Wednesday, May 31, 2017

WAZIRI MKUU AHIMIZA UJENZI WA NYUMBA ZA BEI NAFUU

*Ataka VIGUTA iende kwenye halmashauri, ihamasishe watumishi
*Asema Watanzania wanataka nyumba bora, hawana muda wa kusimamia ujenzi
          
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezitaka Halmashauri za wilaya nchini ziangalie uwezekano wa kuwapatia watumishi wake nyumba za bei nafuu kwa malipo kidogo kidogo.

Amesema Halmashauri za wilaya kupitia mapato ya ndani, japo si makubwa zinaweza kuandaa mazingira yatakayowawezesha watumishi wake kupata nyumba kupitia mpango wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu unaofanywa na Muungano wa Vikundi vya Vicoba Tanzania (VIGUTA).

Ametoa wito huo leo (Jumatano, Mei 31, 2017) mara baada ya kutembelea maonyesho ya Mpango wa Ujenzi wa Nyumba za Waheshimiwa Wabunge (Low Cost Housing) yanayoendelea kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma. 
         
Waziri Mkuu aliwashauri  viongozi wa VIGUTA wafanye mawasiliano na Halmashauri zote na akawataka watenge muda wa kuzitembelea  Halmashauri hizo ili kuonyesha nia na uwezo wao wa kujenga nyumba za gharama nafuu ambazo malipo yake hulipwa kidogo kidogo kwa lengo la kuboresha maisha ya Watanzania.

“Watanzania wengi hivi sasa wanapendelea nyumba ndogo, nzuri na ambazo zimekamilika. “Wengi wao, na hasa wafanyakazi, siku hizi wana shughuli nyingi na hawana muda wa kujenga nyumba na kuzisimamia wenyewe kama zamani. Hivyo, wanahitaji makampuni yanayoweza kuwanjengea nyumba na wao wakalipa kidogo kidogo,” amesisitiza.
         
Aliwaaasa viongozi wa VIGUTA wahakikishe kuwa wanajenga nyumba zenye ubora unaokubalika ili waweze kuaminika hali ambayo itawawezesha kupata wateja wengi zaidi.

“Katika kipindi hiki ambacho Serikali inahamia Dodoma, Muungano wa Vikundi vya VICOBA au VIGUTA unayo nafasi kubwa ya kuwapatia watumishi wanaohamia nyumba za kuishi kupitia mpango wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu,” Waziri Mkuu alisema.

Alisema watumishi wengi wanaoingia gharama kubwa kwa kuishi katika nyumba za kupanga huku wakilipa kodi, sasa wamepata kimbilio kwani  wanaweza kujengewa nyumba kwa muda mfupi na kwa bei nafuu na wakalipa kidogokidogo kwa kipindi cha hadi miaka 15.

Naye, Mwenyekiti wa VIGUTA Taifa, Dkt. Salmin Ibrahim Dauda alimweleza Waziri Mkuu kwamba wana uwezo wa kujenga nyumba kwa gharama ya shilingi milioni 12, milioni 15, milioni 25 na milioni 60 kutegemeana na ukubwa wa nyumba.

Alisema wameweka viwango tofauti ili kuwawezesha Watanzania wenye kipato cha chini kumiliki nyumba zao wenyewe.

(

Tuesday, May 30, 2017

MAJALIWA ATEMBELEA MAONYESHO YA UJENZI WA NYUMBA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama picha za nyumba wakati alipotembelea Maonyesho ya Mpango wa ujenzi wa Nyumba za Gharama Nafuu kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma  Mei 30, 2017. Maonyesho hayo yameandaliwa na Muungano wa  Vikundi Vya Vicoba Tanzania (VIGUTA) .Kushoto  ni  Mwenyekiti wa Taifa wa VIGUTA, Dkt. Salmin Ibrahim Dauda.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama picha za nyumba wakati alipotembelea Maonyesho ya Mpango wa ujenzi wa Nyumba za Gharama Nafuu kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma  Mei 30, 2017. Maonyesho hayo yameandaliwa na Muungano wa  Vikundi Vya Vicoba Tanzania (VIGUTA) .Kushoto  ni  Mwenyekiti wa Taifa wa VIGUTA, Dkt. Salmin Ibrahim Dauda.


