Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. William Lukuvi, amemuwakilisha Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika ibada
maalum ya kuwekwa wakfu kwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Tabora,
Mhashamu Josephat Jackson Bududu.
Ibada hiyo ya Misa Takatifu
imefanyika leo, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Theresia, Jimboni Tabora, na
kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, Kanisa na waumini kutoka maeneo
tofauti.
Katika hotuba iliyosomwa kwa
niaba ya Rais Samia, Mhe. Lukuvi amempongeza Askofu Bududu kwa kuteuliwa
kushika nafasi hiyo, akieleza kuwa Serikali inaendelea kuthamini mchango wa
taasisi za dini katika kuimarisha maadili, amani na maendeleo ya jamii.
Sherehe hiyo imehudhuriwa pia
na viongozi wa madhehebu mbalimbali, ikionyesha mshikamano wa kidini na kijamii
katika mkoa wa Tabora.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.