Friday, May 15, 2026

MHE.MMUYA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA MAWAZIRI WANAOSHUGHULIKIA MAAFA NCHI ZA SADC ULIOFANYIKA ZIMBABWE

 


Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Kaspar Mmuya ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Sita (6) wa Kawaida wa Kamati ya Mawaziri Wanaohusika na Usimamizi wa Maafa kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Mheshimiwa Profesa Palamagamba Kabudi unaofanyika Masvingo, Zimbabwe.

Aidha, Mkutano huo pamoja na masuala mengine umejadili maendeleo yaliyopatikana katika utekelezaji wa programu za kikanda na masuala ya kimkakati katika utekelezaji wa afua mbalimbali katika usimamizi wa maafa, pia mkutano huo utatumika kama jukwaa kwa Mawaziri kuimarisha ushirikiano na Washirika wa Maendeleo wa Kimataifa na Jumuiya ya Wafadhili kuhusu uwekezaji katika Usimamizi wa Maafa ili kujenga ustahimilivu wa kikanda.

Naibu Waziri Ameongozana na mwenyeji wake ambaye ni Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe Mhe. CP-Suzan Kaganda, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Dkt. Jim Yonazi, Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig.Jenerali Hosea Ndagala, Mkurugenzi Msaidizi Urasimishaji Makazi kutoka ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Nicholaus Mwakasege, Mratibu wa Maafa Dkt. Baltazar Leba, Bw. Abubakar Juma kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Msaidizi wa naibu waziri Bw. Blastus Kahemela, Msaidizi wa katibu mkuu Bw. Januari Kitunsi, pamoja na afisa habari Ofisi ya Waziri Mkuu, Bi. Nyamagory Kitwara.

Thursday, May 14, 2026

JUMUIYA YA UMOJA WA ULAYA YASHIRIKIANA (EU) NA SERIKALI KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI KIGOMA.


 Ofisi ya Waziri Mkuu-Sera, Bunge na Uratibu na wenye Ulemavu kupitia Idara ya Menejimenti ya Maafa kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya (EU) imeanza utekelezaji wa mradi wa Mwitikio wa Kikanda dhidi ya Uhamaji Unaotokana na Mabadiliko ya Tabia nchi  (Regional Responses to Climate Displacement in Subsaharan Africa- RE2CLID) unaolenga kujenga uhimilivu wa jamii zinazoishi maeneo yanayozunguka Ziwa Tanganyika mkoani Kigoma dhidi ya athari za mabadiliko ya tabia nchi.

 Mradi huo unafadhiliwa na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya(EU) Unatekelezwa na mashirika ya IOM UN migration, Enabel na kusimamiwa na Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara za kisekta pamoja na Mashirika yasiyo ya kiserikali kama vile RedCross umezinduliwa rasmi na Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Menejimenti ya Maafa Bw. Vonyvako Luvanda kwaniaba ya Naibu Katibu Mkuu Dkt.James Kilabuko, katika Hoteli ya Morena, Jijini Dodoma.

 Akizungumza katika uzinduzi huo Bw. Luvanda amesema, mradi huo unalenga kusaidia jamii zilizoathirika na kuhamishwa kutokana na kuongezeka kwa kina cha maji ya Ziwa Tanganyika pamoja na kuimarisha mifumo ya uratibu wa maafa na usimamizi wa rasilimali za asili.

 Pia, ameeleza kuwa mradi huo unaotekelezwa kwa kipindi cha miaka minne kuanzia mwaka 2025 hadi Septemba 2029 utaongeza uwezo wa jamii kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi huku ukipewa kipaumbele na Serikali pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo.

 Kwa upande wake, Mkuu wa Ushirikiano wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU) Tanzania Bw. Marc Stalmans amesema EU imefadhili mradi huo wenye thamani ya Euro milioni 13 kwa lengo la kusaidia jamii zilizoathirika zaidi na mabadiliko ya tabia nchi, hususan wananchi wanaoishi maeneo yanayozunguka Ziwa Tanganyika.

 Ameongeza kuwa, ongezeko la kina cha maji limeharibu makazi, mashamba, barabara pamoja na huduma muhimu kama maji safi na umeme, hali inayosababisha wananchi wengi kupoteza maeneo yao ya kuishi.

 Aidha, amesema mradi huo utasaidia kutambua maeneo hatarishi na kuweka mipango ya muda mrefu ya kuhimili athari za mafuriko pamoja na kugharamia ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya kijamii ikiwemo shule, hospitali, miradi ya maji na barabara zilizoathirika.

 Naye, Katibu Tawala Msaidizi Mipango na Uratibu Mkoa wa Kigoma Bw. Justin Njuu, amesema kuwa mradi huu  umekuja wakati muafaka kwani wananchi wengi wameendelea kuathirika kutokana na kuongezeka kwa kina cha maji ya Ziwa Tanganyika, hali iliyoharibu maeneo ya kilimo na makazi na kuwalazimu baadhi yao kuhama kwenda maeneo mengine.

 

 

Wednesday, May 13, 2026

TANZANIA YATOA SOMO KWA NCHI ZA SADC KUHUSU USIMAMIZI WA MAAFA


 TANZANIA imeendelea kung’ara katika Ukanda wa Kusini mwa Afrika baada ya kutajwa kuwa miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa mifumo madhubuti ya usimamizi wa maafa, hatua inayozifanya nchi nyingine wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kujifunza kupitia uzoefu wake.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Kaspar Mmuya wakati akimwakilisha  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Mhe.Prof. Palamagamba Kabudi wakati wa Mkutano wa Sita wa Kawaida wa Kamati ya Mawaziri Wanaohusika na Usimamizi wa Maafa kwa nchi wanachama wa SADC unaofanyika mjini Masvingo, Zimbabwe.

Amesema Tanzania imefanikiwa kuimarisha mifumo ya kuzuia, kupunguza madhara, kujiandaa na kurejesha hali baada ya maafa kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa katika sekta ya uratibu wa maafa nchini.

Kwa mujibu wa Mhe. Mmuya amesema moja ya mafanikio makubwa ni kuanzishwa kwa Kituo cha Ufuatiliaji wa Mwenendo wa Majanga na Tahadhari ya Mapema (National Emergency Operation and Communication Center Situation Room), ambacho kinafanya kazi saa 24 kila siku kufuatilia na kuchambua taarifa za majanga.

