Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama amesema serikali ya wamu ya tano
inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika kuhakikisha wananchi wake
wanakuwa na lishe bora, inakamilisha
taratibu kwenye wizara za kisekta kupitia taasisi za serikali za SIDO, VETA, COSTECH
pamoja na wadau wengine, ili kutengeneza
mashine za kuongeza virutubishi kwenye
unga hapa nchini na zitakazotumiwa na wasindikaji
wadogo na wakati
Mhagama ameeleza hayo leo tarehe 13 Machi, 2021 wakati akigawa na kuzindua utumiaji wa ya kuongeza virutubishi kwa wasindikaji wadogo na wakati jijini Tanga. Mashine
hizo 5 zenye thamani ya takribani
shilingi milioni tano kwa kila moja, zimetolewa na Mradi wa Utoaji wa vyakula vilivyorutubishwa shuleni unaoratibiwa na
Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la GAIN
Tanzania.
Amefafanua kuwa serikali imelenga
kutengeneza mashine hizo hapa nchini, kwa kuwa mashine hizo ambazo huagizwa nje
ya nchi, gharama yake ni kubwa kwa wasindikaji wadogo, hali inayosababisha urutubishaji wa unga wa mahindi kwa viwanda
vingi kutofanya vizuri kwani ni asilimia saba (7%) pekee ya unga unaozalishwa
nchini ndiyo unaongezewa virutubishi, hivyo
watumiaji wengi wa unga wanakosa
Vitamini na Madini muhimu mwilini.
“Mashine hizi zikitengenezwa, hapa nchini
zitaweza kuwafikia wasindikaji wadogo wengi. Wasindikaji wengi wakitumia
mashine hizi tutakuwa na jamii yenye afya bora
na uwezo wa kupambana na maradhi.
Wastani wa msindikaji mdogo kwa siku anaweza kusindika unga kati ya tani 5 hadi 10 za unga kwa siku. Hivyo mashine hizi 5 kwa hapa Tanga zitasaidia kusindika unga
uliyorutubishwa wa tani 50 kwa siku” Amesisitiza
Mhagama
Aidha, ameeleza kuwa serikali kupitia
Ofisi ya Waziri Mkuu, inaendelea na jitihada za kusimamia masuala ya lishe kwa
ngazi ya Taifa kwa kuwa tayari sera na sheria zimesha tungwa. Pia, ameeleza
kuwa tayari maagizo yametolewa kwa zabuni zote za usambazaji wa chakula katika
shule lazima chakula kiwe na virutubishi. Vilevile, TBS wanaedelea kukagua
ubora wa chakula nchini hususani kwa wazalishaj wakubwa.
“Tunawahamasisha wasindikaji
wadogo wa unga na mahindi waungane na kutengeneza ushirika ili waweze kupata
unafuu wa kuagiza mashine za kuongeza virutubishi. Lakini pia tunaedelea kuzisisitiza
Halmashauri kuangalia namna ya upatikanaji wa mashine hizi, hata kwa njia ya
kuwakopesha, lakini pia tumezitaka Halmashauri
kutengeneza sheria ndogo ndogo zitakazo
wataka wazalishaji wadogo na wa kati wa mahindi kuongeza virutubishi. Naomba pia
mkoa huu uibebe hii agenda ya lishe ”
Amesisitiza Mhagama.
Awali, Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, ambaye
pia ni mbunge wa jimbo la Tanga mjini, Ummy
Mwalimu, ameeleza kuwa Ofisi hiyo
wameamua kuibeba agenda ya kuhakikisha wananchi wanakuwa na lishe bora. Amebainisha kuwa watakuwa na mpango wa kupanda miti ya
matunda hususan; maembe, mapera, maparachichi na malimau, kwa shule zote nchini
ikiwa ni shule za msingi na shule za
sekondari. Pia amesisitiza kuwa mpango
huo utaanzia jimbo la Tanga mjini.
Kwa upande wake, Mkuu wa mkoa wa
Tanga, Martine Shigela amelishukuru shirika lisilo la kiserikali la GAIN
Tanzania kwa kushirikiana na serikali katika kuhakikisha masuala ya lishe
mkoani humo yanakuwa bora kwa kutoa bure mashine za kuongeza virutubishi kwenye
unga kwa wasindikai wadogo pamoja na virutubishi. Aidha, amefafanua kuwa Tanga haitakuwa nyuma tena kwenye masuala ya
lishe kwa kuwa wamejaliwa kulima mboga mboga, maharage, Maziwa yapo pamoja na samaki na mazao yake.
Naye Meneja Mradi wa urutubishaji vyakula, Gain Tanzania, Archad Ngemela,
ameeleza kuwa shirika hilo limetoa mashine 10 za kuongeza virutubishi kwenye
unga ikiwa mashine 5 kwa mkoa wa Kagera na mashine 5 kwa mkoa wa Tanga. Pia
amefafanua kuwa wametoa virutubishi kilo 700 kwa mkoa wa Kagera na Tanga kilo
700.
