Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora amesema ilikupunguza
madhara ya maafa inahitajika utashi wa kisiasa, uelewa wa umma, elimu ya kisayansi,
mifumo ya tahadhari ya awali katika kujiandaa na kukabili maafa.
Alisema
hayo alipo kua aki hutubia kikao kazi cha kwanza cha Jukwaa la Taifa la
Usimamizi wa Maafa kilichofanyika tarehe 22 Januari mwaka 2018 katika ukumbi wa
Mt. Meru Benki Kuu jijini Dar-es-salaam.
“Hatua hii ni muhimu kwa kuwa nchi yetu imeku wa
ikikumbwa na maafa mbalimbali ikiwemo tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera
mwezi Septemba, 2016 na maafa ya mvua yanayo endelea hivi sasa katika maeneo mbalimbali”
alisema Prof. Kamuzora.
Aidha,
alisisitiza vyombo vinavyo simamia sheria za mazingira kuwa makini katika kuhakikisha
utunzaji wa mazingira ili kuzuia majanga yanayopelekea maafa, na ni jukumu la
kila mtanzania sio tu serikali kufanyia kazi mazingira, uchumi na elimu ili kuzuia
majanga Pia mfumo wa ujenzi ufuate utaratibu ili kujiandaa kuzuia maafa.
Jukwaa
hilo lililoshirikisha wataalamu kutoka sekta mbalimbali ili kusaidia ujuzi na rasilimali
zinazohitajika kwa kujumuisha upunguzaji wa madhara ya maafa katika sera ya Mipango
ya maendeleo, litachangia kikamilifu ongezeko la kujitolea kwa Wizara, Idara na
Mashirika, MamlakanaSerikalizaMitaa, Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Taasisi za Elimu,
Kidini, asasi za kiraia na Sekta binafsi na vyombo vya habari katika shughuliza
usimamizi wa maafa, alisema Prof.Kamuzora.
“Wajibuwa
Jukwaa la Usimamizi wa Maafa ni pamoja na; kushughulikia changamoto za kijamii,
kiuchumi na mazingira ili kupunguza madhara ya maafa katika mipango ya sera za maendeleo
ya taifa, kutumikia kama kichocheo cha majadiliano ya kitaifa na kufikia makubaliano
pamoja na kuainisha vipaumbele usimamizi wa maafa na Kushawishi upatikanaji wa rasilimali
kutoka kwa wafadhili kwa kueleza umuhimu wa kuunga mkono na ushirikiano katika usimamizi
wa maafa na misaada kibinadamu”. aliainisha Prof. Kamuzora.
Kikao
kazi hicho kilijadili masuala mbalimbali ambayo yamekuwa yakitekelezwa na wadau
kwa ajili ya kuimarisha usimamizi wa maafa nchini. Masuala hayo ni pamoja na Mkakati
wa Upunguzaji wa Madhara ya Maafa wa Sendai 2015-2030 ambao ulianzia katika ngazi
ya mataifa, Afrika na sasa kufikia katika ngazi ya nchi na hadi kufikia ngazi ya
mkoa na vijiji.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.