Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene amehimiza kuwa na vikao vya
uratibu vya pamoja kati ya wizara na taasisi zinazotekeleza mradi wa mradi wa
AFDP ili kuongeza kasi ya utekelezaji wa mradi.
Hayo yamesemwa na Waziri wa
Nchi Ofisi ya waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene alipotembelea shirika la
Uvuvi Tanzania (TAFICO) Kigamboni Jijini Dar es salaam ambalo linatekeleza
programu ya kuendeleza kilimo na uvuvi katika mradi wa AFDP unaoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu sera Bunge na Uratibu na
kutekelezwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Kilimo na Wizara ya Uchumi
wa Bluu na Uvuvi – Zanzibar.
Waziri Smbachawene amesema programu
AFDP ni ya miaka sita kuanzia 2021/2022 hadi 2027/2028 ambayo itagharimu jumla
ya Dola za Kimarekani 77.4 millioni (Mkopo toka IFAD USD 58.8 millioni;
Serikali USD 7.7 millioni; Sekta Binafsi 8.4 millioni na Wananchi USD 2.4
millioni).
“Mradi huu wa uchumi wa bluu ukisimamiwa vizuri utaibua
shirikia la TAFICO, na utaibua uchumi wa biashara ya uvuvi zinazofanywa na
sekta binafsi.“
Lazima tutengeneze kikosi kazi
kitakachokuwa kinaashughulikia changamoto zinazojitokeza kutoka taasisi moja
kwenda nyingine pamoja na wizara moja kwenda nyingine katika utekelezaji wa
mradi, alisema Waziri.
“Eneo hili linaloshughulikiwa
na shirika la TAFICO linaenda kujibu ahadi za ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020-2025.”
Naye Katibu Mkuu Ofisi ya
waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Dkt. John Jingu amesema mradi huu ni mradi
mkubwa sana na ni mradi wa kimkakati.
“Tuone namna ambavyo
tutautekeleza huu mradi kikamilifu, spidi na kasi ya utekelezaji wa mradi bado
hairidhishi.”
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
bodi ya shirika la TAFICO Profesa Yunus Mgaya amesema wanalichukulia shirika la
TAFICO kama shirika la kimkakati hasa katika dhana ya kutekeleza uchumi wa
blue.
“Shirika linajukumu la
kuwasaidia wavuvii wadogo wadogo hasa katika kunyanyua vipato vyao, kuwawezesha kuhifadhi mazao yao
ya uvuvi kuingia ubia na wananchi mbalimbali katika shughuli za uvuvi bahari
kuu,”
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.