Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Utawala, Katiba na Sheria imepitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka
wa fedha 2024/25 ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya na
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.
Hayo yamesemwa na Makamu
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Florent Laurent Kyombo akikaimu nafasi ya
Mwenyekiti wa Kamati hiyo hii leo katika Ukumbi wa Mikutano wa
Bunge Jijini Dodoma mara baada ya wajumbe kujadili na kuridhia Bajeti katika
kikao kilichohusisha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria,
Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa
za Kulevya na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.
Alisema baada ya majadiliano
mazuri na maelezo ya ziada kutolewa
kuhusiana na Bajeti iliyotengwa, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala Katiba na Sheria imeridhia.
“Tunawatakia matumizi mema ya fedha hizi pale
zitakapokubaliwa kupitishwa katika vikao vya Bunge la Bajeti na tunahitaji kuona
Bajeti ya fedha hizi inaakisi matarajio ya msingi ya nchi yetu,” alibainisha.
Kwa Upande wake Naibu Waziri
Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga akizungumza
kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ameishukuru kamati kwa ushauri
na kupitia Bajeti hiyo kifungu kwa kifungu na kutoa maelekezo ambayo yatasaidia
Bajeti hiyo kukaa vizuri wakati kusomwa Bungeni kwenye vikao vya Bunge la Bajeti.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.