“Kwa kupitia kituo hiki, Serikali imeweza kupata taarifa za mapema kuhusu majanga yanayoweza kutokea, kufanya uchambuzi wa madhara na kuweka mikakati ya haraka ya kukabiliana nayo,” alisema Mhe Mmuya.

Aliongeza kuwa matumizi ya teknolojia ya kisasa katika ukusanyaji na uchambuzi wa takwimu za wakati halisi yamechangia kuongeza ufanisi wa maamuzi na kurahisisha utoaji wa taarifa rasmi kwa wananchi kuhusu namna ya kujiandaa dhidi ya maafa.

“Tunatumia takwimu za sasa na za zamani kutabiri hatari zinazoweza kujitokeza, jambo ambalo linaisaidia Serikali kupanga kwa usahihi hatua za kurejesha hali na kuendelea kulinda maisha ya wananchi,” alisisitiza

Aidha, aliwaalika wajumbe kutoka nchi wanachama wa SADC kutembelea Tanzania ili kujionea namna mifumo hiyo inavyofanya kazi pamoja na ubunifu unaotumika katika usimamizi wa maafa.

Mkutano huo wa siku nne umezikutanisha nchi 16 wanachama wa SADC pamoja na wataalamu wa kitaifa na mashirika ya kimataifa kujadili utekelezaji wa programu za kikanda za usimamizi wa maafa na namna ya kuimarisha ushirikiano wa kikanda.

Pamoja na mambo mengine, mkutano huo unatarajiwa kuwa jukwaa muhimu kwa mawaziri na washirika wa maendeleo kujadili uwekezaji katika sekta ya usimamizi wa maafa kwa lengo la kujenga ustahimilivu wa kikanda dhidi ya majanga mbalimbali yanayoendelea kujitokeza duniani.

Tuesday, May 12, 2026

NAIBU WAZIRI MMUYA AWASILI ZIMBABWE KUSHIRIKI MKUTANO WA SITA WA MASUALA YA MAAFA NCHINI ZIMBABWE



Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Kaspar Mmuya (Mb), amewasili nchini Zimbabwe kushiriki Mkutano wa Sita (6) wa Kawaida wa Kamati ya Mawaziri Wanaohusika na Usimamizi wa Maafa kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Mheshimiwa Profesa Palamagamba Kabudi unaofanyika Masvingo, Zimbabwe kuanzia tarehe 11 haadi 14 Mei, 2026.

Mara baada ya kuwasili, Mhe. Mmuya amepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini humo, Mhe. Balozi Suzan S. Kaganda na kuipongeza Tanzania kushiriki katika mkutano huo unaolenga kujadili maendeleo yaliyopatikana katika utekelezaji wa programu za kikanda na masuala ya kimkakati katika utekelezaji wa afua mbalimbali katika Usimamizi wa maafa kwa nchi za SADC.

Masuala mengine yaliyoelezwa na Mheshimiwa Balozi Suzani ni  pamoja na Tanzania kuendelea kuzitangaza fursa zilizopo ikiwemo sekta ya utalii, uchukuzi pamoja na kilimo  huku akiahidi kuendelea kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na Zimbabwe.

Sambamba na hayo, mkutano huo utahudhuriwa na wadau mbalimbali wa masuala ya Usimamizi wa Maafa kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ambapo ni fursa kwa Tanzania kuendelea kujitangaza Kimataifa kwa kuwa na mifumo thabiti ya Usimamizi wa Maafa pamoja na  kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya Menejimenti ya maafa.

Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizoshiriki katika Mkutano huo wa siku Nne ambapo umekutanisha wadau wa  masuala ya maafa kutoka nchi kumi na sita wakiwemo wataalamu kutoka  katika ngazi za Kimataifa pamoja na Mashirika ya Umoja wa Kitaifa.

SERIKALI YAPOKEA VIFAA VYA TEHAMA KUIMARISHA MFUMO WA KUKABILIANA NA MAAFA


 Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu kupitia Idara ya Menejimenti ya Maafa imepokea vifaa vya TEHAMA vyenye thamani ya shilingi milioni 120 kutoka Shirika la Chakula Duniani (WFP), kwa lengo la kuimarisha vituo vya operesheni na mawasiliano ya dharura pamoja na utekelezaji wa mfumo wa Anticipatory Action (AA).

 Vifaa hivyo vinavyojumuisha kompyuta za mezani, runinga kubwa tatu za inchi 100 pamoja na mashine za kuchapisha, vimekabidhiwa leo  katika hafla iliyofanyika katika ofisi za WFP jijini Dodoma na kuzinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule.

 Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Senyamule amesema Serikali inaendelea kuwekeza katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia ya nchi na majanga mbalimbali, huku akisisitiza umuhimu wa taarifa kuwafikia wananchi kwa wakati na kwa ufanisi.

 “Vifaa hivi vitaongeza ubora na ufanisi wa taarifa zinazowafikia wananchi kwa haraka ili waweze kuchukua tahadhari dhidi ya maafa yanayoweza kutokea,” amesema Mhe. Senyamule huku akiishukuru (WFP) kwa mchango wake katika kuimarisha sekta ya menejimenti ya maafa nchini.

 Kwa upande wake, Naibu Mwakilishi Mkazi wa (WFP) Bi. Christine Mendes amesema tafiti zinaonyesha kuwa uwekezaji katika maandalizi na kinga dhidi ya majanga ni nafuu zaidi kuliko gharama za kukabiliana na madhara baada ya majanga kutokea. Amesema ushirikiano huo unalenga kujenga ustahimilivu na maendeleo endelevu ya jamii.

Awali, Mkurugenzi Msaidizi wa Operesheni na Uratibu wa Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (SBUU), Kanali Selestine Masalamando amesema vifaa hivyo ni sehemu ya jitihada za Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuimarisha mfumo wa Taifa wa menejimenti ya maafa na kuongeza uwezo wa kukabiliana na majanga yanayoikumba nchi.

 Kanali Masalamando ameongeza kuwa vifaa hivyo vitasaidia kuimarisha ufuatiliaji wa vihatarishi, utoaji wa tahadhari za mapema, ukusanyaji na uchambuzi wa taarifa za maafa pamoja na kuboresha uratibu na mawasiliano kati ya ngazi ya Taifa, mikoa na wilaya wakati wa majanga.