Akiendelea kutaja mafanikio ya mradi huo, ameeleza kuwa katika kujenga
usimamizi bora wa masuala ya lishe kwenye mikoa hiyo, wamewanunulia maafisa
lishe mashine za kupima madini ya chuma ili waweze kuhakiisha yameongezwa
kwenye chakula kwa mujibu wa sheria. Aidha, amesema kuwa wamewajengea uwezo
zaidi ya wazalishaji 40 wa mikoa hiyo pamoja na zaidi ya shule 30 kwa kila
mkoa zimepata mafunzo juu ya
masuala ya lishe. Pia kamati za mikoa
hiyo za usimsmizi masuala ya lishe nazo zimejengewa uwezo .
Shirika lisilo la kiserikali la
GAIN Tanzania limetekeleza agizo la serikali la upatikanaji wa chakula chenye virutubishi shuleni, kwa kuanza na
mkoa wa Kagera na Tanga. Lengo la mradi huo ni kuwapatia chakula kilichorutubishwa wanafunzi elf 12 kwenye shule 30 za mkoa wa Kagera na Tanga. Mradi huo
umetekelezwa kuanzia Desemba 2019 na Machi 2021 utekelezaji wa awamu ya kwanza
unakamilika. Wadau wanaoutekeleza mradi huo chini ya uratibu wa Ofisi ya Waziri
Mkuu ni; TAMISEMI, TFNC, TBS pamoja na RITA.
ENDS.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista
Mhagama, akipata maelezo kutoka kwa Meneja Mradi wa urutubishaji vyakula, Gain
Tanzania, Archad Ngemela, namna ya mashine za kuongeza
virutubishi kwenye unga inavyoweza kumsaidia msindikaji mdogo wa unga mara bada ya kuzinduliwa utumiaji wa mashune hiyo
jijini Tanga.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista
Mhagama, Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu, Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martine Shigela Wakipata
maelezo kutoka kwa Meneja Mradi wa urutubishaji vyakula, Gain
Tanzania, Archad Ngemela, namna ya mashine za kuongeza
virutubishi kwenye unga inavyoweza kumsaidia msindikaji mdogo wa unga mara bada ya kuzinduliwa utumiaji wa mashune hiyo
jijini Tanga.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista
Mhagama, Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martine Shigela, Meneja Mradi wa urutubishaji vyakula, Gain Tanzania, Archad Ngemela, wakizindua
mashine ya kuongeza virutubishi kwenye
unga kwa msindikaji mdogo wa unga mara jijini
Tanga.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista
Mhagama akifurahia mara baada ya kuzindua utumiaji wa mashine ya kuongeza virutubishi kwenye unga hapa
nchini ninayotumiwa na wasindikaji wadogo mara baada ya kuizindua utumiaji wa mashine hiyo jijini Tanga kwenye kiwanda cha
Shenkonde.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista
Mhagama, Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu, Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martine Shigela wakiangalia
unga uliongezwa virutubishi na mashine maalum ya kuongeza virutubishi kwenye unga inayotumiwa
na msindikaji mdogo wa unga mara bada ya kuzinduliwa utumiaji wa mashine hiyo
jijini Tanga.
Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martine
Shigela
akiwaeleza wananchi wa mkoa huo umuhimu wa kutumia unga uliongezwa virutubishi
na mashine maalum ya kuongeza virutubishi kwenye unga inayotumiwa
na msindikaji mdogo wa unga mara bada ya kuzinduliwa utumiaji wa mashine hiyo
jijini Tanga
Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais, Ummy Mwalimu, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga mjini, akiwaeleza
wananchi wa jimbo hilo umuhimu wa kutumia unga uliongezwa virutubishi na mashine maalum
ya kuongeza virutubishi kwenye unga
inayotumiwa na msindikaji mdogo wa unga
mara bada ya kuzinduliwa utumiaji wa
mashine hiyo jijini Tanga.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista
Mhagama akisisitiza umuhimu wa kutengeneza
mashine za kuongeza virutubishi kwenye
unga hapa nchini na kutumiwa na
wasindikaji wadogo kwa wadau wa lishe na
Kamati ya Usimamizi wa Lishe jijini Tanga.
Baadhi
ya Wadau wa lishe na Kamati ya Usimamizi wa Lishe jijini Tanga wakifuatilia
shughuli ya uzinduzi wa mashine za kuongeza virutubishi kwenye unga hapa
nchini na kutumiwa na
wasindikaji wadogo kwa Lishe jijini
Tanga.
]Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista
Mhagama akiwa katika pucha ya pamoja na kikundi cha Tanzania Girls Guide cha
mkoani Tanga amabcho kinajihusisha na masuala ya kuhamasisha masuala ya
lishe mara baada ya kuzindua utumiaji wa mashine za kuongeza
virutubishi kwenye unga na kutumiwa na
wasindikaji jijini Tanga
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.