Friday, August 26, 2022

WAZIRI SIMBACHAWENE: MZEE KUSILA AMEFANYA MAMBO MENGI YA KUIGWA


Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene amesema Mzee William Kusila alipenda kuona viongozi wanazingatia miiko, na kuishi kwa kuwa mfano mwema kwa jamii.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene alipokuwa akitoa salamu za serikali katika ibada ya mazishi ya Mzee Williamu Jonathan Kusila aliyezaliwa Mwaka 28/02/1944 na kufariki 21/08/2022,  iliyofanyika nyumba kwake kata ya Mtitaa-Bahi Dodoma 26/August/2022.

“Mzee kusila ni kipimo cha mtu muadilifu; mtu mwenye Upendo, na mtu aliyefanya mambo mengi mazuri ambayo tunapaswa kuyaiga na kuyaenzi.”

Tumepoteza kiongozi wa kisiasa aliyeshika nafasi mbalimbali za umma na kutimiza majukumu yake ipasavyo, ni mtu aliyepinga na kukataa rushwa, alisema Waziri.

Aidha ametoa rai kwa Watoto wa Mzee Kusila kuzidi kushirikiana na kushikamana ili kutunza jina na heshima ya baba.

“Amefafanua watu hawazaliwi sawa, mtatofautiana kwa uwezo wa elimu, uwezo wa kipato na mambo mengine lakini wote ni Watoto wa mzee Kusila ni lazima mtengeneze mamlaka itakayosaidia kuwaongoza kama familia”

Naye  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amesema  Mzee William Kusila alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Saba wa Dodoma kati ya Mwaka (1993-19995) alikuwa Mbunge wa jimbo la Bahi na katika vipindi tofauti amekuwa waziri wa kilimo, Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi na amewahi kuwa Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma.

 “Alifanya kazi kwa upendo Mkubwa; aliokuwa nao kwa wananchi wa Dodoma, Baba yetu aliongoza kwa Vitendo na sio kwa kuagiza, kama alisema limeni nayeye alikuwa analima”

Naye Mbunge Mstaafu wa jimbo la Chilowa Mhe. Hezekiah Chibulunje akitoa salamu za rambirambi amesema anamkumbuka mzee Kusila kwa jitihada zake za kuondoa Njaa Dodoma na kuhakikisha tunapanda mazao yanayostahimili ukame.

“Alikuwa na uchungu sana katika kuondoa njaa na vile vile katika swala la zima la kusimamia elimu, nimefanya naye kazi kwa ushirikiano mkubwa sana bila nongwa”

 

Read More

Wednesday, August 24, 2022

JITOKEZENI KWENYE ZOEZI LA SENSA ILI MUHESABIWE


 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu  Mhe. George  Simbachawene amehimiza wananchi kujitokeza kuhesabiwa katika zoezi la sensa ya watu na makazi kwa ajili ya maendeleo yetu wenyewe.

“Unapohesabiwa unakuwa upo katika mpango wako wa maendeleo, katika sehemu yako unayoishi na Nchi kwa ujumla”

Hayo yamesemwa na waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene baada ya kushiriki zoezi la sensa ya watu na makazi jimboni kwake Kibakwe katika Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa.

Amefafanua kwamba usipohesabiwa, unakosa lile fungu lako katika miaka 10 ijayo kwa ajili ya mipango ya maendeleo.

“Bado tuna siku tano mbele kwa ajili ya kuhesabiwa hakikisha umeacha kumbukumbu za watu walilolala usiku wa kuamkia tarehe 23 Agusti 2022, alisema  Waziri”

Read More

Saturday, August 20, 2022

WATENDAJI WAHIMIZWA KUONGEZA KASI UTEKELEZAJI WA MRADI WA AFDP


 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene amehimiza kuwa na vikao vya uratibu vya pamoja kati ya wizara na taasisi zinazotekeleza mradi wa mradi wa AFDP ili kuongeza kasi ya utekelezaji wa mradi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe.  George Simbachawene alipotembelea shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) Kigamboni Jijini Dar es salaam ambalo linatekeleza programu ya kuendeleza kilimo na uvuvi katika mradi wa AFDP unaoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu sera Bunge na Uratibu na kutekelezwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Kilimo na Wizara ya Uchumi wa Bluu na Uvuvi – Zanzibar.

Waziri Smbachawene amesema programu AFDP ni ya miaka sita kuanzia 2021/2022 hadi 2027/2028 ambayo itagharimu jumla ya Dola za Kimarekani 77.4 millioni (Mkopo toka IFAD USD 58.8 millioni; Serikali USD 7.7 millioni; Sekta Binafsi 8.4 millioni na Wananchi USD 2.4 millioni).