 

Monday, May 11, 2026

TANZANIA KUENDELEA KUTUMIA AKILI UNDE KATIKA KUKABILIANA NA MAAFA

TANZANIA imesema itaendelea kutumia teknolojia ya Akili Unde (AI) katika kuimarisha mifumo ya usimamizi wa maafa nchini ili kuongeza ufanisi wa utoaji wa tahadhari za mapema na kupunguza madhara yanayosababishwa na majanga mbalimbali.

Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Dkt. Jim Yonazi, wakati wa mkutano wa maandalizi ya Mkutano wa Sita wa Kawaida wa Kamati ya Mawaziri Wanaohusika na Usimamizi wa Maafa kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika  mjini Masvingo, Zimbabwe.

Alisema matumizi ya AI yatasaidia uchakataji na ufuatiliaji wa taarifa mbalimbali zinazoripotiwa kuhusu masuala ya maafa nchini, hatua inayolenga kuongeza uwezo wa Serikali katika kufanya maamuzi ya haraka wakati wa majanga.

“Matumizi ya teknolojia ya Akili Unde yatawezesha uchambuzi wa taarifa kwa haraka, kutabiri hatari zinazoweza kujitokeza na kusaidia hatua za mapema za kukabiliana na maafa,” alisema Dkt. Yonazi.

Dkt. Yonazi alisema Serikali inaendelea kuweka mkazo katika maeneo muhimu yatakayosaidia kuwa na usimamizi wenye tija wa maafa ikiwemo utafiti wa kisayansi, matumizi sahihi ya Akili Unde, ushirikiano katika uhifadhi wa taarifa za matukio pamoja na matumizi ya menejimenti ya maarifa.

Aidha alisema Tanzania imeendelea kuwa mfano katika ukanda wa Kusini mwa Afrika kutokana na uwezo wake wa kuratibu na kusimamia maafa kwa mafanikio huku ikiendelea kuzuia, kupunguza madhara, kujiandaa na kurejesha hali pindi majanga yanapotokea.

Alifafanua kuwa mafanikio hayo yamechangiwa na uwepo wa Kituo cha Ufuatiliaji wa Mwenendo wa Majanga na Tahadhari ya Mapema ambacho hufanya kazi saa 24 kupokea, kufuatilia na kuchambua taarifa za majanga kwa wakati halisi.

“Kituo cha Operesheni ya Maafa kimekuwa msaada mkubwa kwani kimerahisisha upatikanaji wa taarifa za mapema, uchambuzi wa takwimu za wakati halisi na upangaji wa mikakati ya kurejesha hali pamoja na kutoa elimu kwa umma kuhusu namna ya kujiandaa na kukabiliana na maafa,” alisisitiza.

 

 

Wednesday, May 6, 2026

URASIMISHAJI WA UKALIMANI WA LUGHA YA ALAMA WASISITIZWA


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Watu Wenye Ulemavu), Mhe. Ummy H. Nderiananga (Mb), amesisitiza umuhimu wa kuharakisha urasimishaji wa tasnia ya ukalimani wa Lugha ya Alama ya Tanzania, ili kuhakikisha watu wenye ulemavu wa kusikia wanapata huduma kwa usawa.

Akifungua kikao cha mashauriano kilichoandaliwa na Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA), na kuhudhuriwa na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Wabunge pamoja na wadau mbalimbali, Jijini Dodoma, Mhe. Nderiananga amesema hatua hiyo itasaidia kuweka viwango vya taaluma, kuboresha mafunzo, na kutambua rasmi wakalimani wa Lugha ya Alama nchini.

Aidha, Mhe. Nderiananga amesema kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuandaa miongozo na kanuni zitakazosaidia kusimamia taaluma hiyo, huku akihimiza jamii kuongeza uelewa wa matumizi ya Lugha ya Alama, ili kuondoa vikwazo vya mawasiliano.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CHAVITA, Bi. Selina Mlemba amesema, urasimishaji wa tasnia ya ukalimani wa Lugha ya Alama ni hatua muhimu katika kuhakikisha haki za watu wenye ulemavu wa kusikia zinalindwa na kutekelezwa kwa vitendo.

Aidha Bi. Mlemba ameongeza kuwa CHAVITA itaendelea kushirikiana na Serikali pamoja na wadau wengine ili kuhakikisha kunakuwepo na miongozo, mafunzo, pamoja na mfumo rasmi wa usajili wa wakalimani wa Lugha ya Alama nchini, sambamba na hilo amesisitiza kuwa hatua hiyo itachangia kuongeza ubora wa huduma katika sekta mbalimbali na kuwezesha ushiriki kamili wa watu wenye ulemavu wa kusikia katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Washiriki wa kikao hicho wameitaka Serikali kuipa kipaumbele tasnia hiyo, wakisisitiza umuhimu wa ajira kwa wakalimani wa Lugha ya Alama katika sekta zote, pamoja na kuimarisha mafunzo na utambuzi wa taaluma hiyo ili kuboresha huduma kwa watu wenye ulemavu wa kusikia.

Friday, May 1, 2026

OFISI YA WAZIRI MKUU YASHIRIKI MAADHIMISHO YA MEI MOSI 2026 DODOMA

Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) wameungana na watumishi wengine wa Serikali kusherehekea Siku ya Wafanyakazi Duniani leo, Mei 1, 2026, katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Maadhimisho hayo yameongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, ambapo alisisitiza umuhimu wa wafanyakazi kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na kujituma ili kuchochea maendeleo ya taifa.

Amesema kuwa mchango wa wafanyakazi ni msingi muhimu katika kufanikisha malengo ya maendeleo ya nchi, hasa katika kuelekea utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Kaulimbiu ya mwaka huu ni: “Kazi Zenye Staha ni Nguzo Imara kwa Maendeleo Endelevu katika Utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050”, ikilenga kuhamasisha mazingira bora ya kazi na ustawi wa wafanyakazi nchini.



Thursday, April 30, 2026

SERIKALI YASISITIZA MATUMIZI YA MFUMO WA PD-MIS MKOANI ARUSHA


 Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu-Sera, Bunge, Uratibu na wenye Ulemavu imehimiza watendaji wa Halmashauri zote za Jiji la Arusha matumizi ya Mfumo wa ukusanyaji na usimamizi wa taarifa za watu wenye ulemavu.

Hayo yamesemwa katika Mafunzo yavitendo yaliyofanyika katika kata nne za jiji hilo ikiwa ni muendelezo na hitimisho la mafunzo ya mfumo wa PD-MIS yaliyowakutanisha wataalamu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu na maafisa ustawi wa jamii na TEHAMA jutoka Halmshauri zote za jiji la Arusha, yaliyochukua siku tatu ambapo makundi ya watu mbalimbali ya watu wenye ulemavu yamejitokeza kuitikia wito wa kujisajili katika mfumo.

