Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania (SJMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) zitaendelea na
juhudi za kuimarisha dhana ya Ufuatiliaji na Tathmini kwa pande zote mbili za
Muungano hasa katika shughuli za Mipango ya Kitaifa na Miradi ya kimkakati
inayoendelea kutekelezwa hapa nchini.
Hayo yamesemwa na na Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla wakati akifungua Kongamano
la Tatu (3) la Kitaifa la Wiki ya Ufuatiliaji, Tathmini na Kujifunza kwa Niaba
ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt.
Hussein Ali Mwinyi liliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja
wa Ndege jijini Zanzibar.
Amesema Tanzania inaendelea
kupiga hatua katika uimarishaji wa shughuli za Ufuatiliaji na Tathmini ikiwemo
kuweka mifumo na miundombinu yenye kuwezesha utekelezaji wa shughuli za
maendeleo kwa Taasisi za Kitaifa zinazoratibu masuala hayo kwa maslahi mapana
ya nchi.
Makamo wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Mhe.Hemed amesema matumizi ya Teknoloji katika kufanya ufuatiliaji na
Tathmini kutaiwezesha Tanzania kufikia malengo ya kuimarisha uwajibikaji na kuongeza kasi na uwazi katika kuleta
ustawi wa wananchi kwa kutoa huduma sahihi za kijamii na kiuchumi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
amesema kuwa anatambua kuwa mafanikio makubwa yamepatika katika shuhuli za
ufuatiliaji na tathmini nchini hivyo amezitaka Mamlaka husika kufanya jitihada
za kukamilisha maandalizi ya Sera za Ufuatiliaji kwa Serikali zote mbili pamoja
na kutenga rasilimali za kutosha kuwezesha utekelezaji wa shughuli za
Ufuatiliaji na Tathmini.
Aidha amezitaka
Taasisi hizo kuhakikisha taarifa
zinazozalishwa kutokana na kazi za ufuatiliaji na tathmini zinatumika katika
kufanya maamuzi na kuweka mikakati imara ya kuhabarisha Umma juu ya matokeo ya
utekelezaji wa kazi za Serikali kwa kushirikiana na waandishi wa habari ili
kufikia malengo ya taasisi na Taifa kwa ujumla .
Sambamba na hayo Mhe. Hemed
ametoa wito kwa chama cha Wataalamu Afrika(AFrEA) kuendelea kuvilea vyama
vidogo vidogo vilivyomo nchi wanachama pamoja na kuapta fursa za kujifunza na
kujiimarisha ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Nae Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge Mhe. William Lukuvi amesema katika
kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo nchini kunahitaji uwepo wa taasisi
zenye kufanya Ufuatiliaji na Tathmini ili kusaidia kulinda matumizi ya rasilimali
fedha zinazotumika katika miradi hiyo.
Mhe. Lukuvi amesema kuwepo kwa Ufuatiliaji, Tathmini na
Kujifunza vinaakithi dhamira ya Serikali zote mbili ya kuhakikisha mabadiliko
na marekebisho makubwa yanafanyika katika kuimarisha Teknolojia na mifumo
ambayo itasaidia kufikia malengo yaliyowekwa na Serikali hizo kwa maslahi
mapana ya wananchi wa pande zote mbili za muungano.
Akizungumza kwa Niaba ya
Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Fedha na Mipango, Waziri wa Nchi Afisi ya Rais,
Uchumi na Uwekezaji (SMZ) Mhe. Sharif Ali Sharif amesema kufanyika kwa
Kongamano la Ufuatiliaji, Tathmini na Kujifunza hapa Zanzibar litaibua na kupendekeza
njia nzuri zaidi za kuimarisha Ufuatiliaji na Tathmini hasa katika masuala ya
Utalii na Uwekezaji nchini.
Mhe. Sharif amesema kufanyika
kwa Ufuatiliaji na Tathmini kunasaidia katika kupima shuhuli za mipango ya
maendeleo ya Kimataifa, kitaifa na Kikanda kwa kutathmini ufanisi na
uwajibikaji wa Taasisi husika hasa katika kupata taarifa na Takwimu sahihi
zenye matokeo chanya ya mipango hiyo.
Naye Katibu Mkuu Ofisi ya
Waziri Mkuu,Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi akieleza kuhusu kongamano
hilo amesema, Ofisi ya Waziri Mkuu imeendelea kuratibu makongamano hayo ikiwa
hilo ni la Tatu kufanyika na kuhudhuriwa na zaidi ya washiriki 650 na kusema ni
ongezeko kubwa linaloonesha muamko kwa washiriki kwa kulinganisha awamu
zilizopita ambapo Awamu ya kwanza walijitokeza washiriki 302, awamu ya pili
washiriki 624.
“Lengo ni kuendeleza jitihada za Serikali za kujenga uelewa
na utamaduni wa ufuatiliaji na tathmini kwa watendaji wa Serikali, Wadau na
Jamii kwa ujumla. Hivyo, Kongamano hili linawakutanisha wadau mbalimbali wa
kitaifa na kimataifa, na wadau wa Serikali na sekta binafsi wakiwemo watunga
sera, watekelezaji sera na wadau wa maendeleo kwa lengo la kujifunza na
kubadilishana uzoefu.
Aliongezea kuwa Kongamano hilo linatoa fursa ya
kukumbushana juu ya umuhimu na faida za ufuatiliaji na tathmini katika utendaji
wa Serikali.
“Ni matarajio yetu kongamano
litaleta matokeo mengi ikiwemo kuongeza ubunifu katika utendaji wetu, matumizi
ya TEHAMA pamoja na kuongeza weledi katika dhana hii ya ufuatiliaji na
tathmin,”alisema Dkt. Yonazi
Kwa upande wake Mwakilishi wa
USAID Tanzania Bw. Craig Hart ameeleza kuwa uwepo wa kongamano hilo unatarajiwa
kuleta matokezo zaidi katika shughuli za kila siku kwa kuzingatia matumizi ya
Teknolojia ya kisasa.
“Hakika wiki hii ni matarajio
yetu ilete matokeo yanayotarajiwa hivyo litumike kwa usahihi hasa kujifunza na
kuona namna ya kujitathim namna tunavyofanya kazi na ujuzi huu utumike kwa
kuimarisha utendaji kazi, tunaahidi kuendelea kushirikiana katika masuala
mbalimbali.
Naye Mtendaji Mkuu wa Mahakama
ya Tanzania Profesa Elisante Ole Gabriel akiwasilisha mada wakati wa Kongamano
hilo amesema kuwa,tathimin na ufuatiliaji ni jambo la msingi hivyo linapaswa
kuendelea kupewa kipaumbele kwa lengo la kusaidia namna ya kuendelea kuzitumia
malighafi tulizonazo, hivyo ni eneo muhimu sana katika shughuli zetu za kila
siku.
“Ufuatiliaji na tathmini ndiyo
njia pekee inayotusaidia kujua nini kiboreshwe na wapi penye kuhitaji mkazo kwa
kuzingatia umuhimu wake, hivyo hii ndiyo engeene muhimu yenye kutupa uwezo wa
kujitathmin,” alisema Profesa Elisante
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.