Katibu
Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu) amewataka Manaibu Makatibu Wakuu wapya, Menejimenti na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kuongeza
kasi, bidii na ari katika utendaji kazi wa majukumu ili kutoa matokeo yenye
tija kwa wananchi.
Katibu
Mkuu Nzunda ameyasema hayo leo tarehe 8 Aprili, 2021, Jijini Dodoma, wakati wa
kuwapokea Manaibu Makatibu Wakuu wapya wa Ofisi ya Waziri Mkuu walioapishwa
Ikulu Jijini Dar Es Salaam, Aprili 6, 2021 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Ameeleza kuwa, Ofisi hiyo ina majukumu makubwa
ikiwemo kuratibu shughuli za Serikali, hivyo ni muhimu kuongeza nguvu zaidi katika
utekelezaji wa majukumu ili kusimamia kwa ufanisi uratibu wa shughuli za
serikali.
“Jukumu letu ni kumsaidia Mhe. Waziri Mkuu kutekeleza majukumu ya
kusimamia shughuli za serikali, hatunabudi kufanya kazi kwa utaalamu, weledi na
kwa kuwajibika kwa kujituma ili kuhakikisha tunapata matokea anayo yataka,” alisema
Nzunda
Kwa upande wa Manaibu Makatibu
Wakuu wapya; Profesa Jamal Adam Katundu na Bw. Kaspar Kaspar Mmuya. wamemhakikisha Katibu Mkuu, kushirikiana na Watendaji wa Ofisi hiyo
kwa kufanya kazi kwa kasi na weledi ili kuhakikisha changamoto za wananchi zinapata ufumbuzi kwa wakati.
Tarehe 6 Aprili, 2021 Ikulu Jijini Dar Es Salaam,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliwaaapisha
Manaibu Makatibu Wakuu wa Ofisi hiyo.
Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Kaspar Mmuya akipokea ua kutoka kwa
Afisa Tawala wa ofisi hiyo Bi. Leah Kibasa wakati wa mapokezi alipowasili rasmi
mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Suluhu jijini Dar es Salaam na kupokelewa na watumishi wa ofisi hiyo Aprili 8,
2021 katika ofisi ya Waziri Mkuu iliyopo Mtaa wa Relini Dodoma.
Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Profesa Jamal Katundu akipokea ua kutoka kwa
Afisa Utumishi wa ofisi hiyo Bi. Faith Lazaro wakati wa mapokezi rasmi
alipowasili na kupokelewa na watumishi wa ofisi hiyo Aprili8, 2021 katika ofisi
ya Waziri Mkuu iliyopo Mtaa wa Relini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Kaspar Mmuya akisalimiana na watumishi wa Ofisi hiyo mara baada ya kuwasili rasmi katika ofisi hiyo, aliyeongozana naye ni Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu wa ofisi hiyo Bw. Greyson Mwaigombe.
Mkurugenzi
wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.
Greyson Mwaigombe akimtambulisha Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Profesa Jamal
Katundu kwa watumishi wa Ofisi hiyo eneo la Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu mara baada ya kupokelewa katika ofisi hizo Mtumba Dodoma.
Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Kaspar Mmuya akiweka saini kitabu cha
wageni alipowasili katika ofisi ya Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo (Sera, Bunge,
Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Tixon Nzunda Jijini Dodoma.
Naibu
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Profesa Jamal Katundu akiweka saini katika
kitabu cha wageni alipowasili katika ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira
na Wenye Ulemavu) zilizopo Mtumba Jijini Dodoma.
Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Kaspar Mmuya akizungumza na baadhi ya
Wakuu wa Idara na Vitengo vya ofisi hiyo (Sera, Uratibu na Bunge) mara baada ya
kuwasili katika ofisi hiyo Aprili 8, 2021 Jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Profesa Jamal Katundu akizungumza na Menejimenti ya Ofisi hiyo upande wa Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu mara baada ya kuwasili katika ofisi hiyo Aprili 8, 2021 eneo la Mtumba Jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Kaspar Mmuya akizungumza na Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu mara baada ya kuwasili na kupokelewa na watumishi hao katika ofisi zao zilizopo Mtumba Dodoma.
Mkurugenzi
wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu wa Ofisi ya Waziri Mkuu
Bw. Greyson Mwaigombe akimtambulisha Naibu Katibu Mkuu wa ofisi hiyo Bw. Kaspar
Mmuya kwa baadhi ya watumishi wa Ofisi hiyo (Sera, Uratibu na Uwekezaji).
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.