Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala
ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi ameupongeza na kuushukuru Mfuko wa
Dunia (Global Fund) kwa mchango mkubwa unaoutoa katika kuendeleza mapambano
dhidi ya magonjwa ya UKIMWI, Malaria na Kifua Kikuu nchini.
Ametoa pongezi hizo wakati akifungua mkutano wa Uundwaji wa
Miradi ya Mfuko wa Dunia (Global Fund) kwa kipindi cha mwaka 2024- 2026
uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa hoteli ya APC Bunju Dar es Salaam.
Mkutano huo ulioudhuriwa na wajumbe kutoka Ofisi ya Rais
TAMISEMI, Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Fedha, Wizara ya Afya, Wizara ya
Maendeleo ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum,
Sekretarieti ya TNCM, Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini, Tume ya
Kudhibiti UKIMWI Pamoja na Asasi za Kiraia.
Akieleza kuhusu mchango wa Mfuko wa Dunia katika sekta ya
afya nchini, Dkt. Yonazi alisema kuwa, nchi imeendelea kupiga hatua kwa
kuzingatia ufadhali wanaoutoka kwa lengo la kugharamia miradi ya Malaria, Kifua
Kikuu, UKIMWI na Uimarishaji wa Mifumo ya Utoaji wa Huduma za afya.
“Nchi yetu imepiga hatua kubwa katika kupambana na magonjwa
ya UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria kupitia ushirikiano thabiti na misaada
mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi ikiwemo Mfuko wa Dunia yaani Global
Fund,”.Alisisitiza
Aidha alisema kuwa Tanzania bado ni miongoni mwa nchi
zinazokumbwa na changamoto za magonjwa hayo na yameendelea kusababisha vifo kwa
wananchi walio wengi hali inayopelekea kupoteza nguvu kazi ya Taifa.
Alitumia jukwaa hilo kuwaomba wadau mbalimbali kuendelea
kuunga mkono jitihada za Serikali katika uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya.
“Ushirikishwaji wa Wadau Watekelezaji wa Nje ya Serikali
(PR2) katika mapambano haya ni kipaumbele cha Serikali yetu. Niwaombe wadau
wetu kwa pamoja tushirikiane kufikisha huduma hizi katika jamii yote
inayotuzunguka.Ninawasihi muendelee kushirikiana na Serikali katika kuleta
uzoefu hususan pale tunapohitajika kuongeza ufanisi na tija katika miradi na
huduma za afya,”.Alisema Dkt. Yonazi
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Tanzania Natioanal
Coordinationg Mechanism (TNCM) Dkt. Rachel Makunde alimshukuru Katibu Mkuu
ambaye pia ni mwenyekiti wa TNCM kwa usimamizi wake na mchango anaoutoka katika
kuyafika malengo ya chombo hicho.
Naye Dkt. David Sando, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la
MDH aliahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika utekelezaji wa Program
hizo ili kuimarisha huduma za afya nchini.
“Tumeendelea kusupport zaidi ya wagonjwa laki tatu
wanaotumia dawa za kufubaza Makali ya Virusi vya UKIMWI (ARVs) na kupitia
miradi ya HIV, tumeweza kuwafikia wagonjwa wengi katika mikoa 12 tunayoihudumia
ambapo ni zaidi ya nusu ya wagonjwa wote nchini,” alieleza Dkt. Sando
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.