WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema safari ya Watanzania kuachana na nguo za
mitumba imewadia kutokana na uwepo wa viwanda vya kutengeneza nguo
nchini.
Pia
amesema uwepo wa viwanda hivyo utasaidia wakulima wa pamba kupata soko
la uhakika hivyo amewataka walime pamba ya kutosha ili viwanda vipate
malighafi.
Waziri
Mkuu alitoa kauli hiyo jana (Jumamosi, Julai 15, 2017) wakati
alipotembelea kiwanda cha nyuzi cha Namera kilichoko Gongo la Mboto na
kiwanda cha nguo cha Nida kilichopo Ubungo Dar Es Salaam.
Alisema
viwanda vya kutengeneza nguo nchini ni ushahidi tosha kwamba nchi iko
njiani kuondokana na matumizi ya nguo za mitumba kwa kuwa nguo nyingi
zitakuwa zinatengenezwa nchini, hivyo kupatikana kwa bei nafuu.
Alisema
kwa sasa wanunuzi wa pamba hawana sababu ya kwenda kuuza nje ya nchi na
badala yake wauze katika viwanda vya ndani ili vizalishe nguo za
kutosha zitakazouzwa nchini kwa gharama nafuu.
“Pamba
yote inaweza kuchakatwa nchini, hivyo hakuna haja ya kuiuza nje ya
nchi. Natoa wito kwa wakulima wetu wa pamba walime mazao ya kutosha kwa
sababu soko la uhakika ipo na hii ndio safari ya mwisho ya mitumba.”
Awali Waziri
Mkuu alitembelea kiwanda cha saruji cha Lake kinachozalisha saruji ya
nyati ambapo aliwapongeza wawekezaji wote nchini kwa kuunga mkono
jitihada za Rais Dkt. John Magufuli za kuifanya Tanzania kuwa ya uchumi
wa viwanda.
Katika
kiwanda hicho ambacho kinazalisha tani 700,000 kwa mwaka kimeajiri watu
2000 na kinalipa kodi ya sh. bilioni 81.312 kwa mwaka, Waziri Mkuu
aliwataka watumishi wake wawe waaminifu, wafanye kazi kwa weledi na wawe
waadilifu.
Pia
Waziti Mkuu alitoa wito kwa wamiliki wa viwanda vyote nchini
kuhakikisha wanatoa kipaumbele cha ajira kwa wananchi waishio katika
maeneo ya karibu na viwanda sambamba na kulipa kodi kwa wakati na kwa
viwango sahihi.
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.