Mkurugenzi
wa Idara ya Uratibu wa Shughuli za Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy
Matamwe akimkabidhi cheti mmoja wa washiriki wa mafunzo ya Afya Moja katika
kuwafundisha wanafunzi wa ngazi ya Stashahada na Astashahada, mjini Morogoro tarehe 13 Aprili,
Na.
OWM, MOROGORO.
Mtandao wa Afya
moja kwa nchi za Afrika mashariki, Kati na Magharibi (OHCEA) umeendesha mafunzo
ya Dhana ya Afya moja kwa wanafunzi wa ngazi ya Stashahada na Astashahada kutoka vyuo vya kwenye sekta za Afya ya
Binadamu, Mifungo, Wanyamapori na Mazingira. Tanzania imekuwa nchi ya kwanza
Duniani kufundisha Dhana hiyo katika ngazi hizo za taaluma, kwa kuwa nchi nyingine duniani hufundisha tu kwa ngazi ya Shahada na
Shahada ya Uzamivu masuala ya Afya moja.
Dhana ya Afya moja
ambayo ni ushirikishwaji wa pamoja sekta
ya Afya ya Binadamu, Wanyamapori, Mifugo, Kilimo na mazingira katika
kujiandaa, kufuatilia na kukabili magonjwa yatokayo kwa wanyama kwenda
kwa binadamu ama kinyume chake. Wataalamu hao wamepata mafunzo hayo kwakuwa wapo
karibu sana na jamii na pindi utokeapo
mlipuko wa ugonjwa ndio huwa kikosi kazi cha
kwanza na mstari wa mbele kuwa
eneo la tukio katika kufuatilia na kukabili
milipuko, kabla ya wataalamu wengine kushiriki kikamilifu.
Akiongea wakati wa kufunga Warsha ya kufanya tathmini ya namna wakufunzi wanavyotumia mitaala ya
Afya Moja katika kuwafundisha wanafunzi wao wa ngazi ya Stashahada na Astashahada, tarehe 13 Aprili, Mjini
Morogoro, Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Shughuli za Maafa, Ofisi ya Waziri
Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe alifafanua kuwa mafunzo hayo yanajenga kikosi kazi
imara chenye kuchagiza shughuli za Afya moja hapa nchini.
“Katika kuimarisha Afya ya Binadamu pamoja na Afya ya mifugo na
wanyamapori, kwa kutumia Dhana ya Afya moja, ninafarijika kwa jitihada hizi za kuwajengea uwezo Wataalamu
wa sekta za Afya katika ngazi ya Stashahada na Astashahada pamoja na wakufunzi wao,
kwa kuwa tunaandaa rasilimali watu ya kuweza kuwa na uwezo wa kujiandaa,
kufuatilia na kukabili magonjwa kwa Dhana ya Afya moja. Alisema Matamwe.
Wakiongea kwa nyakati tofauti waratibu wa mafunzo hayo Profesa; Japheti Killewo na Profesa. Robinson
Mdegela walifafanua kuwa tayari mitaala ya Afya moja kwa ngazi ya stashahada na
astashahada imekamilika, lakini wakati taratibu za kuingiza masuala ya Afya moja zitakamilika hivi
karibuni katika mitaala ya ngazi ya
stashahada na Astashahada wameamua kufanya mafunzo hayo ili wakufunzi kujifunza
kwa vitendo juu ya kufundisha masuala ya Afya moja lakini pia na kuwaandaa
wanafunzi watakao fundishwa kwa kutumia
mitaala hiyo.
Aidha waratibu hao walibainisha kuwa wanafunzi hao wakiweza kuielewa vizuri dhana ya Afya moja
watatumika vyema kuielimisha jamii juu ya masuala ya Afya Moja, na nchi yetu itaweza kuzuia maambukizi ya
magonjwa ya mlipuko hususani yale yatokayo kwa wanyama kwenda kwa binadamu na
pia kupunguza usugu wa madawa kwa sababu wataweza kuongeza ushirikiano,
mawasiliano na uratibu baina ya sekta husika.
Mafunzo hayo yaliyowajumuisha zaidi ya
wanafunzi 210, wa ngazi ya astashahada na ngazi ya cheti kutoka Chuo Kikuu cha
Afya na Sayansi Shirikishi, Muhimbili, SUA, Wakala wa Vyuo vya Mafunzo ya
Mifugo Morogoro, Chuo cha Afya cha Kilosa, Chuo cha Wanyamapori Pasiansi na
Chuo cha Wanyamapori Mweka,
Aidha,
wakufunzi zaidi ya 30 wameshiriki kutoka Chuo Chuo Kikuu cha Afya na
Sayansi Shirikishi Muhimbili, Chuo kikuu cha Kilimo Sokoine, Vyuo vya Afya
Lindi, Mafinga, Kilosa, Mtwara, Singida, Kagemu, Mirembe, Wakala wa Vyuo vya
Mafunzo ya Mifugo Morogoro, Temeke, Tengeru, Buhuri, pamoja na Vyuo vya Taaluma
ya Wanyamapori , Pasiansi na Mweka.
Mafunzo hayo yameratibiwa na Chuo
Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili na Chuo kikuu cha Kilimo Sokoine kwa
kushirikiana na USAID,
kupitia vyuo vikikuu vya MINNESOTA na
Tufs vya nchini Marekani
MWISHO.
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.