*Ni baada ya kupata soko kubwa nchini China
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya China imetoa fursa ya kufungua
soko la muhogo mkavu kutoka Tanzania, tukio ambalo linafungua ukurasa
mpya wa zao la muhogo kuwa miongoni mwa mazao ya biashara.
Waziri
Mkuu ameyasema hayo leo (Ijumaa, Juni 29, 2018) bungeni jijini
Dodomakatika hotuba yake aliyoitoa wakati wakuahirisha Mkutano wa 11 wa
Bunge.
Amesema
ili kuwezesha wakulima na wafanyabiashara wa Tanzania kunufaika na
fursa hiyo, Mei, 2018 ulisainiwa mkataba kati ya Serikali ya Tanzania na
Serikali ya China kuruhusu bidhaa za muhogo mkavu kutoka Tanzania
kuingia katika soko la China.
Amesema
kufuatia hatua hiyo, mwezi huu wa Juni 2018, tani 74 za muhogo mkavu
kutoka Tanzania zimeingia China kupitia Bandari ya Qingdao iliyopo
katika jimbo la Shandong.
Hata
hivyo, Waziri Mkuu amesema kiasi cha muhogo kilichofanikiwa kuingizwa
katika soko la China bado ni kidogo ikilinganishwa na mahitaji ambayo
yanazidi tani 150,000 kwa mwaka.
Pia,
Waziri Mkuu ametoa wito kwa Watanzania wachangamkie fursa ya kilimo cha
muhogo ambacho kimeonesha kuwa na tija kubwa, pia amevitaka vituo vya
utafiti wa kilimo viwawezeshe wakulima kupata mbegu bora na mbinu za
kisasa ili waongeze uzalishaji na kukidhi mahitaji ya soko hilo.
Waziri Mkuu amesema kutokana na zao la muhogo kuonekana kuwa na matumizi menginezaidi ya chakula, Serikali inaendelea kuvutia uwekezaji wa viwanda vya kuchakata muhogo na kuzalisha bidhaa mbalimbali.
Katika hatua nyingine, Waziri
Mkuu amesema mfumo wa Stakabadhi Ghalani kwamba umekuwa na mafanikio
katika maeneo mengi nchini kwa sababu wakulima wadogo na wa kati wapo
kwenye ushirika, hivyo kuwa na nguvu ya soko na bei nzuri ya mazao yao.
“Mathalani, kwa kutumia mfumo huo, mwezi huu bei ya ufuta imeongezeka kutoka shilingi1,500
hadi shilingi 2,800 kwa kilo na kuua mfumo usio rasmi wa uuzaji wa zao
hilo ujulikanao kama ‘chomachoma’ ambao ulimpunja mkulima kwa ujazo na
bei,” amesema.
Aidha,
Waziri Mkuu amesema mfumo huo unasaidia kuzuia upotevu wa mazao
unaotokana na uhifadhi dhaifu, pia unasaidia kuhifadhi mazao ili
kusubiri kuuza wakati muafaka na kuyaongezea thamani mazao kabla ya
kuyauza.
Hata
hivyo, Waziri Mkuu amesema Serikali imeendelea kuchukua hatua
mbalimbali kuhakikisha kuwa mfumo huo unatekelezwa kikamilifu na kuleta
tija kwa wakulima.
Amesema
hatua hizo ni pamoja na ushirikishwaji wa wadau, kuimarisha ushirika,
kuweka miundombinu ya masoko na kuboresha muundo wa taasisi na
vitendeakazi vya Bodi ya Stakabadhi za Ghala.
Waziri
Mkuu ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa watendaji Serikalini
kuhakikisha kuwa mazao mengi zaidi yanaingizwa katika stakabadhi za
ghala ili kuwe na tija kwa wakulima.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.