 “Mradi huu wa  uchumi wa bluu ukisimamiwa vizuri utaibua shirikia la TAFICO, na utaibua uchumi wa biashara ya uvuvi zinazofanywa na sekta binafsi.“

Lazima tutengeneze kikosi kazi kitakachokuwa kinaashughulikia changamoto zinazojitokeza kutoka taasisi moja kwenda nyingine pamoja na wizara moja kwenda nyingine katika utekelezaji wa mradi, alisema Waziri.

“Eneo hili linaloshughulikiwa na shirika la TAFICO linaenda kujibu ahadi za ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020-2025.”

Naye Katibu Mkuu Ofisi ya waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Dkt. John Jingu amesema mradi huu ni mradi mkubwa sana na ni mradi wa kimkakati.

“Tuone namna ambavyo tutautekeleza huu mradi kikamilifu, spidi na kasi ya utekelezaji wa mradi bado hairidhishi.”

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya shirika la TAFICO Profesa Yunus Mgaya amesema wanalichukulia shirika la TAFICO kama shirika la kimkakati hasa katika dhana ya kutekeleza uchumi wa blue.

“Shirika linajukumu la kuwasaidia wavuvii wadogo wadogo hasa katika kunyanyua  vipato vyao, kuwawezesha kuhifadhi mazao yao ya uvuvi kuingia ubia na wananchi mbalimbali katika shughuli za uvuvi bahari kuu,”

Read More

Thursday, August 18, 2022

WATENDAJI WA SENSA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA BIDII

Watendaji wa Sensa wapewa wito kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kukamilisha kwa ufanisi  zoezi la Sensa ya watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika 23 August 2022, wito huo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene.

“baada ya zoezi la sensa ya watu na makazi kuna kazi kubwa ya Mchakato lazima tuwe tayari kusimama pamoja na kufanya kazi usiku na mchana ili zoezi liweze kukamilika”

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene katika kikao cha saba cha kamati kuu ya Taifa Sensa ya Watu na Makazi 2022 kilichofanyika ukumbi wa Julius Nyerere Convection Centre, Dar es saalam.

Waziri Simbachawene ameipongeza kamati ya Sensa ya Watu na makazi ya mwaka 2022 kwa kufanya kazi zake vizuri na hivyo kufanikisha maamuzi ya kamati kuu ya Taifa ya Sensa.

“Vilevile napongeza Wizara zote, Wadau wa Maendeleo na Sekta binafsi kwa ushirikiano mkubwa  walioonesha wakati wote wa maandalizi ya sensa ya watu na makazi”

Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt, Alibina Chuwa amesema kwa wakuu wa kaya ambao hawatakuwa nyumbani wameandaa fomu maalumu ambayo itakuwa na maswali 11 ambayo itasambazwa kwa wakuu wote wa kaya kupitia kwa makarani wao wa sensa.

“Wakuu wa kaya waandike taarifa za watu ambao watakuwa wamelala usiku wa kuamkia siku ya sensa ili kumrahisishia karani kujaza taarifa kwenye kishikwambi atakapofika kuchukua taarifa”

Read More

Monday, August 15, 2022

MAANDALIZI YA SENSA YA WATU NA MAKAZI YAPAMBA MOTO


 

Serikali imesema maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi yamefika zaidi ya asilimia 95 hivyo ni vyema kuendelea kushirikiana kwa pamoja kwa kuzingatia muda uliobaki ili kulifikia lengo lililopo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene katika Mkutano Maalum wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alipokutana na sekta binafsi kwa lengo la kutambua mchango wao katika kuelekea siku hiyo ikiwemo ya rasilimali fedha, huduma na vifaa kwa ajili ya zoezi la Sensa ya watu na makazi ya Mwaka 2022.

Alisema kuwa, Serikali inatambua mchango wa sekta binafsi hivyo ni vyema kwa kila mdau kushirikia katika zoezi hili  kwa kadri awezavyo kwa kuchangia  rasilimali fedha, huduma na vifaa vitakavyosaidia kufanikisha zoezi la sensa.

“Karibu kila mdau ameshiriki katika maandalizi ya sensa kupitia taasisi ya sekta binafsi (TPSF) na tumekutana hapa ili kuonesha mshikamano wetu na kutambua michango yenu ninawapongeza sana," alisema Simbachawene.

