Program ya Miundo mbinu ya
Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF) imewajengea
uwezo wakulima 56,637 mkoani Kagera kwa kuwawezesha kujiongezea kipato na
kujikwamua kiuchumi.
Hayo yamesemwa na Mhasibu
Mkuu wa Benki ya Wakulima ya Ushiriki Kagera (KFCB) Bi. Adelina Kilaja tarehe
17 Mei, 2017 mkoani Kagera, wakati wataalamu wa MIVARF walipotembelea Benki
hiyo na kujionea maendeleo yaliyofikiwa na benki hiyo kupitia uwezeshaji kutoka
Programu ya MIVARF.
MIVARF imekwamua shughuli
za Benki ya (KFCB) na kuwaongezea wigo mpana wa kuwahudumia wananchi kwa wingi
zaidi ambapo awali haikuwa rahisi. “Program
ya MIVARF umetuwezesha kuhamia katika mfumo wa Tehama ambao umerahisisha
utendaji wetu wa kazi kwa kiwango kikubwa Zaidi, alieleza Kilaja”.
Benki yetu wateja wake
wengi ni wavijijini, ambao ni Wakulima na Wafugaji hivyo benki imefanikiwa kuwajengea
uwezo katika masuala ya Akiba na Mikopo, elimu ya kilimo bora, hii
isingewezekana bila uwezeshaji kutoka MIVARF uliowawezesha wakulima hao
kujikwamua katika maisha yao na kuwaongezea kipato, alisema Kilaja.
Aidha, alifafanua kuwa kabla
ya program ya MIVARF, benki ya KFCB ilikuwa na wateja wa moja kwa moja 7132 kwa
Desemba 2016 na wateja wa vyama vya
Akiba na Mikopo walikuwa 26,874 kutokana na uwezeshaji wa MIVARF idadi ya wateja
hao imefikia 56,637 Desemba 2016.
“Asilimia
70 ya wateja wetu tunaowahudumia ni wakulima wadogowadogo ambao hujishughulisha
na kilimo cha Maharage na Mahindi kwa wingi. Ili kuhakikisha huduma inakuwa
bora MIVARF imewajengea uwezo wafanyakazi wa benki hii na kutuboreshea mfumo wa
uendeshaji wa kibenki ambapo benki imeweza kuanzisha huduma za Uwakala za
kibenki pamoja na sim banking” Alisisitiza Kilaja.
Akifafanua Meneja wa IBUGA
SACCOS Brighton Ferdinand alikiri kuboreshwa kwa huduma za utoaji mikopo katika
SACCOS yao na kushukuru Benki ya KFCB kwa mkopo walio wapatia wa milioni 101 ambao
umewasaidia kuongeza wigo wa utoaji huduma kwa wakulima Mkoani Kagera katika
Wilaya ya Muleba.
Aidha, baadhi ya wanufaika
wa Mikopo hiyo wameeleza kuwa kutokana na mikopo waliyoipata kutoka katika
vyama vya Akiba na Mikopo wameweza kuendeleza kilimo chao kwa tija na kuongeza
kipato hali iliyowezesha kumudu gharama kilimo, biashara na elimu.
Programu ya Mundombinu ya
Masoko, Uongezaji thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF) inagharamiwa
na Serikali ya Tanzania ikishirikiana na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya
Kilimo (IFAD) na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDB) chini ya uratibu wa Ofisi
ya Waziri Mkuu. Lengo likiwa ni kuongeza kipato kwa wakulima na kuchangia
katika kuboresha uhakika wa chakula kwa kaya zenye kipato cha chini hasa maeneo
ya vijijini.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.