Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene amesema serikali itatoa maelekezo
kwa Halmashauri kuweka mipango maalumu ya kuziwezesha ofisi za vikundi vya watu
wanaoishi na virusi vya UKIMWI (Konga) katika maeneo ya usimamizi, ruzuku na
mikopo. Ili kuwa imara na endelevu na kuwa na mchango mkubwa katika kufikia
malengo ya kitaifa na dunia kuhusu UKIMWI.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene wakati
wa uzinduzi wa magari nane ya mradi wa HEBU TUYAJENGE uliofanyika katika Ofisi
za NACOPHA Mbezi Beach Dar es salaam.
“Serikali inatambua umuhimu wa
mifumo ya kijamii kwa sababu ina mchango mkubwa katika maendeleo ya Taifa.
Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Tume ya Kudhibiti UKIMWI itaendelea kuhakikisha Uratibu
wa Sera na miongozo unatoa fursa ya kuziwezesha Konga za WAVIU”
Aidha, katika hotuba yake,
Mheshimiwa Rais alitoa maelekezo mahususi kwa Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia
TACAID, Wizara ya Afya na wadau wengine kuweka jitihada na mikakati madhubuti
katika kuzuia maambukizi mapya ili tuweze kufikia hatua ya kutokomeza kabisa.
Ikiwa ni pamoja na Kuimarisha huduma za
upimaji wa VVU na matumizi ya ARV ili kutokomeza vifo vitokanavyo na UKIMWI, kuweka
mikakati ya kutokomeza ubaguzi na unyanyapaa kwa WAVIU.
“Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya
Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania itayatekeleza maelekezo ya Mheshimiwa Rais kwa haraka ikiwa ni
pamoja na kuziratibu Wizara husika na Wadau katika kuhakikisha maelekezo haya
yanatekelezwa kwa wakati, alisema Waziri.”
Naye Naibu Katibu Mkuu Ofisi
ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Bwn. Kaspar Mmuya amewapongeza NACOPHA kwa
kazi nzuri ya kupambana na maambukizi ya virusi vya UKIMWI.
“Kuhamasisha watu kujitokeza
na kupima afya zao ni njia mojawapo ya kukabiliana na maambukizi mapya ya
virusi vya UKIMWI.”
Akitoa taarifa Mwenyekiti wa
Baraza la Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (NACOPHA) Bi, Leticia Mourice
Kapela, amesema baraza limeneemeka kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu kwa upande wa
vijana, wanawake na WAVIU kwa ujumla.
“Uwezeshi huu katika fursa za
mafunzo, mitaji ya kifedha, vifaa vya kuanzia shughuli za ujasiriamali, umesaidia
vijana WAVIU kupata ujasiri wa kukabiliana na kuziepuka changamoto mbalimbali zinazowaweka
katika hatari ya kupata maambukizi, ikiwemo kuanza ngono katika umri mdogo,
kuwa na mahusiano na watu wenye umri mkubwa
na ulevi wa kupindukia”
Naye Mkurugenzi TACAIDS Bi. Audrey Njelekela, amesema
Konga ziko kwenye Halmashauri 184 na Afua zote zinatekelezwa kwa kushirikiana
na Halmashauri.
“Kupata
magari kutasaidia kuongeza kasi na ufanisi katika kuhakikisha muitikio wa
kitaifa unatekelezwa”
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.