WAZIRI
Mkuu Kassim Majaliwa amesema Taifa limepoteza kijana aliyekuwa msatari
wa mbele kuwahamasisha vijana wajitambue wawe wazalendo kwa nchi yao na
watambue fursa za maendeleo zilizopo na wasiwe walalamikaji.
Ameyasema
hayo leo (Jumatano, Februari 27, alipokwenda kuhani msiba wa aliyekuwa
Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba
kwa niaba ya Serikali, nyumbani kwa wazazi wa marehemu Mikocheni jijini
Dar es Salaam.
Waziri
Mkuu amesema vijana nchini walikuwa na kiongozi aliyekuwa akiwaongoza
kwa kuwafungua kimawazo na kuwaonesha fursa mbalimbali zitakazowawezesha
kuwakwamua kifikra na kiuchumi ili waweze kujitegemea.
Waziri
Mkuu amesema msiba huo ni wa wote kwani marehemu amefanya kazi kubwa ya
kushirikiana na Serikali kuhamasisha vijana kujitambua na kutambua
fursa zilizpo na kuzifanyia kazi. “Ruge ametoa mchango mkubwa kwa Taifa
Amesema
marehemu Ruge katika kipindi cha uhai wake amefanya kazi kubwa kwa
upande wa Serikali, kuanzia awamu ya nne hadi ya tano hususani katika
suala la kuhamasisha vijana kujikwamua na kutokuwa wategemezi.
Pia,
Waziri Mkuu amesema historia yake inaeleza namna alivyozunguka nchi
nzima na kukutana na makundi ya vijana mbalimbali na kuwaelimisha namna
ya kutambua fursa zilizopo nchini huku akiwahamasisha wawe wazalendo.
"Marehemu
alikuwa akitoa hadi fedha zake binafsi kwa ajili ya kuwawezesha vijana
hasa wale ambao hawakuwa na uwezo wa kiuchumi ili nao washiriki katika
shughuli mbalimbali za ujasiriamali na hatimaye waondokane na
utegemezi.”
Kadhalika,
Waziri Mkuu ametoa wito kwa wazazi, watoto wa marehemu pamoja na
wananchi kwa ujumla waendelee kuwa na subira na watulivu katika kipindi
hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao.
(mwisho)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.