Akizungumza wakati wa kilele cha mafunzo hayo, Afisa kutoka kitengo cha huduma kwa watu wenye ulemavu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Gerold Komba ametoa shukrani za dhati Uongozi wa Mkoa na Maafisa ustawi wa jamii na Maafisa TEHAMA kwa kushiriki kikamilifu katika mafunzo hayo tangu siku ya kwanza, Aidha aliwapongeza baadhi ya watu wenye ulemavu waliojitokeza kushiriki .

Amesisitiza kuwa ujuzi uliopatikana utakuwa nguzo muhimu katika kutekeleza majukumu ya msingi ya ukusanyaji wa na usimamizi wa taarifa za watu wenye ulemavu.

Mafunzo haya yanatazamwa kama hatua ya kimkakati ya kuhakikisha Maafisa na Watendaji  wanakuwa na uelewa mpana wa kutekeleza majukumu yao katika kuwahudumia watu wenye ulemavu ikiwa ni pamoja na kukusanya na kusimamia taarifa za watu wenye ulemavu mkoani humo,jambo litakalosaidia kuimarisha  upatikanaji wa takwimu sahihi na kuimarisha na kuobresha upatikanji wa huduma kwa watu wenye ulemavu na kuinua Uchumi kwa watu wa Kundi hili.



Wednesday, April 29, 2026

SERIKALI YASISITIZA USHIRIKI WA VIJANA KATIKA UKUAJI WA UCHUMI


Serikali imesisitiza kuwa, Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inatoa kipaumbele cha pekee kwa ushiriki wa vijana katika maendeleo, kwa lengo la kuinua vipaji, uwezo, na ari yao katika kufanikisha ukuaji wa uchumi jumuishi.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Prof. Palamagamba Kabudi,  leo jijini Dodoma wakati akifungua kongamano la kwanza la kisayansi la vijana kuhusu VVU/UKIMWI, afya ya uzazi, jinsia na masuala mtambuka. Kongamano hilo limeandaliwa na Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS).

Akizungumza katika hafla hiyo, Prof. Kabudi alisisitiza kuwa dhamira kuu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ni kujenga taifa lenye nguvukazi iliyoelimika, yenye ujuzi na maono.

"Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inatoa kipaumbele kwa vijana kwa kutumia vipaji na uwezo wao katika kufanikisha maendeleo endelevu. Nguvukazi hii itajengwa katika misingi imara ya ubunifu, ujasiriamali, na uwajibikaji," amesema Prof. Kabudi.

Katika hatua nyingine, Waziri Kabudi amebainisha kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeweka kipaumbele katika kushughulikia changamoto za ukatili wa kijinsia na afya ya akili.

Ameeleza kuwa, serikali imeanzisha madawati maalum ya ulinzi katika maeneo mbalimbali, ikiwemo shuleni, vyuoni, na kwenye ngazi ya jamii ili kuhakikisha huduma za kinga na msaada zinawafikia wahitaji kwa wakati.

Awali, akimkaribisha Waziri, Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Dkt. James Kilabuko, amebainisha umuhimu wa kongamano hilo kwa ustawi wa vijana.

"Kongamano hili ni chachu ya mabadiliko ya fikra na utendaji, tunatarajia elimu watakayopata itakuwa mwanzo wa safari ya kujenga jamii yenye afya, matumaini, na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi kwa mustakabali wao," amesema  Dkt. Kilabuko.

Kongamano hilo la siku mbili linaongozwa na kaulimbiu; ‘’Kuunganisha Sayansi na Ubunifu katika Kukabiliana na Janga la VVU, Afya ya Uzazi na Jinsia, Kukuza Ustawi Kuelekea Dira 2050”.




KAGERA KUNUFAIKA NA MPANGO WA MKOA WA AFYA MOJA

KAIMU Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Bw. Salum Kimbau amesema maandalizi ya Mpango wa Afya Moja kwa mkoa wa Kagera utaunufaisha mkoa huo kwa kuzingatia malengo yake ya kuboresha uratibu na utekelezaji wa Dhana ya Afya ya Moja na kuendelea kutatua changamoto zilizopo na zenye mwingiliano kati ya binadamu, wanyama na mazingira

Amezungumza hayo wakati akifungua kikao kazi cha wataalamu wa masuala ya Afya Moja kutoka sekta mbalimbali zikiwemo za afya, mifugo, mazingira, wanyamapori na kilimo ambao wamekutana katika Halmashauri ya Wilaya ya Muleba mkoani Kagera kwa siku tano kuanzia tarehe 27 Aprili hadi 01 Mei, 2026 ili kuandaa Mpango huo utakaotumika kubaini rasilimali zitakazosaidia kutatua changamoto na vihatarishi vya afya ya binadamu, wanyama na mazingira.

Bw. Kimbau amesema kuwa, mkoa utanufaika kwa uwepo wa Mpango huo kwani utaongeza tija katika kutatua changamoto zinazokabili sekta hizo hususan katika kuendelea kutatua changamoto za mwingiliano wa magonjwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu na binadamu kwenda kwa wanyama.

“Tunashukuru kuufikia mkoa wetu wa Kagera, tunajua kuwa asilimia 75 ya magonjwa yanatokana na mwingiliano ulipo kati ya wanyama na binadamu, hivyo kuandaliwa kwa mpango kutasaidia utekelezaji wa Dhana ya Afya Moja kwa kushirikiana pamoja, hivyo utatusaidia kutatua changamoto zilizopo na kuwa na jamii salama,” alisema Bw. Kimbau

Aliongezea kuwa ufanisi wa mpango huu unategemea ushirikishwaji wa sekta zote zinazohusika ili kuleta matokeo chanya.

Naye Mratibu wa Maafa kutoka Idara ya Menejimenti ya Maafa sehemu ya Afya Moja kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu Bi. Valentina Sanga amesema kuwa, Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Shirika lisilo la Serikali la CIHEB Tanzania kupitia Mradi wa Usalama wa Afya Duniani imeratibu maandalizi ya uwepo wa mpango huo huku akisihi kuunganisha nguvu ya pamoja katika kuhakikisha utekelezaji wake unaleta matunda yanayotarajiwa.

