Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu),
Mhe. Jenista Mhagama, kwa niaba ya serikali, kupitia Wakala wa Usalama na Afya
Mahali pa Kazi (OSHA), ameikabidhi Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na
Sheria Tuzo yenye lengo la kutambua mchango wa kamati hiyo katika kuboresha
utendaji wa Wakala hiyo.
Waziri Mhagama
ameikabidhi kamati hiyo tuzo leo tarehe 29 Machi, 2021 jijini Dodoma wakati
kamati hiyo ilipokuwa ikipokea taarifa ya utekelezaji wa Wakala hiyo.
Amebainisha kuwa ushauri wa kamati hiyo umeiwezesha wakala kuboresha Utendaji
kwa kutengeneza mifumo ya kimtandao ya kurahisisha utendaji wa Wakala hiyo, Kupunguza
tozo saba zilizokuwa kero kwa wadau wa OSHA pamoja kuongeza mapato ya Wakala
hiyo.
“Mara nyingi tumezoea
serikali kupewa tuzo kwa kufanya vizuri lakini tumekuwa tukisahau kuwa kuna
baadhi ya walioisaidia serikali kufanya vizuri. Tumepima utekelezaji na
utendaji wa OSHA katika kuzingatia ushauri wenu, tumeona kwa sasa hata gawio
limeendelea kuongezeka linalotolewa na OSHA kwenye serikali, mifumo ya
kimtandao imetengenezwa ya kurahisisha utendaji lakini pia tozo saba zimefutwa,
hivyo hatunabudi kuwashukuru kwa mchango huo umeiboresha OSHA” Amesema Mhe.
Mhagama.
Tozo saba ambazo OSHA
tayari imezifuta kufuatia ushauri uliotolewa na Kamati hiyo ni; Tozo ya Usajili
wa maeneo ya kazi, Tozo ya Fomu ya Usajili, Tozo ya ada ya leseni ya kukidhi
matakwa ya sharia ya Usalama na Afya Mahali Pa kazi, Tozo ya Ushauri wa mambo
Usala na Afya, Faini zinazohusiana na vifaa vya kuzimia moto, Tozo ya elimu kwa
umma, Tozo ya Uchunguzi wa ajali ambayo imepunguzwa kutoka shilingi 500,000/=
hadi shilingi 120,000/=.
Akiongea baada ya
kupokea Tuzo hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Katiba na Sheria, Mhe. Mohamed Mchengerwa amefafanua kuwa kamati hiyo imekuwa
ikitoa ushauri kwa OSHA wa namna ya kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa
majukumu pamoja na kuongeza kipato. Aidha, amebainisha kuwa Ofisi ya Waziri
Mkuu inayoirtaibu Wakala hiyo, imekuwa sikivu kwa kufuata ushauri wao wa kufuta
tozo ambapo kwa kiasi kikubwa imekuwa ni faraja kwa watanzania na wawekezaji
nchini.
Kikao hicho kimehudhuriwa
na Naibu
Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Patrobas Katambi, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye
Ulemavu) Mhe. Ummy Ngeriananga, Katibu Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu), Andrew Massawe, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na
Afya Mahali Pa Kazi (OSHA), Bi. Khadija Mwenda, pamoja na baadhi ya Wakurugenzi
wa OSHA.
OSHA
ni Wakala wa serikali chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na
wenye Ulemavu). Taasisi hii ina wajibu wa kuwalinda wafanyakazi dhidi ya
vihatarishi vilivyopo katika sehemu za kazi ambavyo vinaweza kusabisha magonjwa
na ajali. Wajibu huu unatekelzwa kupitia usimamizi wa Sheria Na. 5 ya Afya na
Usalama Mahali pa Kazi ya mwaka 2003.
Mwaka 2001, ilianzishwa OSHA chini ya Sheria Na. 30 ya Wakala wa Serikali ya mwaka 1997 kama sehemu ya Mpango wa Maboresho katika utoaji wa Huduma za Serikali kwa wananchi. Makusudi ya kuanzishwa kwa OSHA ni kupata chombo cha serikali kwa ajili ya kusimamia Usalama na Afya mahali pa kazi. OSHA ina jukumu la kuhakikisha kuwa wafanyakazi wanafanya kazi katika mazingira ambayo ni salama na yenye kulinda afya zao kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa katika kuzuia ajali na magonjwa yatokanayo na kazi.
mwisho.
Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu),
Mhe. Jenista Mhagama, akimkabidhi tuzo Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Katiba na Sheria, Mhe. Mohamed Mchengerwa, ikiwa ni kutambua mchango wa
Kamati hiyo katika kuboresha utendaji kazi wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali
pa Kazi (OSHA), leo tarehe 29 Machi, jijini Dodoma.Wanaoshuhudia ni Makamu
mwenyekiti wa Kamati hiyo, Najma Giga (Kulia), Katibu Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Andrew Massawe (wa pili
kulia) na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (OSHA), Bi. Khadija Mwenda (kulia).
Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu),
Mhe. Jenista Mhagama, akifafanua namna ushauri wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Katiba na Sheria jinsi ulivyoboresha utendaji wa Wakala wa Usalama na Afya
Mahali pa Kazi (OSHA), wakati kamati hiyo ilipokutana na watendaji wa OSHA, leo tarehe 29 Machi, jijini Dodoma.
Manaibu Mawaziri Ofisi ya Waziri Mkuu; Naibu Waziri, (Kazi,
Vijana na Ajira) Mhe. Patrobas Katambi, (katikati), Naibu Waziri (Wenye Ulemavu) Mhe. Ummy Ngeriananga (kulia) na Katibu
Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Andrew Massawe wakifuatilia
kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria na Wakala wa Usalama na Afya
Mahali pa Kazi (OSHA), leo tarehe 29 Machi, jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Mhe. Mohamed Mchengerwa, (katikati)
akifafanua jinsi ushauri wa kamati hiyo ulivyowezesha Wakala wa Usalama na Afya
Mahali pa Kazi (OSHA) kuboresha utendaji wake, kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Katiba na Sheria, Mhe. Najma Giga na kulia ni Katibu wa kamati hiyo, Ndg.
Stanslaus Kagisa, leo tarehe 29 Machi, jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Mafunzo, Utafiti na Takwimu wa OSHA, Joshua Matiko, akiwasilisha mada kuhusu misingi ya Afya na Usalama mahali Pa Kazi, wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria ipokutana na na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), leo tarehe 29 Machi, jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu),
Mhe. Jenista Mhagama, akifuatilia uwasilishwaji wa mada ya kuhusu misingi ya Afya na Usalama
mahali Pa Kazi wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria ilipokutana na Wakala
wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), leo
tarehe 29 Machi, jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu),
Mhe. Jenista Mhagama, pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Katiba na Sheria, Mhe. Mohamed Mchengerwa, wakiwa na Tuzo iliyotolewa na Kamati
hiyo kwa kuchangia ufanisi wa utendaji wa Wakala wa Usalama na Afya Mahala Pa Kazi
(OSHA), wengine ni wajumbe wa kamati hiyo, watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu na
OSHA, leo tarehe 29 Machi, jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.