Friday, February 12, 2021

Mpango wa kukabiliana na Vitendo vya kihalifu katika Maziwa na Bahari kuu nchini wazinduliwa

 

Serikali ya Tanzania kupitia Ofisi ya waziri Mkuu kwa kushirikiana serikali ya Japan na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), wamezindua mpango wa Kukabiliana na Vitendo vya Kiuhalifu katika Maziwa na Bahari nchini. Mradi huo utaimarisha juhudi za kupambana na vitendo vya kihalifu hususani; uvuvi haramu, uhamiaji haramu, usafirishwaji wa nyara za serikali pamoja na upitishwaji wa madawa ya Kulevya.

Akiongea wakati wa kuuzindua Mradi huo Jijini Dodoma, leo tarehe 12 Februari 2021, Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Bi. Dorothy Mwaluko, amefafanua kuwa mpangoi huo utatekelezwa kwa kipindi cha mwaka mmoja, lengo lake ni kuimarisha usalama katika maziwa na bahari na utanufaisha wavuvi kwa kuwapa elimu ya njia bora za uvuvi na kujenga miundombinu ya kisasa ya kukausha samaki.

 

“Serikali inakusudia kutekeleza mpango huu kwa ufanisi kwa kuhakikisha wadau wa mradi huu wananufaika na utekelezaji wake. Kupitia mradi huu serikali itaweza kununua boti ili kuimarisha doria katika bahari na hivyo kuweza kupunguza vitendo vya kihalifu. Ni matarajio yangu mpango kazi huu  utakidhi mahitaji tulionayo ya kuainisha mfumo wa kitaasisi, makundi ya wadau na wajibu wao katika kupambana na uhalifu katika maziwa na bahari.” Amesisitiza Mwaluko

 

Awali akiongea katika uzinduzi huo; Mwakilishi kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bi. Christine Musisi,  ameeleza kuwa wanaamini Maendeleo ya Uchumi na ustawi wa watu hauwezi kupatikana bila kuwa na ulinzi imara katika maziwa na bahari pamoja na uboreshwaji wa  maisha ya watu wanaoishi katika maeneo ya maziwa na bahari. Ameongeza kuwa Kupitia mpango huo wataiwezesha serikali ya Tanzania kufanikisha malengo yake ya kuimarisha uchumi wa bluu.

 

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah ameeleza kuwa mpango  huo ni muhimu kwa nchi kwa kuwa utajikita katika kupambana na uvuvi haramu ambao umekuwa ukisabbisha uharibifu wa rasilimali katika Bahari. Ameongeza kuwa kwa sasa nchini asilimia 30 hadi 40 ya samaki wanaovuliwa na wavuvu wadogo wadogo wanaharibika, hivyo ujio wa mpango huo utakuwa ni mkombozi kwa wavuvi kwa kuboresha miundo mbinu ya kukausha samaki ambayo itawezesha kuongeza thamani samaki na kupata soko la kikanda.

Naye Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya ndani, Christopher Kadio, ameongeza kuwa mpango huo utaisiadia wizara hiyo katika uwezo wa kudhibiti vitendo vya kiuhalifu hususan kwenye meneo ya ufukwe wa bahari na maziwa. Amesisitiza kuwa utekelezaji wa mpango huo utawezesha katika kuimarisha uchumi  wa nchi na ustawi wa jamii.

Utekelezaji wa mpango huo utasimamiwa na Kamati ya Usimamizi ambayo pamoja na kusimamia jukumu la utekelzaji wa Mradi huo, kamati itakuwa na jukumu la kuidhinisha mpango kazi  na taarifa ya utekelezaji. Mwenyekiti wa Kamati hiyo ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu). Wajumbe wengine wa Kamati hiyo ni Makatibu wakuu wa Wizara ya TAMISEMI, Ofisi ya Makamu wa Rais, Feddha na Mipango; Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Mambo ya ndani, Maliasili na Utaliina Ujenzi na Uchukuzi.