Aidha, aliwasihi wataalamu wa Masuala ya Afya Moja kutumia fursa hiyo kuja na Mpango utakaoinufaisha Kagera, kwa kuzingatia ni miongoni mwa Mikoa inayokumbwa na majanga ya mlipuko mengine yakichangiwa na mwingiliano wa wanyama na binadamu.

“Dhana ya Afya Moja (One Health) inatoa fursa ya kutambua uhusiano wa karibu kati ya afya ya binadamu, wanyama, na mazingira. Inasisitizwa kuendelea kujifunza zaidi dhana hii ili kutatua changamoto zilizopo zikiwemo za milipuko ya magonjwa na kuweza kuyakabili endapo yanatokea katika maeneo yetu,” alisisitiza Bi. Valentina

Aliongezea kuwa, Mpango huo utasaidia kutatua changamoto za masuala ya kiafya zinazotokea katika Halmashauri za mkoa wa Kagera, kujiandaa na kukabili majanga hayo ili kuwa na jamii salama kwa maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la CIHEB Tanzania, Bw. Mark Lwakatare alisema mradi wa Usalama wa Afya Duniani utaendelea kushirikiana na mikoa husika katika kuimairisha utekelezaji wa dhana ya Afya Moja ili nchi iweze kukabiliana na vihatarishi vya majanga mbalimbali.

“Mradi huu unashirikiana na Serikali kuboresha na kuimarisha utekelezaji wa afua mbalimbali kupitia dhana ya Afya Moja nchini, hivyo mradi utaendelea kushirikiana katika kujiandaa na kukabili athari katika afya ya binadamu, manyama na mazingira,” alisisitiza Lwakatare.

Tuesday, April 28, 2026

SERIKALI YAENDELEA KUIMARISHA MATUMIZI YA MFUMO WA PD-MIS KWA WATENDAJI ARUSHA


Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu imeendelea kuimarisha huduma kwa watu wenye ulemavu kwa kutoa mafunzo ya matumizi ya Mfumo wa Kielektroniki wa Ukusanyaji na Usimamizi wa Taarifa za Watu Wenye Ulemavu (PD-MIS) kwa watendaji wa mkoa wa Arusha.

Mafunzo hayo yametolewa na Wataalamu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kwenda kwa Maafisa Ustawi wa Jamii pamoja na Maafisa TEHAMA kutoka halmashauri mbalimbali za Mkoa wa Arusha kwa lengo la kuwajengea uwezo na kuimarisha matumizi ya mfumo huo katika ukusanyaji, uhifadhi na usimamizi wa taarifa sahihi za watu wenye ulemavu yamefanyika, katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Afisa kutoka Kitengo cha Huduma kwa Watu Wenye Ulemavu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Gerold Komba, alisema Serikali inaendelea kuhakikisha inaendelea kuweka mipango yake vizuri katika kuhakikisha kwamba kundi hili la watu wenye ulemavu linahudumiwa ipasavyo nchi nzima.

Alisema Mfumo huu wa PD-MIS kwasasa umeshasambazwa katika mikoa mbalimbali ambapo kwasasa mikoa yote ya Kanda ya ziwa, Magharibi na Kanda ya Kusini imeshafikiwa na Mfumo huu, na kwasasa Mfumo umeanza kanda ya kaskazini katika mkoa wa Arusha.

Kwa upande wake Afisa Ustawi wa jamii Mkoa wa Arusha Bw. Dennis Mgie ameishukuru Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuandaa mafunzo haya kwani kupitia Mfumo huu takwimu za mkoa zinakua zenye ufanisi lakini pia zitawaongoza kwenye kutoa huduma kwa watu wenye ulemavu.

"Takwimu hizi zitatusaidia kuweza kuwaunganisha watu wenye ulemavu na huduma na fursa mbalimbali ambazo serikali inawezesha watu wenye ulemavu ambao tutawatambua kwa hali zao na kazi zao kupitia mfumo huu". Amesema Bw. Mgie.

 

 





 

Saturday, April 18, 2026

WATUMISHI OFISI YA WAZIRI MKUU WAJENGEWA UWEZO UENDESHAJI HUDUMA NATIONAL CALL CENTER

Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) wamejengewa uwezo katika usimamizi wa mawasiliano kwa wananchi na mbinu bora za kuhudumia wananchi pamoja na matumizi ya mifumo ya kisasa ya National call centre.

Mafunzo hayo yamefanyika Jijini Dar es Salaam ambapo Muwezeshaji Bw. Willynevilline Msamo kutoka Benki ya NMB alieleza umuhimu uwezo wa kushughulikia mawasiliano kwa ufanisi na kuongeza kasi ya utoaji wa huduma ili kuhakikisha kila mwananchi anayewasiliana na taasisi anapata msaada unaostahili kwa wakati.

“Uanzishwaji na uimarishaji wa huduma za call centre, Ofisi ya Waziri Mkuu unalenga kutatua changamoto za wananchi kwa haraka kwa kuweka mfumo rahisi na wa moja kwa moja wa kupokea na kushughulikia maoni, malalamiko na mapendekezo yao,” alifafanua

Aidha huduma hii itawawezesha wananchi kupata mrejesho kwa wakati, kufuatilia masuala yao kwa ufanisi, pamoja na kuongeza uwazi na uwajibikaji katika utoaji wa huduma za serikali.

Bw, Msamo alisema, “hatua hii inaonesha dhamira ya Ofisi ya Waziri Mkuu ya kuendelea kuboresha mifumo ya mawasiliano na kuhakikisha huduma zinawafikia wananchi kwa haraka, kwa ufanisi na kwa viwango vya juu zaidi”.


Friday, April 17, 2026

SERIKALI YAKUTANA NA WADAU KUJADILI MIKAKATI YA KUIMARISHA MASLAHI YA WATU WENYE ULEMAVU TANZANIA

 


Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) imekutana na Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu, viongozi wa vyama vya watu wenye ulemavu pamoja na wawakilishi wa watu wenye ulemavu kutoka Mikoa mbalimbali ya Tanzania bara kwa lengo la kujadili masuala yanayohusu ustawi wa watu wenye ulemavu nchini.

Kikao hicho kilichofanyika Jijini Dar es salaam, kimelenga kujadili na kuimarisha uelewa kuhusu Mwongozo wa Uratibu wa Vyama vya Watu Wenye Ulemavu,kujadili rasimu ya Mwongozo wa Kitaifa wa Viwango vya Ufikivu, pamoja na kuongeza uelewa juu ya utekelezaji wa fursa ya asilimia 30 ya manunuzi ya umma kwa makundi maalum.

