Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama ametoa wito kwa watendaji wa
Serikali; kujipanga na kuhakikisha Muongozo wa uwekezaji kwa Mkoa Manyara
unawafikia wananchi wote ili kufanya kazi kwa tija.
Kauli hiyo ameitoa Mkoani
Manyara wakati wa Ufunguzi wa wiki ya Kitaifa ya Vijana tukio alilolifanya kwa
niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa.
“Tunataka Muongozo huu uweze kutoa fursa nyingi kwa vijana
ili uweze kujenga kizazi ambacho kitatatumia Muongozo huu kwa muda mrefu”
alieleza.
Aliendelea kusema kuwa, Ofisi
ya Waziri Mkuu italeta timu ya baraza la uwezeshaji kiuchumi, timu ambayo
itasaidia kujenga uwezo kwenye dhana kutengeneza vitu asilia (Local content)
ili kuongeza tija na kuweka mazingira wezeshi yatakayochochea wanawekezaji.
“Makapuni yaliyowekeza katika Mkoa
wa Manyara yaone namna ya kutumia fedha zile zinazorudi kwa jamii, kwa kuwekeza
katika vikundi vya vijana wabunifu ili kupitia muongozo wa uwekezaji usaidie
kuleta tija kwa vijana na maendeleo ya Mkoa,” alihimiza
Akizungumza kuhusu madhimisho
ya wiki ya vijana, Mhe. Waziri Mhagama amesema ubunifu aliyouona wakati
alipotembelea Mabanda, hasa uliofanywa na kijana Said Mussa wa kubuni namna ya kutengeneza
taa za magari zilozoharibika na kurudisha katika muonekano mpya ni ubunifu
mzuri.
“Kijana Huyu wa Kitanzania
akifanikiwa kuhuisha teknolojia hiyo basi tutakuwa uwezo huko mbele kujenga
viwanda vidogo vidogo vingi vya kuzalisha taa za magari nakusaidia kuongeza
pato la kigeni na Kubrand Tanzania ya Mhe. Samia Kupitia Ubunifu wa Vijana,”
alisema.
Namshukuru sana Mhe. Mhe.
Prof. Joyce L. Ndalichako na Katibu Mkuu Mhandisi Cyprian John Luhemeja kwa
kuridhia kumpatia Mkopo kijana huyu ili kuhakikisha anafanya vizuri katika
ugunduzi alioufanya.
Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi vijana ajira
na Wenye Ulemavu) Mhe. Joyce Ndalichako amesema wiki ya vijana inalenga
kutambua Mchango wa Waasisi wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na
Hayati Shekh Abeid Amani Karume.
Ameongeza kusema Maadhimisho
ya wiki ya vijana Kitaifa ya Mwaka 2023 yanayofanyika Mkoani Manyara, kauli
mbiu yake ni,” Vijana na Ujuzi Rafiki kwa Mazingira na Maendeleo Endelevu”.
Maadhimisho ya vijana yanakutanisha vijana na wananchi wa Mikoa yote ya
Tanzania Bara na Visiwani ambapo vijana wanapata fursa ya kubadilishana uzoefu.
Ni fursa kwa Serikali na Wadau kutambua mchango mzuri wa vijana kwa maendeleo
ya nchi yetu.
“Natoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali na kuthamini
vijana wa Tanzania kwa matendo kwa kuhakikisha vijana wanapatiwa mitaji ya
kuendeleza biashara zao au kwa kuanzisha shughuli za maendeleo,” alibainisha
Awali Mkuu wa Mkoa wa Manyara
Bi, Queen Sendiga alimshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt,
Samia Suluhu Hassan kwa kuchagua Manyara kuwa Mwenyeji wa Kilele cha Madhimisho
ya Siku ya vijana kitaifa, Mwenyeji wa Misa Maalumu ya Kumbukizi ya Baba wa
Taifa, na Mwenyeji wa Killele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru.
“Moja ya mambo makubwa
yatakayoachwa katika Mkoa wa Manyara, kutokana na kuwa Mwenyeji wa kilele cha
Mbio za Mwenge wa uhuru ni pamoja na Ujenzi wa uwanja Mkubwa wa kisasa wa Mpira
wa Miguu ambao Umejengwa kwa hadhi,” alisema
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.