Ends-

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Bi. Dorothy Mwaluko (kushoto) akikata utepe kwenye vitabu vya Mpango wa Utekelezaji wa  kukabiliana na Vitendo vya Kihalifu katika Maziwa na Bahari kuu nchini, wengine ni kutoka kulia; Mwakilishi kutoka Shirika la UNDP, Bi. Christine Musisi, Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya ndani, Christopher Kadio na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah, Jijini Dodoma, tarehe 12 Februari 2021.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Bi. Dorothy Mwaluko (kushoto) akionesha  Kitabu cha  Mpango wa Utekelezaji  wa Mradi wa kukabiliana na Vitendo vya Kihalifu katika Maziwa na Bahari kuu nchini, wengine ni kutoka kulia; Mwakilishi kutoka Shirika la UNDP, Bi. Christine Musisi, Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya ndani, Christopher Kadio na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah, Jijini Dodoma, tarehe 12 Februari 2021.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Bi. Dorothy Mwaluko (kushoto) akikabidhi   Mpango wa Utekelezaji wa kukabiliana na Vitendo vya Kihalifu katika Maziwa na Bahari kuu nchini, kwa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah na  Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya ndani, Christopher Kadio anayeshuhudia ni Mwakilishi kutoka Shirika la UNDP, Bi. Christine Musisi,  Jijini Dodoma, tarehe 12 Februari 2021.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Bi. Dorothy Mwaluko (kushoto)  akionesha Mpango wa Utekelezaji wa kukabiliana na Vitendo vya Kihalifu katika Maziwa na Bahari kuu nchini, wengine ni kutoka kulia; Mwakilishi kutoka Shirika la UNDP, Bi. Christine Musisi, Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya ndani, Christopher Kadio na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah, Jijini Dodoma, tarehe 12 Februari 2021.

Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Shughuli za serikali, Ofisi ya Waziri Mkuu, Paul Sangawe,  akifafanua jambo juu ya Mpango wa Utekelezaji wa kukabiliana na Vitendo vya Kihalifu katika Maziwa na Bahari kuu nchini, wakati wa uzinduzi wa mradi huo unaofadhiliwa na Serikali ya Japan na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP),  Jijini Dodoma, tarehe 12 Februari 2021.

Baadhi ya wadau  Mpango wa Utekelezaji wa kukabiliana na Vitendo vya Kihalifu katika Maziwa na Bahari kuu nchini wakifuatilia uzinduzi wa mradi huo unaofadhiliwa na Serikali ya Japan na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na kuratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu,  Jijini Dodoma, tarehe 12 Februari 2021.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah (katikati) akileleza umuhimu Mpango wa Utekelezaji wa kukabiliana na Vitendo vya Kihalifu katika Maziwa na Bahari kuu nchini, utakavyoboresha miundombinu ya kisasa ya kukausha samaki,  wakati wa uzinduzi wa mradi huo, kulia kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya ndani, Christopher Kadio na, Jijini Dodoma, tarehe 12 Februari 2021.

Baadhi ya wadau  wa Utekelezaji Mpango wa  kukabiliana na Vitendo vya Kihalifu katika Maziwa na Bahari kuu nchini wakifuatilia uzinduzi wa mpango huo, Jijini Dodoma, tarehe 12 Februari 2021. Mradi utaimarisha juhudi za kupambana na vitendo vya kihalifu hususani; uvuvi haramu, uhamiaji haramu, usafirishwaji wa nyara za serikali pamoja na upitishwaji wa madawa ya Kulevya.

Baadhi ya wajumbe wa sekretarieti walioshiriki katika shughuli ya uzinduzi wa Mpango wa Utekelezaji wa kukabiliana na Vitendo vya Kihalifu katika Maziwa na Bahari kuu nchini Jijini Dodoma, tarehe 12 Februari 2021, mradi huo unaoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Bi. Dorothy Mwaluko (wa pili kushoto walio kaa) akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Mpango wa  kukabiliana na Vitendo vya Kihalifu katika Maziwa na Bahari kuu nchini, wengine; kulia kwake ni ; Mwakilishi kutoka Shirika la UNDP,Bi. Christine Musisi, Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya ndani, Christopher Kadio (wa kwanza kulia walio kaa) na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah(wa kwanza kushoto walio kaa), Jijini Dodoma, tarehe 12 Februari 2021.


Read More