Naye katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Dkt. John Jingu amesema serikali imeshirikiana sekta binafsi  katika maandalizi ya kuelekea siku ya sensa kwa namna mbalimbali ikiwemo, kugharamia matangazo yanayotoka kwenye vyombo vya habari.

“Kampuni za simu zilisaidia kutoa ujumbe mfupi wa kuhamasisha wananchi na kuelimisha wananchi juu ya zoezi la sensa ya watu na makazi na baadhi kuahidi kuchangia fedha na vifaa mbalimbali ili kufanikisha zoezi la sensa ya watu na makazi” alisisitiza Dkt. Jingu

Naye Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Mhe. Anne Makinda ameshukuru sekta binfasi kwa mchango wao katika kuwezesha maandalizi ya kuelekea siku ya sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika tarehe 23 Agosti, 2022.

“Tumejipanga kusimamia matumizi yote tunayopewa na kuhakikisha tunapata matunda tunayotegemea.” aliesema Mhe. Makinda

Read More

Sunday, August 14, 2022

WAUMINI WAOMBWA KUENDELEA KUIOMBEA NCHI

 


Waumini waombwa kuiombea nchi dhidi ya majanga mbalimbali likiwemo janga la njaa, changamoto za kiuchumi zinazo sababishwa ama na sisi wenyewe au mataifa mengine, magonjwa, dhiki na mmomonyoko wa maadili.

“Uwekezaji katika familia imara ni jambo la msingi, bila kwekeza katika familia hakuna nchi hakuna mataifa hakuna dunia.Msukumo wa watu wanaosimamia dhambi kutumia rasilimali fedha kwenye mambo maovu ni mkubwa  kuliko msukumo wa kutetea mambo mema.”

Wito huo umetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene ufunguzi rasmi wa sikukuu za vibanda (makambi) za kanisa la waadventista wa sabato Magomeni Mwaka 2022, Kwembe Jijini Dar es Salaam yaliyokuwa na Kauli mbiu “NITAKWENDA KWA NGUVU ZA MUNGU.”

Amefafanua kwamba pamoja na kumtegemea Mungu, bado maandiko matakatifu yanatuhimiza kufanya kazi kwa bidii. Katika hili niendelee kuwasihi ndugu Waumini kufanya kazi kwa bidiii huku tukimtumainia Mungu na kuomba baraka zake katika kila kitu. Licha ya kwamba nchi yetu haiegemei upande wowote katika masuala ya dini (Secular State) lakini sehemu kubwa ya watu wake wanaamini katika Mungu kupitia dini na madhehebu mbalimbali.

“Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan inatambua mchango wa Kanisa la Waadventista wa Sabato katika Sekta ya elimu kupitia taasisi zake za elimu; Sekta ya afya kupitia hospitali na vituo vya afya; pamoja na Sekta ya habari kupitia vyombo vya Habari vinavyomilikiwa na kuendeshwa na Kanisa. Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi na rafiki kwa ustawi wa taasisi hizo ili ziendelee kuwa sehemu ya kuliletea maendeleo Taifa letu.”

Naye Mchungaji Fidelis Mngwabi, Askofu wa Jimbo la Mashariki Kati mwa Tanzania (ECT), katika neno lake la shukrani ameishukuru serikali kwa kutambua mchango wa kanisa la  waadventista wa Sabato katika kulinda umoja amani na Upendo.

“kanisa litaendelea kuwa na msimamo wa Mungu katika kusaidia waumini kwenda katika njia iliyo sahihi.”Read More

Thursday, August 11, 2022

WIZARA ZAHIMIZWA UFUTAILIAJI WA TAARIFA ZA MPANGO KAZI

Viongozi wa Wizara wapewa rai kufuatilia na kusimamia kwa karibu maafisa viungo ambao wanahusika kuweka taarifa kwenye mfumo ili Viongozi wawe na umiliki (ownership) wa taarifa zilizo katika mfumo huo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene katika kikao kazi cha Mawaziri kilichofanyika katika Ukumbi wa Kambarage Hazina Jijini Dodoma.

“Kwa upande wa uwasilishaji wa Taarifa ya Ilani ya Chama Tawala, uchambuzi umeonesha kuwa kwa kipindi cha mwaka 2022 ni Wizara 14 zilizowasilisha Mpango Kazi wa Utekelezaji wa Ilani kwa mwaka 2022 na Wizara 13 hazijawasilisha. Taarifa za Mpango kazi hutakiwa kuwasilishwa kwenye Mfumo wa ‘DASHBOARD’ mwezi Januari kila mwaka. Aidha, kwa upande wa Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani kwa kipindi cha nusu mwaka, ambazo hutakiwa kuwasilishwa Julai 2022 ni wizara 4 zilizowasilisha.”

