WAZIRIMKUU
Kassim Majaliwa amewataka wataalamu wa sekta za kilimo, mifugo na maji
watumie taarifa za hali ya hewa zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa
Tanzania (TMA) ili waongeze ufanisi katika utendaji kazi wao.
Ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Juni 27, 2018) wakati akizinduavituo
51 vya kufuatilia taarifa za hali ya hewa, vituo 15 vya haidrolojia,
kanzidata ya taarifa za hali ya hewa na kituo cha operesheni na
mawasiliano ya dharura wilayani Bahi, Dodoma.
Amesemakuwa
kuongezeka kwa vituo vipya vya kisasa vya ufuatiliaji wa mwenendo wa
hali ya hewa kumeboresha uhakika wa utabiri kutoka asilimia 81 hadi 87
kama inavyoshuhudiwa kwenye taarifa zinazotolewa katika siku za hivi
karibuni. “Hivi sasa tukiambiwa kwamba mvua itanyesha katika maeneo
fulani tunakuwa na uhakika kwa asilimia 87 ya utabiri huo,”.
“Vituo
hivi ni muhimu katika kuimarisha uwezo wa nchi wa utoaji wa huduma za
hali ya hewa na haidrolojia kwa ajili ya shughuli za maendeleo na
kuongeza ufanisi katika utoaji wa tahadhari za awali za majanga
yanayosababishwa na hali mbaya ya hewa na mabadiliko ya tabianchi,”.
Amesema
kupitia mradi huo uliofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa (UNDP) Serikali imeweza kufungua vituo 51 vya kisasa vya hali ya
hewa katika maeneo mbalimbali nchini na vituo 15 vya kupima ujazo wa
maji kwenye mito iliyopo kwenye mabonde ya Pangani, Ruvuma na Pwani ya
Kusini ambavyo vinajiendesha vyenyewe.
“Pia,
mradi huu umeiwezesha Serikali kuanzisha kanzidata ya takwimu na
taarifa za mafuriko na ukame na taarifa za hali ya hewa na
kuondoa ucheleweshwaji wa kupata takwimu au taarifa kutoka Wizara moja
kwenda Wizara nyingine,” amesema.
Hata
hivyo, Waziri Mkuu ameziagiza Wizara ya Maji na Umwagiliaji na Wizara
ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano zitenge fedha kwenye bajeti zao ili
ziweze kufuatilia na kusimamia mradi huo baada ya wafadhili kumaliza
muda wao.
Waziri
Mkuu amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John
Magufuli, itaendelea kushirikiana na washirika wa maendeleo katika
kuhakikisha kuwa vituo na mifumo iliyowekwa inafanya kazi ipasavyo kwa
usimamizi bora ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Uzinduzi
huo umehudhuriwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,
Vijana, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Bibi Jenista Mhagama, Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe na Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.