Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. William Lukuvi ameipongeza Wizara ya Maliasili
na Utalii kwa kutekeleza kikamilifu maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwa Wizara ya kwanza kukamilisha
ujenzi wa jengo la Ofisi na kuwezesha Idara na Vitengo vyake kuhamia Mji wa
Serikali Mtumba, Dodoma.
Waziri Likuvi ametoa pongezi
hizo leo alipotembelea Wizara hiyo kwa lengo la kukagua ujenzi wa Majengo ya
Serikali ambao ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu ya Serikali kuhamia Dodoma.
Mhe. Lukuvi amesema kuwa
Wizara ya Maliasili na Utalii licha ya kukamilisha mapema ujenzi wa jengo hilo,
inastahili pia kupongezwa kuwa wa kwanza kuhamia na kuwa mfano katika Matumizi
ya samani za Ofisini zilizozalishwa hapa nchini kupitia mazao ya Misitu.
"Ninyi ni mabalozi wazuri
wa Matumizi ya bidhaa zetu za hapa nchini zinazotokana na Misitu yetu, niimani
yangu kuwa Wizara zote zitaiga mfano huu". Aliongeza Mhe. Lukuvi
Aidha Mhe. Lukuvi ametoa rai
kwa watumishi wa Wizara hiyo kuhakikisha wanatunza vyema miundombinu na vifaa
vilivyopo ili viweze kudumu kama ilivyo kusudiwa.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya
Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbasi amemshukuru Waziri Lukuvi kwa ziara
yake, na kuahidi kuwa Wizara itatekeleza vyema maelekezo aliyoyatoa hususani ya
usimamizi mzuri wa Matumizi ya jengo na vifaa vilivyopo.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.