Programu
ya kuendeleza kilimo na Uvuvi (AFDP) imewezesha Tafiti za Kiteknolijia kupitia
Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Nchini (TARI) katika kuzalisha mbegu za kisasa
zenye uwezo wa kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi.
Hayo
yamesemwa leo na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibi)
Mhe. Ummy Nderianaga wakati wa wasilisho la Taarifa ya Utekelezaji wa Programu
ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala
Katiba na Sheria, Bungeni Dodoma.
Akitolea
mfano aina ya mbegu sita za mahindi ikiwa ni Pamoja na Situka M1, TMV1, STAHA,
Bora, T104 na T105, kuwa zikipandwa kwa kufuata kanuni bora za kilimo
zinapelekea kuleta matokeao bora na Tafiti zinaonesha kuwa mbegu hizi zina
uwezo mkubwa wa ustahimilivu dhidi ya changamoto mbalimbali za mabadiliko
tabianchi.
Akiongelea
suala la usalama wa chakula, Naibu Waziri Nderianaga alisema kuwa suala hili
linakwenda sambamba na kipengele cha Usalama wa mbengu. “tulimaliza hivi punde
mkutano wa Chakula Afrika na Tanzania imeonekana kuwa ni kitovu kwenye suala la
chakula hivyo kama hatutakuwa na mbegu Bora na nzuri kufikia malengo itakuwa ni
kazi.” Alibainisha
Kwa
upande Mratibu wa Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) kutoka Ofisi ya
Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Bw. Salimu Mwinjaka, alisema katika sekta ya
Kilimo, Programu hii ya kimkakati inalenga kuongeza uzalishaji na upatikanaji
wa mbegu bora kwa wakulima, na jitihada kubwa ni kuweka miundombinu ya
umwagiliaji ili kuondokana na kilimo cha kutegemea mvua sambamba na kuihamasisha
jamii ya wakulima, umuhimu wa kutumia mbegu bora katika kuleta tija na mageuzi
ya kilimo.
Akiongoza
kikao hicho, Kaimu Mwenyetiki wa Kamati hiyo ya Kudumu ya Bunge ya Utawala
Katiba na Sheria, Mhe. Florent Laurent Kyombo Alisema “Tumeona mikakati Mizuri
ya Serikali ambayo imewekwa hasa katika suala la mbegu, hii ni kuhakikisha
kwamba suala zima la uzalishwaji wa mbegu bora na kwa wakati linafanikiwa.”
Akiongea
katika kikao hicho, Mhe. Boniphace Nyangindu Butondo (Mjumbe wa kamati)
alishauri Wakala wa Mbegu za Kilimo Nchini (ASA) kuwa na mkakati wa kuzalisha
mbegu zenye tija za kutosha na kuangalia mbegu za mazao mengine kama vile
Mtama, Mpunga na Pamba na kuzalisha mbegu za kutosha za Asili ili kuweza
kukabiliana na mabadiliko yoyote yanayoweza kutokea kwani mbegu nyingi za
kisasa zinaonesha kushambuliwa na wadudu mbalimbali.
Kwa Upande wake Mhe. Dkt. Alice Kaijage
(Mjumbe wa Kamati) Alishauri Wakala wa Mbegu za Kilimo Nchini (ASA) kuongeza
uwanda wa Tafiti hususani katika zao la Alizeti, kama linaweza kustawi bila
tatizo katika mikoa mingine tofauti na Singida, akitolea mfano Mkoa wa Pwani.
Awali
akiongelea suala la Mbegu la Asili, Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mbegu za
Kilimo Nchini (ASA) Dkt. Sophia Kashenge Kilenga, Alisema kuna nasaba nyingi
sana ya benki ya Mbegu za asili Mkoani Arusha,”Ni kweli kabisa Mbegu za Asili
zina sifa ambazo kila mtu anahitaji, na zina nasaba nyingi mchanganyiko
zinazopelekea ukuaji wa mbegu kwenda polepole na una mipaka, hivyo kwa ukuaji
wa sasa wa idadi ya watu ni vyema kuwa na maeneo maalum ambayo mbegu za asili
zitatumika na kwa kulisha idadi kubwa ya watu ni vizuri kutumika kwa mbegu
zinazozaa kwa wingi katika eneo dogo.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.