Akifungua kikao hicho, kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Watu Wenye Ulemavu, Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (SBUU), Bw. Bruno Mwakibibi, amesema kuwa Serikali inaendelea kujenga mazingira wezeshi na rafiki kwa kushirikiana na vyama vya watu wenye ulemavu ili kuongeza ustawi wa kundi hilo.

Aidha,amesisitiza umuhimu wa viongozi hao kuendeleza umoja, mshikamano na upendo ili kuhakikisha malengo ya kuwainua watu wenye ulemavu yanafikiwa sambamba na hilo amebainisha kuwa lengo kuu la hivyo ni kuwaunganisha wanachama, jamii na Serikali kwa manufaa ya pamoja.

Aliendelea kusema kuwa, mwongozo huo, pamoja na sera, sheria na kanuni zilizopo, unalenga kuongeza ushiriki na ujumuishwaji wa watu wenye ulemavu katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, ajira, siasa na afya, huku ukihakikisha hakuna kundi linaloachwa nyuma.

Akiwasilisha rasimu ya Mwongozo wa Viwango vya Ufikivu, Afisa Sheria kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Jacob Mwinula, amesema kuwa ufikivu unahusisha kuboresha mazingira, huduma na taarifa ili ziwe rafiki na kuwawezesha watu wenye ulemavu kuishi kwa kujitegemea na kushiriki kikamilifu katika jamii.

Aliongeza kuwa, mwongozo huo wa kitaifa wa Viwango vya ufikivu unalenga kuweka viwango mahsusi vya ufikivu katika sekta mbalimbali, kuchochea ushiriki jumuishi na wenye tija, pamoja na kuhakikisha mazingira yanakuwa fursa kwa watu wenye ulemavu badala ya vikwazo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu, Bi. Tungi Mwanjala, ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa elimu kuhusu fursa zilizopo kwa watu wenye ulemavu na kupokea maoni yao kuhusu changamoto wanazokutana nazo.

Amewahimiza washiriki kutumia kikamilifu fursa ya asilimia 30 ya manunuzi ya umma ili kuboresha hali zao za maisha na kuongeza ushiriki wao katika shughuli za kiuchumi.



Monday, April 13, 2026

DKT. MANYATTA:NGUVU YA PAMOJA YATAKIWA KATIKA MAFANIKIO YA DHANA YA AFYA MOJA


 Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Afya Moja kutoka Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu inayoshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Dkt. Salum Manyatta, amesema kuwa Mpango Mkakati wa Afya Moja umejikita kuhakikisha wananchi wananufaika kuanzia ngazi ya  Kaya hadi Taifa kupitia utekelezaji shirikishi wa sekta mbalimbali nchini ili kuhakikisha malengo yake yanafikiwa na kuwa na tija kwa jamii kwa ujumla.

Dkt. Manyatta ameyasema hayo mkoani Tanga wakati wa kikao kazi cha wataalam cha kuandaa Mpango wa Mkoa wa Afya Moja kilichoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Sehemu ya Afya Moja kwa kushirikiana na Shirika lisilo la Serikali la CIHEB Tanzania kupitia Mradi wa Usalama wa Afya Duniani.

Amesema kuwa lengo kuu la kikao hicho ni kuwajengea uwezo Watalamu ngazi ya mkoa kuhusu utekelezaji wa Dhana ya Afya Moja na kuwawezesha kutengeneza Mpango wa Utekelezaji wa Afya Moja wa Mkoa ambacho kitafanyika kwa siku tano kuanzia tarehe 13 hadi 17 Aprili 2026 katika Halmashauri ya Mji wa Korongwe, Mkoani Tanga.

Dkt. Manyatta ameeleza kuwa, lengo la dhana ya Afya Moja ni kupanua na kuimarisha ushirikiano baina ya sekta/taaluma mbalimbali katika hatua zote za kuzuia, kujiandaa na kukabiliana na milipuko ya magonjwa na hatari nyingine za afya zinazohitaji ushiriki wa sekta zaidi ya moja na taaluma mbalimbali.

“Ushirikiano huu pamoja na wadau wengine ikiwemo jamii, kimsingi unaongozwa na sekta/wizara za msingi (lead Ministries) ambazo ni Afya ya Binadamu, Wanyama (Mifugo na Wanyama Pori), Mazingira na Kilimo katika ngazi zote,” alifafanua Dkt. Manyatta.

Alifafanua kuwa, uwepo wa Mpango Mkakati ni muhimu kwani unatarajiwa kuweza kujibu na kutatua changamoto zilizopo katika Mkoa wa Tanga, hivyo utumike kama fursa ya kuhakikisha mkoa unakuwa na uelewa wa pamoja wa masuala ya Afya Moja kwa kuunganisha nguvu ya pamoja na kuweza kufanya kazi pamoja kwani hii ndiyo maana halisi ya dhana ya Afya Moja.

Naye Mwakilishi wa Katibu Tawala, ambaye ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt. Japhet Simeo amepongeza uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu kwa namna inavyoendelea kutoa elimu ya masuala ya Afya Moja, na kueleza kuwa mkoa wa Tanga utanufaika kwa uwepo wa Mpango Mkakati wa Afya Moja na kusisitiza kuwa Tanga itautekeleza kwa vitendo na kufanya mkoa  huo kuwa wa mfano

“Ifike mahali tutoke katika mambo ya concept to Action, yaani kuwa na mipango na mikakati ya namna hii na kuitekeleza na hiyo ndiyo umuhimu wa dhana Afya Moja,” alisisitiza Dkt. Simeo

Kwa upande wake, Msimamizi wa  Afya Moja na Mratibu wa Mradi wa Usalama wa Afya Duniani unaotekelezwa na Shirika lisilo la Serikali la  CIHEB Tanzania Dkt. Irene Massawe amesema kuwa, ushirikiano uliopo utasaidia kufanikisha malengo yaliyopo kwa nguvu ya pamoja na kuhakikisha matarajio ya uwepo wa mpango huo yanafika hadi ngazi za chini.

Aliongezea kuwa, sekta husika zikiungana kwa pamoja katika kutekeleza dhana ya Afya Moja itasaidia kudhibiti vihatarishi vya afya ikiwemo magonjwa ya mlipuko hasa yale yanayoweza kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu, yakiwemo ya kimeta, kichaa cha mbwa kwani itarahisisha na kuleta ufanisi katika kukabiliana na changamoto hizo.