Monday, May 29, 2017

BUNGENI LEO MEI 29,2017

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wabunge wa Viti Maalum, Asha Abdullah Juma (kushoto) na Taska Mbogo kwenye Jengo la Utawala la Bunge mjini Dodoma Mei 29, 2017.


Sunday, May 28, 2017

RAMADHAN KAREEM

Salaam za kheri ya mfungo wa Ramadhani  kwa Waislam wote Duniani kutoka kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Mheshimiwa Kassim Majaliwa.

Friday, May 26, 2017

MATUKIO PICHA BUNGENI LEO 26 MEI,2017

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Mbulu  Vijijini, Fratei Massay kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Mei 26, 2017. Wapili kulia ni Mbunge wa Iramba Mashariki, Allan Kiula.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wanachuo wa Chuo Kikuu cha Makumira kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Mei 26, 2017. Kushoto ni  Mbunge wa Newala Mjini, Capt. George Mkuchika.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Wabunge wa Viti Maalum, Amina Makiragi na Anna Lupembe kwenye jengo la Utawala la Bunge mjini Dodoma Mei 26, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Viongozi wa Chama cha Wafanyabiashara wa Pikipiki na Vipuri  vyake pamoja na baadhi ya wabunge, ofisini kwake, Bungeni mjini Dodoma Mei 26, 2017. Kulia kwake ni Waziri wa Fedha na Uchumi, Dkt. Philip Mpango. 


Tuesday, May 23, 2017

MAJALIWA: BENKI VIKOPESHENI VIKUNDI VYA WAKULIMA


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezitaka benki mbalimbali nchini ikiwemo Benki ya Maendeleo ya Kilimo kutoa mikopo kwa vikundi vya kilimo ili viweze kupata fedha za kununulia matrekta.

Amesema Serikali imedhamiria kuimarisha Sekta ya kilimo ili kwenda sambamba na adhma yake ya kuwa nchi ya uchumi wa viwanda.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumanne, Mei 23, 2017) wakati alipotembelea kiwanda cha kuunganisha Matrekta URSUS-TAMCO, Kibaha mkoani Pwani.

Amesema kiwanda hicho kinalenga kuboresha sekta ya kilimo nchini na kuongeza uzalishaji wa malighafi za viwandani kwa kuwa wakulima watakuwa na zana za kisasa.

Aidha, amevitaka vyuo vya kilimo nchini kununua matrekta hayo kwa lengo la kufundishia wanafunzi wake ili wanapohotimu wawe na uwezo wa kutumia zana hizo vizuri na kwenda kuwasaidia wakulima katika maeneo yao.

Pia Waziri Mkuu ametoa wito kwa Halmashauri nchini kuendelea kupanga matumizi bora ya ardhi kwa kutenga maeneo ya kilimo, uwekezaji, makazi, biashara na huduma za jamii, hivyo kuepuka migogoro ya ardhi kwa siku zijazo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Bw. Mlingi Mkucha amesema wataunganisha matrekta 2,400,  harrow 2,400 na majembe 2,400 katika mradi huo wa kiwanda cha kuunganisha matrekta URSUS-TAMCO ikiwa ni mkataba wa awali.

Amesema kiwanda hicho kina wafanyakazi 27 kwa hatua za mwanzo. Aidha, idadi hiyo itaongezeka kutokana na mahitaji ambapo baadhi ya wafanyakazi watapewa mafunzo nchini Poland na watakaporudi watakuwa wakufunzi wa watakaoajiriwa.

Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa kiwanda hicho kimeazima wafanyakazi wengine wakiwemo watano kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, 10 kutoka vyuo mbalimbali vya ufundi nchini, wawili kutoka CAMARTEC ambao wanashirikiana na wataalamu 10 kutoka URSUS kuunganisha matrekta.

Bw. Mkucha amesema wafanyakazi 10 kutoka Tanzania wanatarajiwa kwenda nchini Poland kufanya mafunzo mahsusi na watakaporejea watakuwa wakufunzi kwa watumishi wengine watakaoajiriwa katika kiwanda hicho.

Amesema mbali na ujenzi wa kiwanda hicho cha kuunganishia matrekta ya URSUS, mradi unahusisha uanzishwaji wa vituo vinane kwa ajili ya kutoa huduma kwa wateja na kuuzia matrekta, zana na vifaa vingine.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Everest Ndikilo amesema miongoni mwa changamoto zinazoikabili sekta ya viwanda mkoani humo ni pamoja na kukatika kwa umeme, hivyo ameliomba Shirika la Umeme Tanzania (TANECO) kuongeza vituo vya kupozea umeme.

