Saturday, April 24, 2021
Friday, April 23, 2021
Friday, April 9, 2021
Waziri Mhagama atoa maagizo 22 kwa Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama, ametoa maagizo kwa menejimenti ya ofisi hiyo ili kuboresha utendaji katika ofisi hiyo kutokana na mabadiliko ya kiuongozi yaliyofanywa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Kwa sasa majukumu ya ofisi hiyo ya Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu yatakuwa yanasimamiwa na Katibu Mkuu mmoja na Manaibu Makatibu Wakuu wawili, awali majukumu hayo yalikuwa yanasimamiwa na Makatibu Wakuu wa tatu kwa kila mmoja akisimamia majukumu yake.
Kabla ya kutoa maelekezo hayo kwenye kikao kazi na menejimenti ya ofisi hiyo kilichojumuisha wakuu wa idara, vitengo na taasisi zilizo chini ya ofisi hiyo leo tarehe 9 Aprili, 2021 Jijini Dodoma, Waziri Mhagama amebainisha kutoridhishwa na baadhi ya watendaji kutoshiriki kikamilifu kwenye kikao cha Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa ajili ya kutoa ufafanuzi wa masuala kama ilivyotakiwa na mkaguzi huyo.
“Kila tunachofanya ni kwa ajili ya taswira ya Mhe. Waziri Mkuu na ofisi ya Waziri Mkuu, nasikitika miongoni mwetu tukishindwa kutekeleza wajibu wetu tutatia doa ofisi ya Waziri Mkuu. Katibu mkuu fikiria utaratibu wa kudhibiti uzembe lazima kila mmoja awajibike. Tumepanga katika mambo ya msingi hatutasita kufuatilia utendaji ili kila mmoja atekeleze wajibu wake.”Amesema Mhe. Mhagama.
Akitoa maagizo katika kikao hicho amewataka watumishi kutanguliza taifa kwa kila jambo pia na kuwa wazalendo katika kutekeleza majukumu yao. Aidha amewataka kutumia ubobezi wa taaluma walizo nazo ili kuleta matokeo yenye tija kwenye ofisi hiyo. Amewasistiza kuwa wabunifu katika utendaji wa shughuli zao kwa kuizingatia kasi ya serikali ya awamu ya sita.
Aidha, Mhe. Mhagama ameagiza kufanyika kwa vikao vya kila robo muhula ili kujipima na kutathimini namna ya utendaji wa shughuli za idara na taasisi za ofisi hiyo, amesisitiza vikao hivyo vitaweza kuchangia kuleta mabadiliko ya haraka ya kiutendaji katika idara zote na kupata matokeo yaliyo kusudiwa.
Pia, Mhe.Mhagama amezitaka Idara na Taasisi zilizo chini ya ofisi hiyo kuendeleza dhana ya mshikamano katika utekelezaji wa shughuli za ofisi hiyo. Amefafanua kuwa mafanikio ya moja ya idara ya ofisi hiyo ni mafanikio ya ofisi nzima hivyo amewataka watumishi wote kushirikiana.
Mhe.Mhagama ameagiza kuhakikisha Mabaraza ya wafanyakazi katika ofisi hiyo yaendelee kufanyika.Aidha, amesisitiza kuhakikisha katika idara,wizara na tasisi za serikali pamoja na kwenye sekta binafsi mabaraza hayo yanafanyika ili waweze kuimarisha mauhusiano kati ya waajiri na wafanyakazi.
Aidha Waziri ameagiza kabla ya mwisho wa mwezi huu wa Aprili, mfumo wa kielektroniki wa vibali vya kazi na ukaazi kwa wageni uwe umezinduliwa na kufanya kazi ili kudhibiti mianya ya rushwa. Mfumo huo utasaidia kupunguza urasimu wa utoaji vibali kwa wawekezaji.
“Tayari tumesha wafukuza baadhi ya maafisa kazi wanye tabia ya kupokea rushwa kwenye vibali, tunataka mfumo huo kusaidia kuondoa tatizo la rushwa kwenye vibali, tunazo taarifa sisi tukisha pitisha utoaji vibali hivyo vinachukua zaidi ya wiki mbili havijatolewa ili kumfikia muhusika. Nataka mfumo huo uanze kufanya kazi.” Amesisitiza Mhe. Mhagama.
