WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amekutana
na kufanya mazungumzo wa wajumbe wa Bodi ya Mishahara na Maslahi katika
Utumishi wa Umma na ameitaka ifanye kazi kwa weledi.
Ameiagiza
ifanye marekebisho ya maslahi kulingana na mazingira ya mtumishi,
akitolea mfano kada za elimu, afya, kilimo na mifugo ili yalingane na
kazi wanazozifanya.
Amekutana
na wajumbe wa bodi hiyo leo (Alhamisi,Januari 24, 2019) katika kikao
kilichofanyika kwenye makazi ya Waziri Mkuu Oysterbay jijini Dar es
Salaam.
Waziri
Mkuu amesema Serikali ina nia njema ya kuhakikisha mishara na maslahi
ya watumishi wa umma nchini yanaboreshwa, hivyo ameiagiza bodi hiyo
ifanye kazi kwa bidii.
Amesema
Serikali imeunda bodi hiyo ili kupata ushauri utakaotokana na tathmini
sahihi ya nini Serikali inatakakiwa kufanya ili kuboresha utendaji wa
watumishi wa umma nchini.
Serikali inaimani kubwa na wajumbe wote wa bodi hiyo kutokana na uzoefu walionao kwenye utumishi wa umma.
“Tunataka
muongozo mzuri wa kuwafanya watumishi wa umma wafanye kazi yao kwa
waledi bila ya kuwa na vishawishi vya aina yoyote ikiwemo kuomba na
kupokea rushwa.”
Amesema
Serikali inataka kila mtumishi wa umma anawajibika ipasavyo katika
kuwatumikia wananchi mambo ambayo yatakuwa yameimarishwa kutokana na
upatikanaji wa maslahi mazuri. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.