*Asema kukamilika kwa taasisi hiyo kutakuwa na manufaa makubwa kwa jamii
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amefungua
Jengo la Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia (KIST), wilaya ya
Magharibi ‘B’ lililojengwa kwa ghararama ya sh. bilioni 4.2.
Afungua
jengo hilo leo (Jumanne, Januari 8, 2019) ikiwa ni sehemu ya
maadhimisho ya sherehe za miaka 55 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
yaliyotokea Januari 12, 1964.
Waziri
Mkuu amesema kukamilika kwa Jengo la taasisi hiyo kuna manufaa makubwa
kwa jamii ikiwemo kutoa elimu ya ufundi itakayowasaidia vijana kujiajiri
na kuondokana na utegemezi.
“Kusaidia
azma ya Serikali ya kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025 na msukumo
katika sekta ya viwanda kwa vijana kujiajiri na kuajiriwa katika sehemu
mbalimbali pamoja na Serikalini.”
Amesema
manufaa mengine ya KIST ni kutoa mafunzo ya fani mbalimbali
zinazokwenda sambamba na mabadiliko ya ulimwengu katika Nyanja za
sayansi, teknolojia na ualimu.
Kadhalika,
Waziri Mkuu ameutaka uongozi wa KIST ubuni mbinu mbalimbali na utafute
miradi mingine ya ujenzi itakayosaidia kuwa na miundombinu ya kisasa ya
kutolea elimu.
Amesema
uongozi wa taasisi hiyo hauna budi kuweka mikakati ya kushirikiana na
taasisi nyingine zinazotoa mafunzo ya ufundi ndani na nje ya nchi ili
kubadilishana uzoefu.
Waziri
Mkuu amesema kulingana na maendeleo ya kiteknolojia na mahitaji ya soko
uongozi wa KIST ujipange kutoa mafunzi ya biomedical Engineering na
kuimarisha mafunzo ya matengenezo ya ndege na urubani katika ngazi ya
stashahada.
Awali,
Waziri wa Elimu na Mafunzi ya Amali, Riziki Pembe Juma alisema Wizara
yake itaendeleza taasisi hiyo ili kuwaendeleza vijana na baadae waweze
kujiajiri na kuajiri.
Alisema
vijana wanaohitimu mafunzo ya fani mbalimbali katika taasisi hiyo
wanapewa mikopo ya masharti nafuu na Serikali baada ya kujiunga kwenye
vikundi.
Waziri
Huyo, alisema wahitimu hao kabla ya kupewa mikopo wanaandika andiko la
miradi ambayo watakwenda kuitekeleza ambapo tayari vikundi zaidi ya 10
vya vijana vimeshawezeshwa.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.