kila baada ya miezi sita kwa wanafunzi 1,324 walioko ndani ya shule. Aidha, ameeleza kuwa wilaya hiyo tayari inao mfuko wa elimu wa Halmashauri ambao utawaendeleza kieleimu wanafunzi hao hadi elimu ya chuo kikuu.

Naye Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mwitikio wa Taifa, Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania, Audrey Njelekela, amefafanua kuwa Kambi hiyo ni sehemu ya Utekelezaji wa mradi wa TIMIZA MALENGO unaowalenga Wasichana Balehe na Wanawake Vijana walioko ndani na nje ya shule kutimiza malengo yao. Kwa sasa mradi huo unatekelezwa katika Halmashauri 10 nchini za mikoa ya Dodoma, Singida na Morogoro ambapo mikoa ya Tanga na Geita imeongezwa kwenye mradi huo. Amesisitiza  kuwa Mradi wa kambi utatekelezwa pia katika Halmashauri za mikoa hiyo.

Wakiongea kwa nyakati tofauti baada ya kufunga Kambi hiyo Mratibu wa Mradi huo  wa Kambi Salum Kilipamwambu ambainisha kuwa Tafiti za elimu ya sekondari zinaonesha wanafunzi wasichana wa sekondari wamekuwa wakishindwa kuhitimu masomo yao kwa kukosa uelewa na kutojitambua na kujiamini, naye, Mwajuma Hamisi kutoka shule ya sekondari Kigwe, Bahi jijini Dodoma, ameeleza kuwa mafunzo hayo yamewawezesha kujitambua, kujiamini na wameongeza weledi kwenye masomo ya sayansi na Hisabati hivyo wataweza kufanya vizuri kwenye masomo na hatimaye kuweza kutimiza elimu.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Bi. Dorothy Mwaluko akizungumza na wanafunzi wa kike kutoka shule 18 za Wilaya ya Bahi walio katika mpango wa kuhudumia kaya masikini, wakati wa kufunga kambi ya siku tano katika shule ya Sekondari ya Dodoma iliyolengo kuwapa Mafunzo ya namna ya Kujikinga VVU na UKIMWI, Stadi za Maisha na Mafunzo ya masomo ya Sayansi na Hisabati.
Baadhi ya wanafunzi wa kike kutoka shule 18 za Wilaya ya Bahi walio katika mpango wa kuhudumia kaya masikini, wakifuatilia shughuli za kufunga kambi ya siku tano katika shule ya Sekondari ya Dodoma waliyoshiriki kwa lengo la kuwapa Mafunzo ya namna ya Kujikinga na VVU na UKIMWI, Stadi za Maisha na Mafunzo ya masomo ya Sayansi na Hisabati
Mkuu wa wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda, akizungumza na wanafunzi wa kike kutoka shule 18 za Wilaya ya Bahi walio katika mpango wa kuhudumia kaya masikini, wakati wa kufunga kambi ya siku tano katika shule ya Sekondari ya Dodoma iliyolengo kuwapa Mafunzo ya namna ya Kujikinga VVU na UKIMWI, Stadi za Maisha na Mafunzo ya masomo ya Sayansi na Hisabati.
Baadhi ya wanafunzi wa kike kutoka shule 18 za Wilaya ya Bahi walio katika mpango wa kuhudumia kaya masikini, wakionesha vipaji vyao wakati wa kufunga kambi ya siku tano katika shule ya Sekondari ya Dodoma, lengo ni kuwapa Mafunzo ya namna ya Kujikinga na VVU na UKIMWI, Stadi za Maisha na Mafunzo ya masomo ya Sayansi na Hisabati\
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mwitikio wa Taifa, Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania, Audrey Njelekela akieleza umuhimu wa kambi kwa wanafunzi wa kike kutoka shule 18 za Wilaya ya Bahi walio katika mpango wa kuhudumia kaya masikini, kambi hiyo imefanyika jijini, Dodoma ikihusisha wasichana 105, kutoka Halmashauri ya Bahi.
Baadhi ya wawezeshaji wa Kambi wanafunzi wasichana balehe wanaotoka kwenye kaya masikini, wakifuatilia shughuliza kufunga kambi hiyo, Jijini Dodoma, Mafunzo ya namna ya Kujikinga na VVU na UKIMWI, Stadi za Maisha na Mafunzo ya masomo ya Sayansi na Hisabati, yalifundshwa.
Mwakilishi wa shirika la Peae corps, Tanzania Bw. Allanse Mbilu akieleza kuwa shirika hilo lipo tyari kushirikiana na Serikali kupitia TACAIDS katika utekelezaji wa Mradi wa kuwaweka kwenye Kambi wanafunzi wasichana balehe wanaotoka kwenye kaya masikini, wakati wa kufunga kambi hiyo ya siku tano jijini Dodoma
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Bi. Dorothy Mwaluko akimkabidhi, Irine Emmanuel Mallya kutoka shule ya sekondari Kigwe, Bahi jijini Dodoma, kwa ushiriki hodari kwenye kambi ya wanafunzi wasichana balehe wanaotoka kwenye kaya masikini, wakati wa kufunga kambi hiyo ya siku tano jijini Dodoma.
Wanafunzi walioshiriki kwenye kambi ya wanafunzi wasichana balehe wanaotoka kwenye kaya masikini, wakisoma risala yao wakati wa kufunga kambi hiyo ya siku tano jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Bi. Dorothy Mwaluko akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi walioshiriki kambi ya wanafunzi wasichana balehe wanaotoka kwenye kaya masikini, wakati wa kufunga kambi hiyo ya siku tano jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Bi. Dorothy Mwaluko akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wawezeshaji walioshiriki kufundisha wanafunzi wakati wa kambi ya wanafunzi wasichana balehe wanaotoka kwenye kaya masikini, wakati wa kufunga kambi hiyo ya siku tano jijini Dodoma.
Read More