Awali Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mheshimiwa Charles Mwijage amesema kwa sasa nchini kuna viwanda vikubwa 393 kati yake 84 viko mkoani Pwani, ambapo amewaomba viongozi wa mkoa huo kutenga maeneo kwa ajili ya wanawake na vijana kuanzisha viwanda vidogo.

Mara baada ya kutembea kiwanda cha kuunganisha matrekta URSUS-TAMCO Waziri Mkuu alitembelea eneo la uwekezaji la Kamal (Kamal Indusrial Estate) lililoko katika Kata ya Kerege wilayani Bagamoyo.

MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA KUUNGANISHA MATREKTA YA URSUS KILICHOPO KIBAHA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Bagamoyo wakati alipotembelea eneo la uwekezaji la Kamal Industrial Estate lililopo Kerege mkoani Pwani Mei 23, 2017.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama moja kati ya mtrekta aina URSUS yanayounganishwa kwenye karakana ya TAMCO mjini Kibaha Mei 23, 2017.Kulia  kwake  ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji,  Charles Mwijage.

Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akikagua matrekta aina ya URSUS yanayounganishwa katika karakana ya TAMCO mjini Kibaha Mei  23, 2017. Wengine pichani kutoka kulia kutoka kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NDC Mlingi Elisha Mkucha, Waziri wa Viwanda, Biahara na Uwekezaji, Charles Mwijage, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evaresti, Ndikilo na kulia kwake ni Mbunge wa Kibaha mjini Silvestry Koka.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama moja kati ya mtrekta aina URSUS yanayounganishwa kwenye karakana ya TAMCO mjini Kibaha Mei 23, 2017.Kulia  kwake  ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji,  Charles Mwijage.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkurugenzi  Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka baada ya kutembelea eneo la uwekezaji la Kamal Industrual Estate lililopo Kerege, Bagamoyo Mei 23, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya viongozi, wabunge na wananchi waliohudhuria wakati alipotembelea eneo la uwekezaji la Kamal Industrial Estate lililopo Kerenge, Bagamoyo Mei 23, 2017. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya viongozi, wabunge na wananchi waliohudhuria wakati alipotembelea eneo la uwekezaji la Kamal Industrial Estate lililopo Kerenge, Bagamoyo Mei 23, 2017. 


Saturday, May 20, 2017

MAJALIWA AMTEMBELEA RAIS MSTAAFU MKAPA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa wakati alipomtembelea Rais huyo Mstaafu  nyumbani kwake jijini Dar es salaam Mei 20, 2017. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa wakati alipomtembelea  Rais huyo Mstaafu nyumbani kwake jijini Dar es salaam Mei 20, 2017. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa wakati alipomtembelea Rais huyo Mstaafu  nyumbani kwake jijini Dar es salaam Mei 20, 2017.


Wednesday, May 17, 2017

WAZIRI MKUU KATIKA MATUKIO PICHA BUNGENI LEO 17 MEI,2017

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Kavuu, Dkt. Pudenciana Kikwembe kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Mei 17, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na mbunge wa Viti Maalum, Cecilia Pareso kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Mei 17, 2017.
 Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Morogoro Kusini, Prosper Mbena kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Mei 17, 2017.

Saturday, May 13, 2017

WMA REKEBISHENI MIZANI KWENYE MAGHALA YA KOROSHO-MAJALIWA


*Serikali kugawa salpha bure kwa wakulima wa korosho

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkurugenzi wa Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) kuhakikisha wanafanya marekebisho ya mizani katika maghala ya kuhifadhia korosho ili kuepuka changamoto ya kutofautiana kwa uzito wa bidhaa hiyo kila inapofikishwa kutoka katika vyama vya msingi.

Amesema kitendo cha mizani za kwenye maghala hayo kupunguza uzito wa korosho zinazopelekwa kutoka kwenye Chama cha Ushirika cha Msingi (AMCOS) hakivumiliki, hivyo Wakala wa Vipimo ipendekeze aina ya mizani zitakazotumika katika upimaji wa korosho.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumamosi, Mei 13, 2017) wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wadau wa Tasnia ya Korosho uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma.