“Tunaamini kuwepo kwetu ndani ya siku tano hizi Korogwe kutazaa matunda kwa washiriki wote kisha kuyaleta haya katika utekelezaji wa kila siku na kuhakikisha tunaleta matokeo chanya  ya mipango hii,” alisema Dkt. Irene.

AWALI

Afya Moja ni Dhana ya Kimataifa iliyoridhiwa na Shirika la Afya Duniani (WHO), shirika linaloshughulika na Afya ya Wanyama (OIE), Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Programu ya Kimataifa ya Mazingira (UNEP) kupitia “Global Health Security Agenda” (GHSA) na wadau wengine wa Afya duniani kote. Shirika la Afya Duniani (WHO), Shirika linaloshughulika na Afya ya Wanyama (OIE) na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) yamekuwa yakishirikiana duniani kote na kutoa wito kwa wataalamu wa sekta za Afya ya Binadamu, Wanyama na Mazingira kuongeza na kuimarisha ushirikiano na mawasiliano ili kuboresha ufanisi katika kukabiliana na tishio la magonjwa ya kuambukiza yanayoenea kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu na yanayovuka mipaka; tatizo la usugu wa vimelea vya magonjwa na changamoto zingine zinazokabili afya ya jamii zinazohitaji nguvu ya pamoja.

 

Thursday, April 9, 2026

PROF. KABUDI AKUTANA NA MJUMBE MAALUM WA KATIBU MKUU JUMUIYA YA MADOLA


 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Mhe.  Prof. Palamagamba Kabudi amekutana na Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Mhe. Lazarus Chakwera jijini Dar Es Salaam.

Mjumbe Maalum huyo yupo nchini kwa ziara ya kikazi ambapo atakutana na wadau mbalimbali jijini Dar Es Salaam, Dodoma na Zanzibar.

Wakati wa ziara hiyo ambayo itahitimishwa Aprili 16, 2026. Mhe. Chakwera amepangiwa miadi ya kukutana na viongozi wa Serikali, vyama vya siasa, asasi za kiraia na viongozi wastaafu.

Mhe. Chakwera aliwasili nchini Aprili 08, 2026 na kupokelewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Ngwaru Maghembe na alianza ratiba yake kwa kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo Aprili 09, 2026 jijini Dar EsSalaam.



MAKATIBU WAKUU WAKUTANA KUJADILI HALI YA UPATIKANAJI WA MAFUTA

 


Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Dkt. Jim Yonazi, ameongoza kikao cha Makatibu Wakuu kilicholenga kujadili hali ya upatikanaji wa mafuta nchini, hususan petroli na dizeli.

Kikao hicho kilichofanyika katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Jijini Dodoma, kimejadili kwa kina changamoto zinazoikabili sekta ya mafuta pamoja na hatua zinazoweza kuchukuliwa ili kuhakikisha upatikanaji wa nishati hiyo muhimu unaendelea kuwa wa uhakika.

Aidha, kikao hicho kilipokea na kuchambua taarifa ya kitaalamu kuhusu hali ya soko la mafuta, ikiwemo athari za mabadiliko ya kimataifa yaliyotokana na vita ya Iran, ambayo imeathiri mwenendo wa upatikanaji na bei za mafuta.

Washiriki wa kikao hicho walisisitiza umuhimu wa kuimarisha mikakati ya kitaifa ya kukabiliana na changamoto hizo, ikiwa ni pamoja na kuimarisha usimamizi wa akiba ya mafuta na kuongeza ufanisi katika mifumo ya usambazaji.

Serikali imeendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa soko la mafuta duniani ili kuchukua hatua stahiki kwa wakati, kwa lengo la kulinda uchumi wa nchi na kuhakikisha huduma muhimu zinaendelea kutolewa bila usumbufu.

SERIKALI YAZINDUA KIKOSI KAZI CHA TAIFA CHA UFUATILIAJI, TATHMINI NA UTOAJI TAARIFA

 


Serikali imezindua Kikosi Kazi cha Taifa cha Ufuatiliaji, Tathmini na Utoaji Taarifa (ME&R National Task Force) kwa lengo kuratibu utekelezaji wa Mwongozo Jumuishi wa Ufuatiliaji na Tathmini katika kusimamia utendaji wa shughuli za Serikali.

Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu Dkt. James Kilabuko  wakati akifungua Kikao Kazi Cha Kikosi Kazi cha Taifa cha Ufuatiliaji, Tathmini na Utoaji Taarifa (ME&R National Task Force) kilichofanyika mkoani Morogoro.

Dkt. Kilabuko amesema, Ufuatiliaji na Tathmini ni dhana muhimu ya usimamizi inayotumika kwa lengo la kuhakikisha uwajibikaji na uwazi katika utekelezaji wa afua za maendeleo.

“Kikosi Kazi hiki kitakuwa chombo cha kitaalamu cha kusaidia kuratibu utekelezaji wa Mwongozo Jumuishi wa U&Tc, kuoanisha mifumo ya kitaifa ya utendaji, kuimarisha ubora wa takwimu na taarifa za Serikali na  kuandaa mapendekezo ya sera na maboresho ya kiutendaji” alisema Naibu Katibu Mkuu huyo.

Ameeleza kuwa, kikao kazi hicho ni fursa ya kipekee ya kujifunza, kubadilishana uzoefu na kuweka mikakati ya pamoja ya namna bora ya kutekeleza majukumu ya  Ufuatiliaji na Tathmini nchini.

“Matarajio yangu ni kwamba, baada ya kikao hiki tutaboresha uratibu na kuoanisha viwango vya kitaifa vya Ufuatiliaji na Tathmini (M&E) katika Wizara, Idara na Wakala (MDAs), Sekretarieti za Mikoa (RSs) na Mamlaka za Serikali za Mitaa (LGAs) ni hatua muhimu katika kuhakikisha uwiano na ufanisi wa utekelezaji wa shughuli za maendeleo” amefafanua.

Vilevile, Dkt. Kilabuko amebainisha kuwa ipo haja ya  kuoanisha viashiria vya taasisi na maeneo muhimu ya matokeo ya Kitaifa ili kuhakikisha kuwa juhudi za taasisi mbalimbali zinaendana na vipaumbele vya Taifa.

