Na. OWM, ARUSHA
Kwa mara ya kwanza Barani
Afrika na kwa mara ya kwanza katika utendaji wake Benki ya Dunia, kwa
kushirikiana na serikali ya Tanzania kupitia
Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Menejimenti ya Maafa, wamefanya zoezi
la mezani la Kupima uwezo utekelezaji wa Mpango wa Kujiandaa na kukabili Maafa kwa kutumia maafa
ambayo yamepata kutokea kweli hapa nchini, ambapo zoezi hilo limetumia maafa ya
mafuriko mkoani Morogoro, wilayani Kilosa kwa mwaka 2014 na mwaka 2016. Mazoezi
mengine ya mezani ya kujiandaa na kukabli maafa hutumia matukio ya maafa ya
kinadharia na hufanyika kabla ya maafa kutokea.
Mtaalam Mwandamizi wa
menejimenti ya Maafa, kutoka Benki ya Dunia, Elad Shenfeld, amebainisha mambo
matano ambayo yameifanya Benki hiyo kuichagua Tanzania kuwa nchi ya kwanza
barani Afrika kufanya zoezi hilo, kuwa
ni Uwajibikaji na uwazi katika kuratibu shughuli za menejimenti ya maafa unaofanywa na serikali ya Tanzania kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu,
Idara ya Menejimenti ya Maafa, uwepo wa
Sheria ya Maafa, ambayo ni Sheria ya Menejimenti ya Maafa ya mwaka 2015, Mpango
wa Taifa wa kujiandaa na Kukabili maafa wa mwaka 2012, Uwezo, Weledi na Uwajibikaji
wa watumishi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa katika menejimenti ya maafa pamoja na Ushirikiano mzuri wa serikali ya
Tanzania na Benki ya Dunia Tanzania na Kanda ya Afrika katika masuala ya menejimenti
ya maafa nchini.
Akiongea mara baada ya
kufunga zoezi hilo mjini Arusha, tarehe 16, Julai, 2019, Mkurugenzi wa Idara ya
Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe amebainisha
kuwa nchi nyingi barani Afrika ikiwemo Tanzania zimekuwa zikifanya mazoezi ya kujiandaa na kukabili maafa kwa
kutumia nadharia za maafa yanoyoweza kutokea, lakini zoezi hilo ni tofauti kwani limejikita kwa maafa ambayo
yamewahi kutokea kweli hapa nchini.
“Zoezi hili ambalo limeangalia maafa ya mafuriko
yaliyotokea, Kilosa kwa mwaka 2014 na 2016,
litatusaidia kuimarisha mifumo yetu serikalini ya kujiandaa na kukabili
maafa ya mafuriko na majanga mengine kwani tumejua ni wapi hatukufanya vizuri
na namna gani ya kuboresha mifumo yetu,
lakini pia zoezi hili litawajengea uwezo waratibu wa maafa serikalini na
wataalam kutoka katika mashirika yasiyokuwa ya serikali katika kushirikiana na
serikali katika kujiandaa na kukabili maafa yatapotokea” Alisema Matamwe.
Aidha, washiriki wa zoezi
hilo waliweza kutoa uzoefu wao katika kujiandaa na kukabili maafa ya mafuriko
ambayo yalitokea wilayani Kilosa kwa
mwaka 2014 na 2016. Washiriki hao kwa nyakati tofauti walibainisha kuwa
wamejifunza kutoka mafuriko ya Kilosa kuwa ipo haja ya kila Serikali za mitaa
na Taasisi za serikali pamoja na wadau wa menejimenti ya maafa kutenga bajeti
kwa ajili ya masuala ya usimamizi wa shughuli za maafa.
Zoezi hilo lililofanyika
kwa muda wa siku mbili tarehe 15 hadi 16, Julai, 2019, liliwashirikisha wataalam wa usimamizi wa
shughuli za maafa kutoka serikalini na mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali, limeratibiwa
na Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Menejimenti ya Maafa, kwa ufadhili wa Benki ya Dunia.