“Kuna jambo baya sana linaendelea kila korosho inayofikishwa katika ghala kuu lazima kilo ziwe zimepungua kwa zaidi ya kilo mia moja mpaka elfu, kwa nini korosho tani kumi zikiletwa kwenye mizani yenu zinasoma tani nane kwa nini?

“Na huwa haitokei ikasoma tani kumi na mbili, wakati wote huwa inasoma chini tu, watu wa WMA mpo fanyesni marekebisho, haiwezekani tukavumilia wizi huu. Huna mkorosho hata mmoja lakini mwaka huu utasikia umeuza tani zaidi ya elfu tano.
Jambo hili lisijitokeze tena,” amesisitiza.

Aidha, Waziri Mkuu amesema Serikali imeendelea kuimarisha na kuboresha utaratibu wa stakabadhi ghalani na kupambana na biashara ya kangomba, hivyo viongozi wa Mikoa inayolima korosho wahakikishe  wanawashughulikia watu wote watakaobainika kushiriki kwenye biashara hiyo bila ya kujali wadhifa wao.

 Amesema mwelekeo wa Serikali kwenye sekta ya kilimo ni kuhakikisha kuwa kilimo kinakuwa sehemu muhimu ya kuimarisha uchumi, kuongeza kipato cha mkulima na kuchochea ukuaji wa viwanda ili kuongeza ajira.

Kwa upande wake, Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba amesema takwimu zilizotolewa na Benku Kuu ya Tanzania (BoT)  mwezi Februari mwaka huu, zinaonyesha zao la korosho linaongoza kwa kuliingizia Taifa fedha za kigeni. Zao la korosho  limeliingizia Taifa Dola milioni 346.6, likifuatiwa na zao la tumbaku dola 276 na kahawa dola 152.9.

“Zao la korosho linakuwa zao kuu la biashara nchini na tayari mikoa ya Dodoma, Morogoro, Iringa, Njombe na Mbeya imeanza kulima, hivyo kuongeza idadi ya mikoa inayolima zao hilo nchini na kufikia 11 na wilaya 40,” amesema.

Aidha, Dkt. Tizeba ameitaka Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) kuhakikisha inakuwa makini na viuatilifu vinavyoingizwa nchini kwa kuvipima kwa kutumia wataalamu wa Serikali ili kujiridhisha ubora wake kabla ya kuwafikishia wakulima.

Pia Dkt. Tizeba amesema katika msimu wa mwaka huu Serikali itagawa salpha bure kwa wakulima wa zao la korosho kwa ajili ya kupuliza kwenye mikorosho yao ili isishambuliwe na wadudu.

MKUTANO WA WADAU TASNIA YA KOROSHO- DODOMA

Waziri Mkuu  Kassim  Majaliwa  akimsikiliza kwa makini  Mwenyekiti  wa  Bodi ya Korosho , Mama  Anna  Abdala  baada ya Ufunguzi wa  Mkutano  Mkuu  wawa Dau wa Tansnia  ya Korosho  Nchini katikati ni Waziri wa Kilimo ,Mifugo na Uvuvi  Dr Chales  Chizeba  , Waziri Kuu  amefungua Mkutano huo  May 13, 2017 katika  Ukumbi wa  Chuo cha Mipango   Mkoani  Dododma.
Wadau  wa Tasnia ya Korosho   wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  wakati wa ufunguzi wa Mkutano  Mkuu  wawa Dau wa Tansnia  ya Korosho  Nchini  ambao  umefunguliwa  na Waziri Mkuu  May 13, 2017 katika  Ukumbi wa  Chuo cha Mipango   Mkoani  Dododma.

Waziri  Mkuu  Kassim  Majaliwa  akihutubia    wakati wa ufunguzi wa Mkutano  Mkuu  wawa Dau wa Tansnia  ya Korosho  Nchini  ambao  umefunguliwa  na Waziri Mkuu  May 13, 2017 katika  Ukumbi wa  Chuo cha Mipango   Mkoani  Dododma 

Thursday, May 11, 2017

MATUKIO PICHA BUNGENI LEO MEI 11,2017

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni Freeman Mbowe, bungeni mjini Dodoma Mei 11, 2017 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu maswali ya papo kwa papo Bungeni mjini Dodoma Mei 11, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Rombo Roman Joseph Selasini,kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Mei 11, 2017, katikati ni Mbunge wa Vunjo na Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi James Francis Mbatia
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Nchi,  Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama bungeni mjini Dodoma Mei 11, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijadili jambo na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu bungeni mjini Dodoma Mei 11, 2017. 


