Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu anayeshughulika na Sera Bunge na Uratibu Mhe. George
Simbachawene amesema maswala ya upungufu wa chakula yanachukuliwa kama maafa
kwa mujibu ya sheria ya maafa iliyopo.
Waziri ametoa kauli
hiyo wakati akifafanua hoja iliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Nanyumbu Mhe.
Yahaya Ally Mhata Bungeni katika Mkutano wa Kumi Kikao cha Nne
cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu taratibu za kufuata ili
kupata chakula cha bei nafuu.
Alisema kuwa, Ofisi
yake inajukumu ya kuratibu upatikanaji wa chakula cha msaada kwa kushirikiana
na sekta tofauti tofauti ikiwemo hatua zote muhimu za uzalishaji, upatikanaji
hadi matumizi kwa walaji.
Alifafanua Ofisi ya
Waziri Mkuu inajukumu la kutoa kibali kwa ajili ya chakula cha bei nafuu au
msaada linaratibiwa kwa kuielekeza Wizara ya Kilimo kuchukua hatua kupitia
NFRA.
“Kimsingi jukumu
la kutoa chakula cha bei nafuu au msaada ni jukumu la Ofisi ya Waziri Mkuu
ambalo inalitekeleza kwa kuelekeza Wizara ya Kilimo ili ielekeze NFRA kupeleka
eneo la kukipeleka kile chakula na kwenda kukiuza kwa bei nafuu iliyopangwa,”
alisisitiza waziri.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.