Viongozi wa Wizara wapewa rai kufuatilia
na kusimamia kwa karibu maafisa viungo ambao wanahusika kuweka taarifa kwenye
mfumo ili Viongozi wawe na umiliki (ownership) wa taarifa
zilizo katika mfumo huo.
Hayo yamesemwa na Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene katika kikao kazi cha Mawaziri kilichofanyika katika
Ukumbi wa Kambarage Hazina Jijini Dodoma.
“Kwa upande wa uwasilishaji wa Taarifa
ya Ilani ya Chama Tawala, uchambuzi umeonesha kuwa kwa kipindi cha
mwaka 2022 ni Wizara 14 zilizowasilisha Mpango Kazi wa Utekelezaji
wa Ilani kwa mwaka 2022 na Wizara 13 hazijawasilisha. Taarifa za Mpango kazi
hutakiwa kuwasilishwa kwenye Mfumo wa ‘DASHBOARD’ mwezi
Januari kila mwaka. Aidha, kwa upande wa Taarifa ya Utekelezaji wa
Ilani kwa kipindi cha nusu mwaka, ambazo hutakiwa kuwasilishwa Julai
2022 ni wizara 4 zilizowasilisha.”
Kwa mwaka 2022 tumepokea
maelekezo yako kuwa Taarifa ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
kuhusu Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 na Taarifa ya
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kuhusu Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa
Mwaka 2020 itawasilishwa mwezi Novemba, 2022. Ili kuratibu taarifa hiyo vyema
na kwa wakati, napenda Mawaziri kuratibu taarifa katika maeneo yanayowahusu na
kuhakikisha zinawasilishwa kwa wakati kupitia mfumo huo, alisema Waziri.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.