Pia, Mhe. Mhagama meagiza andaliwe kikao na maafisa rasilimali watu kutoka kwenye makampuni makubwa ya uwekezaji nchini, ili waelezwe utaratibu sahihi wa utoaji vibali. Amefafanua kwamba baadhi ya mawakala wanao wasaidia makampuni hayo katika kupata vibali hivyo wamekuwa wakikiuka taratibu na tayari wamewachukulia hatua. Aidha ameagiza kuhakikisha kuwa mikataba ya ajira inatolewa na wajiri nchini pamoja na kuzingatia masuala ya mishahara.
Mhe.Waziri ameagiza kila Ijumaa ya mwisho wa mwezi, ufanyike utekelezaji wa Mpango kazi wa kushughulikia kero na malalmiko za wafanyakazi, waajiri na ya wadau wengine katika sekta ya kazi na ajira.Aidha, ameagiza kufanyika ukaguzi kwenye makampuni na migodi, miradi ya kimkakati na makampuni, amesema kuwa ukaguzi huo utasaidia uwekezaji kuwa wa tija kwa watanzania kwa kuwa na uwiano wa ajira pamoja na mishahara.
“Natambua tupo kipindi cha mpito cha kubadili mifuko ya hifadhi ya jamii nataka ndani ya wiki moja Katibu Mkuu hakikisha vikao vya kimkakati tulivyo viweka kwa kushirikiana vyama vya waajiri, vyama vya wafanyakazi na sisi serikali vinaanza kufanyika ili zoezi hilo liweze kukamilika kama lilivyo agizwa. ” Amesisitiza Mhe.Mhagama.
Masuala mengine ambayo ameagiza Mhe.Mhagama ni kufuatilia mradi wa kukuza ujuzi, mafunzo ya uwanagenzi, mafunzo kwa vitendo mahali pa kazi kwa wahitimu, suala la migogoro kwa wafanyakazi kupitia tume ya usuluishi na uwamuzi, masuala ya mawakala kukagua mahali pa kazi. Pia ameitaka Kitengo cha Huduma za Ajira kushirikiana na Uhamiaji na Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kwa kuibua ajira zenye staha nje ya nchi na kuangalia masuala ya mikataba ya ajira hizo.
Aidha, ameelekeza utekelezaji wa maagizo yake kwenye miradi ya Mbigili na Mkulazi iliyopo chini ya NSSF. Ameagiza aandaliwe kikao kazi na timu ya NSSF kwajili ya miradi hiyo pia ameelekeza kukutana na maafisa matekelezo wa mikoa wa NSSF. Amesisitiza na kuagiza ni muhimu shughuli zote zinazotekelzwa kwenye ofisi hiyo zizingatie kuhusisha masuala ya wenye ulemavu pia na ameataka wahakikishi hata sekta nyingine kufanya hivyo.
Kwa upande wake katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajiara na Wenye Ulemavu) Tixon Nzunda, amemhakikishia Waziri Mhagama kutekeleza Maagizo yote kwa kuzingatia misingi ya weledi, Uadilifu, bidii ya kazi ili kuhakikisha maagizo hayo yanatekelezwa kwa wakati.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Patrobas Katambi, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu) Mhe. Ummy Ngeriananga, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Bw. Tixon Nzunda pamoja na Manaibu Makatibu Wakuu ; Profesa Jamal Adam Katundu na Kaspar Kaspar Mmuya.
MWISHO.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Bw. Tixon Nzunda akizungumza wakati wa kikao hicho, kuushoto kwake ni Profesa Jamal Adam Katundu na Kaspar Kaspar Mmuya.
Thursday, April 8, 2021
Katibu Mkuu Nzunda ahimiza Kasi na Matokeo Ofisi ya Waziri Mkuu
Katibu
Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu) amewataka Manaibu Makatibu Wakuu wapya, Menejimenti na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kuongeza
kasi, bidii na ari katika utendaji kazi wa majukumu ili kutoa matokeo yenye
tija kwa wananchi.