 “ Katika hili, ni muhimu kuimarisha mwingiliano na utangamano wa Mfumo wa Kupima Utendaji Kazi wa Watumishi wa Umma na Taasisi (PEPMIS), PIPMIS na Mfumo wa Kitaifa wa Usimamizi wa Miradi ya Maendeleo na Programu (NPMIS) ili kuwezesha mtiririko mzuri wa taarifa na matumizi ya data kwa ufanisi” ameeleza.



Wednesday, April 8, 2026

WATENDAJI OFISI YA WAZIRI MKUU WAKUMBUSHWA KUIMARISHA WELEDI KUTIMIZA DIRA YA TAIFA 2050

Watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu wamekumbushwa kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa weledi, ufanisi na kujituma ili kuhakikisha wanachangia kikamilifu katika kufanikisha malengo ya Dira ya Taifa 2050, hususan katika maeneo ya sera, uratibu na usimamizi wa utekelezaji wake.

Wito huo umetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Mhe. Prof. Palamagamba J.A. Kabudi, wakati akizungumza na watumishi wa Ofisi hiyo mara baada ya kuwasili rasmi na kupokelewa na uongozi na watumishi wa Ofisi hiyo katika Jengo la Ngome Jijini Dodoma.

Prof. Kabudi alisisitiza umuhimu wa ushirikiano na ubunifu miongoni mwa watumishi ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi.

“Ni muhimu tushirikishane mawazo na kufanya kazi kwa pamoja ili kumsaidia Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufanikisha adhima ya maendeleo yenye kuleta ustawi na furaha kwa Watanzania," alisema Prof. Kabudi

Aliongezea kuwa upo umuhimu wa kushikamana ili kuendelea kuimarisha utendaji wetu ili kumwezesha Mheshimiwa Waziri Mkuu kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi zaidi.

Aidha, Waziri Kabudi alibainisha kuwa mazingira ya kazi yenye mshikamano na mahusiano ya kifamilia hayapaswi kuwa chanzo cha uzembe au utovu wa nidhamu, bali yawe kichocheo cha kuongeza uwajibikaji na kufikia viwango vya juu vya utendaji.

Katika hatua nyingine, Waziri Kabudi aliwataka watumishi kuendelea kumuombea aliyekuwa Waziri wa Nchi katika Ofisi hiyo, Marehemu William Vangimembe Lukuvi, ili Mwenyezi Mungu amrehemu na kumpa pumziko la milele.

“Nitaendeleza, kadri nitakavyoweza, misingi na jitihada zilizoanzishwa na mtangulizi wangu katika kuijenga Ofisi hii,” aliongeza.

Awali, Naibu Waziri wa Ofisi hiyo, Mhe. Ummy Nderiananga, alimpongeza Prof. Kabudi kwa kuaminiwa na kuteuliwa na Mheshimiwa Rais kushika nafasi hiyo, akiahidi ushirikiano wa dhati kutoka kwa watumishi wote katika utekelezaji wa majukumu yake.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Dkt. Jim Yonazi, naye alimpongeza Waziri Kabudi kwa uteuzi huo na kusisitiza kuwa watumishi wako tayari kuongozwa na kushirikiana naye katika kuendelea kuwahudumia wananchi kwa ufanisi.





 

WAZIRI KABUDI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA SPIKA WA BUNGE MHE. ZUNGU

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Profesa Palamagamba Kabudi (Mb), amekutana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb), katika Ofisi ya Spika Jijini Dodoma.

Katika kikao hicho, Dkt. Jim Yonazi, Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), alihudhuria na kushiriki katika mazungumzo hayo.

Wednesday, April 1, 2026

MAKATIBU WAKUU OFISI YA WAZIRI MKUU WAKIFUATILIA HOTUBA YA BAJETI

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) Dkt. Jim Yonazi (kushoto), Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano) Bi. Mary Maganga  pamoja na  Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) Bw. Sospeter Mtwale(kulia) wakifuatilia Hotuba ya Bajeti inayotolewa na Waziri Mkuu, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba kwa Mwaka 2026/2027 tarehe 1 Aprili, 2026 Bungeni Jijini Dodoma.

Tuesday, March 31, 2026

WANANCHI IDODI WAMLILIA LUKUVI


 WANANCHI wamlilia aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge Uratibu na Wenye Ulemavu na Mbunge wa Jimbo la Isimani Marehemu William Lukuvi kwa kazi nzuri alizozifanya wakati akitekeleza majukumu yake katika sekta mbalimbali serikalini na kuwaletea maendeleo katika nyanja mbalimbali.

Hayo yamelezwa kwa wakati tofauti hii leo wakati mwili wa marehemu Lukuvi ulipowasili Kijijini Kwake Kata ya Idodi, Wilaya ya Iringa  ambapo ndipo kunatarajiwa kuwa makazi yake ya milele mara baada ya ibada ya mazishi kijijini hapo.

Wananchi hao wameonesha simanzi kubwa na kumkumbuka kama kiongozi shupavu, na mtetezi wa wanyonge hususan kwa wakazi wa Jimbo Lake la Isimani Mkoani Iringa.

Akizungumza na waandishi wa habari Mmoja wa waombolezaji Bw. Kombo  Jumbe amesema Marehemu William Lukuvi aliasisi utaratibu wa kliniki za ardhi wakati akiwa anahudumu kama Waziri wa Ardhi na hivyo kuwezesha wananchi kuhudumiwa kwa  urahisi na kwa haraka.

“Marehemu Lukuvi alituwezesha sisi hupata huduma kwa haraka hasa zilizohusu masuala ya migogoro ya ardhi na kufanya kufikiwa kwa urahisi na watoa huduma katika wizara ya ardhi  na yeye ndiye aliyezindua upatikanaji wa hati za ardhi na kufanya zoezi lile kuwa endelevu” alieleza

Kwa upande wake Bw. Frank Mbindile Mkazi wa Kijiji cha Magozi Wilaya ya Iringa amesema Marehe William Lukuvi alikuwa ni mtu anayependa kusikiliza shida za watu kwa makundi na hata shida za mwananchi mmoja mmoja na kukiri kuwa wamepoteza mtu muhimu na Lulu kwa Taifa.

“Ni aina ya kiongozi anayeamini katika kusimamia mambo ya msingi kwa ajili ya maslahi mapana ya wananchi na akizungumza jambo alikuwa anauwezo wa kulisimamia, hivyo wanaisimani tumepoteza kiongozi mkubwa,” alieleza.