MWISHO.
|
Mkurugenzi wa Idara ya
Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe (mwenye tai nyekundu), kushoto ni
kwake Mkurugenzi Msaidizi wa Ofisi hiyo (Utafiti na Mipango), Bashiru Taratibu,
kushoto kwake ni Wawezeshaji kutoka
Benki ya Dunia, Elad Shenfeld, Adam Mc Allister na HugoWesley, wakati wa zoezi la mezani la kupima uwezo wa
utekelezaji wa Mpango wa Kujiandaa na Kukabili Maafa nchini, kwa taasisi za serikali na mashirika yasiyo ya
kiserikali yanayohusika katika menejimenti za maafa , mjini Arusha tarehe 16
Julai, 2019.
|
|
Mkurugenzi, Idara ya
Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe akiongea na
wataalam kutoka taasisi za serikali na mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali
yanayohusika katika menejimenti za maafa wakati wa zoezi la mezani la kupima
uwezo wa Utekelezaji wa Mipango ya menejimenti ya maafa nchini, mjini Arusha, tarehe
16 Julai, 2019.
|
|
Mkurugenzi Msaidizi
(Utafiti na Mipango), Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri
Mkuu Bashiru Taratibu akisisitiza jambo kwa wataalam kutoka taasisi za serikali
na mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali yanayohusika katika menejimenti za maafa
wakati wa zoezi la mezani la kupima
uwezo wa wa Utekelezaji wa Mipango ya , tarehe
16 Julai, 2019.
|
|
Mtaalam wa Shughuli za
Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Menejimenti ya Maafa, Charles Msangi
akieleza jinsi ofisi hiyo inavyoratibu shughuli za maafa wakati wa zoezi la mezani la kupima uwezo wa Utekelezaji
wa Mpango wa Kujiandaa na Kukabili Maafa nchini, kwa taasisi za serikali na
mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali yanayohusika katika menejimenti za maafa
wakati wa mjini Arusha, Julai 16, 2019.
|
|
Kamishina Msaidizi wa
Jeshi la Polisi kutoka makao makuu ya Jeshi la Polisi nchini, Balele Edward,
akiandika katika moja ya nyenzo za kujifunzia wakati wa zoezi la mezani la
kupima uwezo wa Utekelezaji wa Mpango wa Kujiandaa na Kukabili Maafa nchini kwa
taasisi za serikali na mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali yanayohusika katika
menejimenti za maafa, mjini Arusha Julai 16, 2019, zoezi hilo limeratibiwa na
Ofisi ya Waziri Mkuu kwa ufadhili wa Benki ya Dunia.
|
|
Baadhi ya washiriki kutoka taasisi za serikali na
mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali yanayohusika katika menejimenti ya maafa
wakijadiliana wakati wa zoezi la mezani la kupima uwezo wa utekelezaji wa Mpango wa Kujiandaa na Kukabili Maafa nchini,
mjini Arusha Julai 16, 2019, zoezi hilo limeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu
kwa Ufadhili wa Benki ya Dunia |
|
Baadhi ya washiriki kutoka taasisi za serikali na
mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali yanayohusika katika menejimenti ya maafa
wakijadiliana wakati wa zoezi la mezani la kupima uwezo wa utekelezaji wa Mpango wa Kujiandaa na Kukabili Maafa nchini,
mjini Arusha Julai 16, 2019, zoezi hilo limeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu
kwa Ufadhili wa Benki ya Dunia |
|
Mwezeshaji kutoka Benki ya Dunia Adam Mc Allister
akisisitiza umuhimu wa Mipango ya Menejimenti ya Maafa kwa taasisi za serikali na mashirika yasiyo kuwa
ya kiserikali yanayohusika katika menejimenti za maafa wakati wa zoezi la mezani la kupima Utekelezaji wa Mpango
wa Kujiandaa na Kukabili Maafa nchini, mjini Arusha, Julai 16, 2019, zoezi hilo
limeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Ufadhili wa Benki ya Dunia.
|
|
Baadhi ya washiriki kutoka
taasisi za serikali na mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali yanayohusika katika
menejimenti ya maafa wakijadiliana wakati wa zoezi la mezani la kupima uwezo wa
utekelezaji wa Mpango wa Kujiandaa na
Kukabili Maafa nchini, mjini Arusha Julai 16, 2019, zoezi hilo limeratibiwa na
Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Ufadhili wa Benki ya Dunia.
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.