Katibu
Mkuu Nzunda ameyasema hayo leo tarehe 8 Aprili, 2021, Jijini Dodoma, wakati wa
kuwapokea Manaibu Makatibu Wakuu wapya wa Ofisi ya Waziri Mkuu walioapishwa
Ikulu Jijini Dar Es Salaam, Aprili 6, 2021 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Ameeleza kuwa, Ofisi hiyo ina majukumu makubwa
ikiwemo kuratibu shughuli za Serikali, hivyo ni muhimu kuongeza nguvu zaidi katika
utekelezaji wa majukumu ili kusimamia kwa ufanisi uratibu wa shughuli za
serikali.
“Jukumu letu ni kumsaidia Mhe. Waziri Mkuu kutekeleza majukumu ya
kusimamia shughuli za serikali, hatunabudi kufanya kazi kwa utaalamu, weledi na
kwa kuwajibika kwa kujituma ili kuhakikisha tunapata matokea anayo yataka,” alisema
Nzunda
Kwa upande wa Manaibu Makatibu
Wakuu wapya; Profesa Jamal Adam Katundu na Bw. Kaspar Kaspar Mmuya. wamemhakikisha Katibu Mkuu, kushirikiana na Watendaji wa Ofisi hiyo
kwa kufanya kazi kwa kasi na weledi ili kuhakikisha changamoto za wananchi zinapata ufumbuzi kwa wakati.
Tarehe 6 Aprili, 2021 Ikulu Jijini Dar Es Salaam,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliwaaapisha
Manaibu Makatibu Wakuu wa Ofisi hiyo.
Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Kaspar Mmuya akipokea ua kutoka kwa
Afisa Tawala wa ofisi hiyo Bi. Leah Kibasa wakati wa mapokezi alipowasili rasmi
mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Suluhu jijini Dar es Salaam na kupokelewa na watumishi wa ofisi hiyo Aprili 8,
2021 katika ofisi ya Waziri Mkuu iliyopo Mtaa wa Relini Dodoma.
Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Profesa Jamal Katundu akipokea ua kutoka kwa
Afisa Utumishi wa ofisi hiyo Bi. Faith Lazaro wakati wa mapokezi rasmi
alipowasili na kupokelewa na watumishi wa ofisi hiyo Aprili8, 2021 katika ofisi
ya Waziri Mkuu iliyopo Mtaa wa Relini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Kaspar Mmuya akisalimiana na watumishi wa Ofisi hiyo mara baada ya kuwasili rasmi katika ofisi hiyo, aliyeongozana naye ni Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu wa ofisi hiyo Bw. Greyson Mwaigombe.
Mkurugenzi
wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.
Greyson Mwaigombe akimtambulisha Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Profesa Jamal
Katundu kwa watumishi wa Ofisi hiyo eneo la Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu mara baada ya kupokelewa katika ofisi hizo Mtumba Dodoma.
Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Kaspar Mmuya akiweka saini kitabu cha
wageni alipowasili katika ofisi ya Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo (Sera, Bunge,
Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Tixon Nzunda Jijini Dodoma.
Naibu
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Profesa Jamal Katundu akiweka saini katika
kitabu cha wageni alipowasili katika ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira
na Wenye Ulemavu) zilizopo Mtumba Jijini Dodoma.
Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Kaspar Mmuya akizungumza na baadhi ya
Wakuu wa Idara na Vitengo vya ofisi hiyo (Sera, Uratibu na Bunge) mara baada ya
kuwasili katika ofisi hiyo Aprili 8, 2021 Jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Profesa Jamal Katundu akizungumza na Menejimenti ya Ofisi hiyo upande wa Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu mara baada ya kuwasili katika ofisi hiyo Aprili 8, 2021 eneo la Mtumba Jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Kaspar Mmuya akizungumza na Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu mara baada ya kuwasili na kupokelewa na watumishi hao katika ofisi zao zilizopo Mtumba Dodoma.
Mkurugenzi
wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu wa Ofisi ya Waziri Mkuu
Bw. Greyson Mwaigombe akimtambulisha Naibu Katibu Mkuu wa ofisi hiyo Bw. Kaspar
Mmuya kwa baadhi ya watumishi wa Ofisi hiyo (Sera, Uratibu na Uwekezaji).