Thursday, August 3, 2017

WAZIRI JENISTA AKUTANA NA MWAKILISHI MKAZI WA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA UNICEF MS. MANIZA ZAMAN.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Mb) Jenista Mhagama akutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa UNICEF Tanzania Ms. Maniza Zaman Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam Agosti 3, 2017.

Waziri Jenista pamoja na masuala mengine amelishukuru Shirika la Umoja wa Mataifa (UNICEF) kwa kushirikiana na Serikali ya Awamu ya Tano katika utekelezaji wa Programu ya Kitaifa ya Masuala ya Kijamii (National Frame -work Social Protection) na mapitio ya utengenezaji wa Sera ya Hifadhi ya Jamii (Social Security Policy) na  kueleza kuwa Serikali imeguswa na jitihada za UNICEF kwa kuunga mkono jitihada za serikali katika Nyanja hii.

Ms. Maniza amesema “UNICEF ina mipango mbalimbali inayotaka kutekeleza kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania mipango hiyo ni pamoja na kuboresha masuala ya Watu Wenye Ulemavu, Hifadhi ya Jamii na kuangalia nmna ya kuwainua Vijana katika sekta mbalimbali ili waweze kujikwamua kimaendeleo na kusisitiza kuwa vijana ndio taifa la kesho hivyo UNICEF itaangalia namna ya kutekeleza mipango hii kwa Tanzania”. 

“Tumeweza kuandaa makongamano na majukwaa ya wahariri kutoa elimu kupitia Vyombo vya Habari, Viongozi wa Dini kuhusu masuala ya Hifadhi ya Jamii, Watu Wenye Ulemavu na mambo menginine nchini Uganda na Brazili ambapo UNICEF imefanikiwa kwa asilimia 80 hivyo tunaamini Tanzania pia inaweza kuanzisha majukwaa kama hayo katika kuboresha masuala ya watoto hapa nchi kwa kushirikiana na UNICEF” alisisitiza Ms. Maiza.

Jenista amemuahidi Mwakilishi Mkazi Ms. Maiza kuandaa mazungumzo ya pamoja kwa kushirikiana na Wizara na sekta nyingine ili kuweza kuzungumzia masuala hayo kwa kina na kuangalia namna ya kuyatekeleza. 

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.