Kwa mwaka 2022 tumepokea maelekezo yako kuwa Taarifa ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuhusu Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 na Taarifa ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kuhusu Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 itawasilishwa mwezi Novemba, 2022. Ili kuratibu taarifa hiyo vyema na kwa wakati, napenda Mawaziri kuratibu taarifa katika maeneo yanayowahusu na kuhakikisha zinawasilishwa kwa wakati kupitia mfumo huo, alisema Waziri.

 

 

Read More

Monday, August 8, 2022

WADAU WA KILIMO WAHIMIZWA KUTUMIA TEKNOLOJIA KUTATUA CHANGAMOTO ZA KILIMO

 


Serikali imetoa rai kwa wadau wa kilimo kuendelea kutambua Ubunifu na Teknolojia mpya zinazooneshwa katika maonesho ya Nanenane ili kuweza kuzikuza na kuzisambaza kwa walengwa wakiwemo Wakulima, Wafugaji na Wavuvi

“Maonesho ya Nanenane yawe ni kitovu cha teknolojia mpya (innovation hub) kwa kuhakikisha kuwa wadau wote wa Sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi wanashiriki Maonesho haya, ili kuonesha na kujifunza teknolojia zote zinazotoa majawabu ya changamoto za Sekta hizo,”

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene alipokuwa akihutubia katika kilele cha maonesho ya siku ya Nanenane kanda ya Mashariki yaliyofanyika Uwanja wa Mwl. Julius Nyerere Mjini Morogoro kwa niaba ya mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Sote tunatambua mchango mkubwa wa Sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi katika kuchangia pato la Taifa, ajira, usalama wa chakula na malighafi za viwandani. Ndiyo maana kauli mbiu ya maonesho ya mwaka huu inasema “Ajenda ya Kilimo  ni Biashara, Shiriki Kuhesabiwa kwa Mipango Bora ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

“Waoneshaji wanatakiwa kuhakikisha kuwa takwimu na taarifa sahihi zenye ulinganifu kuhusu teknolojia na bidhaa wanazoonesha zinakuwepo ili ziweze kuwasaidia walengwa kufanya maamuzi sahihi, alisema Waziri” 

Aidha Maonesho ya Nanenane yatumike kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo katika Sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi ili kuvutia wawekezaji wengi.

Amefafanua kila ngazi kwa maana ya Kanda, Mikoa, Halmashauri na Wadau wengine ifanye tathmini kwa kuangalia mambo mbalimbali ikiwemo hali ya ushiriki na uhalisia wa teknolojia zinazooneshwa kama zinatumika katika maeneo wanayotoka.

Naye naibu waziri wa kilimo Mhe. Anthony Mavunde amesema bajeti ya kilimo imetoka billioni 294 (2021-2022) mpaka kufikia billioni 954 kwa mwaka wa fedha (2022-2023). Wizara ya kilimo tumejipanga kuleta mapinduzi ya kweli katika kufikia ajenda ya 2030 kwa ushirikiano wa wadau wote kuikuza sekta ya kilimo kufikia 10%.

“Bajeti ya umwagiliaji imepanda kutoka billioni 46 ya mwaka wa fedha uliopita hadi kufikia billioni zaidi ya 400 kwa mwaka huu wa fedha (2022-2023).  Mikakati ni kuwa na mfumo mzuri wa Umwagiliaji na utekelezaji wake umeanza kwa kupitia mabonde yote 22 ya umwagiliaji ili kufanya upembuzi yakinifu na usanifu ili tuanze kufanya kilimo cha umwagiliaji katika maeneo hayo, alisema Naibu waziri.”

Amebainisha katika Utafiti bajeti imepanda kutoka billioni 11.7 kwenda billioni 40 ili kuviwezesha vituo vya utafiti kuja na mbegu bora na mbegu ambazo zinastahimili ukame, sambamba na kujengea uwezo vituo vyetu hasa katika maabara za kupima afya ya udongo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma A. Mwasa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kurudisha pembejeo kwa wakulima. Kupitia ruzuku hiyo mkulima hata nunua kwa bei ya kawaida  bali kutakuwa na punguzo ili kumuwezesha mkulima azalishe kwa tija.

“Maonesho haya yana umuhimu mkubwa na yanatoa elimu kubwa kwa wakulima, tumedhamiria kuichukua teknolojia tuliyoipata kuihamishia vijijini alisema mkuu wa mkoa wa Morogoro.”

Read More