HUDUMA ZA AFYA ZISIFUNGWE WAKATI WA ZOEZI LA USAFI-MAJALIWA


WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa ngazi mbalimbali waweke utaratibu utakaoruhusu huduma za afya kuendelea kutolewa kwa wananchi katika maeneo yao hata kama zoezi la usafi la kila mwezi litakuwa linaendelea.

Serikali imeweka utaratibu wa wananchi kushiriki katika shughuli za usafi wa mazingira siku ya Jumamosi ya mwisho wa mwezi, zoezi ambalo linashirikisha watu wote wakiwemo wafanyabiashara na watoa huduma nyingine zoezi linalofanyika kuanzia saa 12.00 asubuhi hadi saa 4.00 asubuhi.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Mei 11, 2017) Bungeni mjini Dodoma katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu wakati akijibu swali la Mheshimiwa Abdallah Ulega mbunge wa Mkuranga.

Mheshimiwa Ulega alitaka kupata kauli ya Serikali kuhusu maeneo ya kutolea huduma mbalimbali zikiwemo za afya ambayo hufungwa wakati wa zoezi la usafi linalofanyika kila mwezi nchini, jambo linalosababisha kero kwa wagonjwa na wengine wenye dharula.

Waziri Mkuu amesema “Hospitali na maeneo mengine ya kutolea huduma za afya hayawezi kufungwa, viongozi wa maeneo husika waweke utaratibu mzuri utakaoruhusu huduma hizo ziendelee kutolewa bila ya kuathiri zoezi la usafi wa mazingira,”.

Katika hatua nyingineWaziri Mkuu amesema Serikali imeagiza tani 131,000 za sukari ili kukabiliana na upungufu uliopo nchini. Amesema Serikali iko macho na inajua maeneo yanayohitaji kuboreshwa kulingana na mahitaji.

 “Mahitaji ya sukari nchini kwa mwaka ni tani 420,000, ambapo tunazalisha tani 320,000, hivyo tunaupungufu wa tani 100,000 hata hivyo tumeagiza tani 131,000 na tayari tani 80,000 zimewasili nchini, ambapo kati yake tani 35,000 zimeingizwa sokoni,” amesema.

Ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali lililoulizwa na Mheshimiwa Jaku Hashim Ayoub aliyetaka Serikali iwahakikishie wananchi upatikanaji wa sukari hususan katika kipindi cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani unaotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu.

Wednesday, May 10, 2017

WAZIRI MKUU AKIWA BUNGENI KATIKA MATUKIO PICHA LEO MEI 10,2017

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na wabunge Mussa Ntimizi wa Igalula na Felista Bura wa Viti Maalum, bugeni mjini Dodoma Mei 10, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijadili jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, George Simbachawene kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma, Mei 10, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aizungumza na wabunge, Kange Lugora wa Mwibara (kushoto)  na Katani Ahmed Katani wa Tandahimba (katikati) kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Mei 10,2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na Mbunge wa Geita, Joseph Kasheku Musukuma (katikati) na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Mei 10, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum, Mwanne Mchemba (kushoto) na Mbunge wa Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Mei 10, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Mtwara Vijijini Hawa Ghasia kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Mei 10, 2017.


BUNGENI LEO 10 MAY,2017

Waziri wa Nchi,  Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akiteta na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi, Hamad Masauni, bungeni mjini Dodoma Mei 10, 2017.
Waziri wa Maji, Mhandisi Gerson Lwenge  akwasilisha Makadiro ya Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2017/18, bungeni mjini Dodoma, Mei 10, 2017. 
 Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akiteta na Naibu Waziri wa mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi, Hamad Masauni  na Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega bungeni mjini Dodoma Mei 10, 2017.
Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum, Upendo Pendeza kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Mei 10, 2017. 


Tuesday, May 9, 2017

BUNGENI LEO 09 MAY,2017

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa zamani, Lawrence Masha kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Mei 9, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Kiembesamaki, Ibrahim Raza kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Mei 9, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Songea Mjini, Leonidas Gama kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Mei 9, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Spika wa Bunge, Job Ndugai kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Mei 9, 2017. Katikati ni Mbunge wa zamani, Hezekia Wenje.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Sengerema, William Ngereja kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma, Mei 9, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Spika wa Bunge, Job Ndugai kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Mei 9, 2017.