Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama amesema mahitaji ya virutubishi vya chakula ni ajenda kubwa ambayo itachochea katika kuongeza ajira kwa wakulima wetu na kuwa na uhakika na virutubishi tunavyovitumia hapa nchini.
Waziri amesema hayo
alipotemebelea na kukagua kiwanda cha Sanku kilichopo Mwenge Jijini Dar es
salaam leo tarehe 25/12/2024 na kujionea maendeleo ya kiwanda hicho cha uchanganyaji
wa virutubishi kwenye unga wa mahindi na ngano kwa bei nafuu.
Naomba muendeele kufanya
ufutailiaji wa karibu katika kutoa elimu ili kuondoa matatizo mengine ya
udumavu, utapiamlo na shida ya kupungukiwa vitamini A kwa wakinamama
wajawazito.
“Hii kazi ni kazi yenye
manufaa makubwa na itaweza kutusaidia sana kama nchi tuweze kusonga mbele na
kusaidia kuitangaza nchi kwa kuwa na kiwanda kikubwa cha kuchanganya
virutubishi,” alisema Waziri Mhagama
Kwa upande wake Meneja
Muandamizi wa Sanku Bw. Gwao Omari Gwao amesema kampuni yao inasaidia
wafanyabishara wadogo na wakati kufanya urutubishaji ambazo zimefunguliwa
katika Mikoa 26 Tanzania Bara na katika Halmashauri 142 Tanzania Bara.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.