WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amefanya ziara kwenye mgodi wa dhahabu wa Buzwagi
uliopo wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga na kuchukua sampuli za mchanga
katika makontena mbalimbali kwa lengo la kwenda kuyapima kwa wataalamu
wa madini ili kubaini kiasi cha dhahabu kilichomo.
Amesema
wanataka kuona mchanga unaosafirishwa na mwekezaji huyo unakiasi gani
cha dhahabu, pia Serikali inataka kufahamu kama kodi inayolipwa ni
sahihi.” Hata hivyo tayari Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli alishatoa
tangazo la kuzuia usafirishaji wa michanga kwenda nje ya nchi,”.
Waziri
Mkuu alitembelea mgodi huo jana jioni (Jumatatu, Machi 27, 2017) na
kuchukua sampuli za mchanga kwa lengo la kuondoa mashaka juu ya
kinachosafirishwa. Sampuli hizo amezichukuwa kwenye makontena
yaliyofungwa kwa ajili ya kusafirishwa kwenda nje ya nchi.
“Tumeamua
kuchukua sampuli za mchanga ambao mwekezaj anasema wanaupeleka nje ya
nchi kwa ajili ya kwenda kutenganisha madini ya dhahabu na shaba. Hata
hivyo nimemuhoji kwa nini mitambo hiyo isiletwe nchini ili kila kitu
kifanyike hapahapa,”
Waziri
Mkuu amesema sera ya uwekezaji inasema mtambo huo unatakiwa uwepo
nchini ili kila hatua ya uchenjuaji ifanyike hapa hapa, hivyo tunataka
kujiridhisha na mwenendo wa mwekezaji na mapato tunayoyapata kama
yanastahili.
Aliongeza
kwamba “Hili lipo miongoni mwa masharti ya uwekezaji kwenye sekta ya
madini nchini kwamba mitambo hiyo ije kujengwa hapa nchini na itaongeza
fursa ya ajira na kukuza sekta nyingine ikiwemo ya kilimo,”.
Wakati
huohuo Waziri Mkuu amewataka Watanzania kuwa nasubira wakati Serikali
ikiendelea na zoezi la kuchunguza athari zitokanazo na kusafirisha
mchanga wa madini nje ya nchi. Pia amewatoa wasiwasi wafanyakazi katika
migodi na wamiliki kutowapunguza na badala yake waache waendelee na
majukumu yao.
Kwa
upande wake Meneja Uendelezaji wa mgodi huo Bw. George Mkanza alisema
mgodi huo ulionzishwa mwaka 2009 umeajiri watumishi 720 pamoja na
vibarua 500.
Alisema
kwa siku wanachenjua makontena matatu hadi sita ambapo katika kila
kontena moja wanapata kilo tatu za madini ya dhahabu na tani nne za
madini ya shaba.
Bw.
Mkanza alisema wanazalisha asilimia 50 ya madini ya dhahabu na asilimia
50 ya dhahabu iko kwenye mchanga na inakuwa imechanganyika na madini ya
shaba ambayo ndiyo unaosafirishwa kwenda nje ya nchi kwa ajili ya
kutenganishwa.
“Hapa
Buzwagi tuna makontena 179, makontena mengine 152 yako Dar es Salaam
kwenye bandari kavu ya Nazam na 21 yako bandarini. Kila siku
tunapoendelea kuzalisha tunakuwa na makontena manne hadi sita. Ndugu
zetu wa Bulyanhulu nao wanamakontena 108 yako mgodini na 104 yako Nazam
Cargo Dar es Salaam,” alisema.
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.